Askofu Gwajima: Kamati ya Bunge imenifanya nionekane kama Jitu baya na Korofi, sasa hili ndio lililojiri kikaoni

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,961
141,956
Askofu Gwajima yuko mubashara Rudisha Online tv anatoa ufsfanuzi na kujibu yale yaliyosemwa na kamati e maadili ya bunge.

Updates;

Niliitwa na kamati ya maadili ya bunge na kunihoji yale niliyohubiri Kanisani nami nikawaambia wao hawana mandate ya kuhoji kile kilichotokea Kanisani ambapo niliongea kwa uwezo wa Roho mtakatifu.

Pili, nimeijulisha kamati ya bunge kwamba sisi Kanisa la ufufuo na uzima hatutachanja iwe leo au kesho

Tatu, nimewajulisha kwamba hakuna mtu wa kunizuia na kwamba mtu huyo bado hajazaliwa.

Sasa askofu Gwajima anaelezea umuhimu wa Royal tour inayofanywa na Rais Samia.

Mwisho askofu Gwajima amefanya maombi rasmi kwa Rais Samia, makamu wa Rais Dr Mpango, Waziri mkuu mh Majaliwa na Jaji mkuu Prof Juma.

Tofauti na ibada nyingine leo Askofu Gwajima hajamuombea Spika Ndugai, Naibu spika Dr Tulia wala muhimili wa bunge.

Mwimbo ulioongoza ibada ni " Msalaba mbele dunia nyuma"

=====

#Kutoka_Kanisani_kwa_Gwajima

"Niliitwa na Kamati ya Maadili ya Bunge wengi mliniuliza kimejiri nini nikasema sitosema hadi Kamati iseme na kwasababu imeshasema acha nizungumze kwasababu wameniongelea kama Jitu baya ambalo kama lipo kama lilivyotajwa halitakiwi hata kuwa Kiongozi wa Kanisa

Mimi Mchungaji wa muda mrefu, nilipoitwa kwenye Kamati niliyoitiwa ni kuhusu mahubiri ya Kanisani nikawaambia sidhani kama Kamati mmefanya vizuri maana yote nimeongea Kanisani na hakuna mwenye mamlaka ya kuuliza maswali juu ya Ibada ya Kanisani na imani za Watu

Niliwaambia Kamati ya Maadili ya Bunge mmesema mmesikia nimewaambia Watu wasichanjwe nikasema hiyo haibadiliki milele, nikaweka wazi kwamba sisi Ufufuo na Uzima chanjo ni hiari na sisi tumechagua hatuchanjwi.

Siikupindisha maneno mbele ya Kamati ya Maadili ya Bunge, nilisema sisi Ufufuo na Uzima hatutowaruhusu Waumini kuchanja na sababu zetu ni hatujapata taarifa za kutosha juu ya chanjo, madhara ya chanjo ya muda mfupi, siku zijazo na siku nyingi.

Kama nimeitwa mkorofi ukorofi wangu ni kusimamia ukweli, Kamati ya Maadili ya Bunge wakaniambia jitetee nikasema sina la kujitetea, siwezi kujitetea kwa mahubiri niliyohubiri yanatoka kwa roho mtakatifu, nimefafanua ili mjue Mimi sio mkorofi." Bishop Dr Josephat Gwajima
 
Back
Top Bottom