Askofu Gwajima ashindwa kutoa ushahidi wa tuhuma zake dhidi ya chanjo

ngebe

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
1,789
5,105
Katika kikao kinachoendelea Bungeni leo agosti 31, Kamati ya maadili iliyowahoji Askofu Josephat Gwajima na mbunge Jerry Slaa imetoa ripoti yake na mapendekezo ya adhabu.

Kwa upande wa askofu josephat Gwajima, Kamati imesema kua ilimtaka atoe evidence juu ya zile tuhuma alizokua akizisema zikiwemo kwamba kuna watu wamepokea hela ili chanjo iingie nchini, Wachoma chanjo watapata madhara baadaye.

baada ya kuambiwa alete ushahidi wake juu ya madai hayo Askofu Gwajima alisema Hayo ni mahubiri ya kiroho hivyo hayapaswi kukosolewa na alivyoendelea kutakiwa atoe evidence za utafiti wake alikaa kimya.

download.jpeg

ikumbukwe Askofu Gwajima aliwahaaidi wahumini wake kwamba atakwenda kuieleza ukweli kamati ya maadili
===

“Askofu Gwajima alishindwa kuthibitisha kauli zake wala hakuwa na ushahidi na kielelezo chochote kama alivyouaminisha umma kuwa anao ushahidi”.

Kufuatia maelezo hayo Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Emmanuel Mwakasaka ameeleza kuwa kamati imemtia hatiani, Mbunge wa Kawe Askofu Gwajima.

Mwenyekiti Mwakasaka, ameeleza kuwa “Askofu Gwajima hakukiri wala kujutia makosa yake, alionyesha dharau na hivyo Kamati imemtia hatiani, Bunge linaazimia kuwa apewe adhabu ya kutohudhuria mikutano miwili mfululizo ya Bunge baada ya kupitisha azimio.”
 
Unapewa msaada wa chanjo 1M na mwenye hizo chanjo. Wakati ukitegemea utaenda sokoni kununua chanjo nyingine say 5M. Dhamira itakusukuma na kukusuta urudi kwa mfadhili anayezalisha na kuziuza hizo alizo kupa za msadaa. Hii si inaweza ikawa ni rushwa inayo tumia ujanjaujanja wa akili kubwa
 
Unapewa msaada wa chanjo 1M na mwenye hizo chanjo. Wakati ukitegemea utaenda sokoni kununua chanjo nyingine say 5M. Dhamira itakusukuma na kukusuta urudi kwa mfadhili anayezalisha na kuziuza hizo alizo kupa za msadaa. Hii si inaweza ikawa ni rushwa inayo tumia ujanjaujanja wa akili kubwa
kwaiyo ulitaka upewe chanjo bure?
 
Kwa hiyo akisimamishwa vikao viwili atàcha kuhamasisha watu wasichanjwe?
 
Katika kikao kinachoendelea Bungeni leo agosti 31, Kamati ya maadili iliyowahoji Askofu Josephat Gwajima na mbunge Jerry Slaa imetoa ripoti yake na mapendekezo ya adhabu...
…je Magufuli alikuwa na ushahidi wa ubaya wa chanjo?
 
Wewe nawe siyo ameshindwa kuthibisha,ungesema akataa kuthibitisha.
Mambo ya rohoni hutambulikana kwa jinsi ya rohoni.
Yuko sawa.
Mambo ya rohoni wakati mwanzo alisema anao ushahidi wa kutosha
 
Wewe nawe siyo ameshindwa kuthibisha,ungesema akataa kuthibitisha.
Mambo ya rohoni hutambulikana kwa jinsi ya rohoni.
Yuko sawa.
Alipokuwa anamla yule demu alikuwa rohoni? Huyo ni msanii kama wasanii wengine usimuhusishe Roho Mtakatifu na ufedhuli
 
Kamati ya Maadili imependekeza vyombo vya Usalama kumchunguza Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima kutokana na kauli alizokiri kutoa Kanisani kwake

Aidha, Chama kilichompa tiketi ya kupata Ubunge (CCM) kimetakiwa kumuwajibisha kwa mujibu wa taratibu zao

Kamati imependekeza Gwajima asihudhurie mikutano miwili ya Bunge mfululizo
 
Back
Top Bottom