Gwajima, Polepole na Silaa waitwa Kamati ya Maadili ya CCM

jme

JF-Expert Member
Aug 4, 2013
4,665
4,797
Dodoma. Wabunge watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwamo Mbunge wa Kuteuliwa, Humpherey Polepole watawekwa kikaangoni leo na Kamati ya Maadili ya Wabunge wa CCM kuhojiwa kuhusu masuala tofauti.

Wabunge wengine watakaohojiwa leo ni Askofu Josephat Gwajima (Kawe) na Jerry Silaa (Ukonga) ambao Bunge lilipitisha azimio la kuwasimamisha kwa mikutano miwili kutokana na tuhuma za kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge.

Vilevile, Kamati imependekeza Askofu Gwajima kufikishwa mbele ya kamati ya chama chake CCM na kuhojiwa kuhusu mwenendo wake.

Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ilipendekeza Silaa asimamishwe mikutano miwili ya Bunge la Tanzania na avuliwe uwakilishi kwenye Bunge la Afrika (PAP) kwa madai kuwa anaweza kusema uongo akienda huko.

Kilichomponza Silaa ni kauli yake ya kutaka wabunge wakatwe kodi kwenye mapato yao, jambo lililoelezwa kuwa ni uongo, kwani wabunge wanalipa kodi.

Kwa upande wa Gwajima, atatakiwa kujieleza kuhusu kauli anazozitoa katika Kanisa lake la Ufufuo na Uzima kuanzia Julai 25 mpaka Agosti 15 kuhusu chanjo ya korona.

Chanzo: Mwananchi
 
CCM ina taratibu zake....

Ni mwiko kumpinga MWENYEKITI WETU hadharani kwa njia za kumshambulia ,kedi na kebehi.....

#SiempreCCM
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
#KaziIendelee
 
Askofu Gwajima ana watu

Pole pole ana watu.

Jerry Slaa ana Hoja.
Yes.

Askofu Gwajima ana watu wasiozidi hata elfu 1 - wale waumini kanisani kwake (akiwemo johnthebatist)!

Pole pole ana watu wasiozidi hata 10 (mfano Musiba, johnthebaptist, Bashiru, Bashite, Mjalalani na wengineo wa aina hii)

Jerry Slaa ana Hoja, tena ni hoja nzito na yenye mashiko!
 
Back
Top Bottom