Askofu Gwajima atembea tena baada ya kupooza

Askofu Gwajima atembea tena baada ya kupooza

Kipofu wa kiroho hawezi kuelewa kitu,hivyo usibishane naye.

ebu acha kuwa mpuuzi wewe kuna siku atakufungia ndani na kukutia kiberiti ili uende peponi amka wewe usiwe kilaza
 
Nijuavyo mimi hakuna mtu anaweza kujifanya msukule,misukule yote inatengenezwa na watu
na watu wanapata faida kupitia hiyo misukule.
Kitendo cha gwajima kufungua misukule,ni hasara kwa watengenezaji
Hivyo sishangai kuona watu wanatukana humu,kwani wengine wana majeraha ya mali zao kuchukuliwa na kuharibiwa.
wengine wanadandia treni.
Kama mtu huna manufaa binafsi Kwanini upoteze muda kumjadili mtu ambaye kimsingi hajakudhuru.

Mnaodai issue ya Flora na Mbasha,Cha ajabu hapo ni kipi? Wangapi wameachana na wake zao na maisha
yanaendelea,kama mbashaa hakujipanga akadhani kumuoa star ndo umemaliza kila kitu,utakula utalala bure
hilo liwe fundisho kwetu wanaume,kwamba uanaume si suruali bali ni kuwajibika.

Kama Gwajima alikuwa na mapungufu serikali ilitakiwa imshughulikie hata bila kumsema kiongozi mwenzake,
serikali ndo ilimpa Viwanja tajwa wala hakuomba bali walipoona umati pale ubungo unafika hadi barabarani
walimpa eneo hilo kwa muda ili alitumie,na si ajabu kwani chuo cha Tanesco Morogoro
walipewa waislam wakakiendeleza na sasa wanatoa elimu kwa umma na hakuna tatizo.
Shida inajitokeza pale mali ya umma anapopewa mtu binafsi na haina manufaa kwa wananchi.
 
Alivyokuwa kiwete mbona mliamini? Madaktari walidhibitisha alipoteza fahamu, na Madaktari wa jeshi walidhibitisha alikuwa na presha juu sana, hilo linaeza leta kupooza hata upofu. Hao nao hamuwaamini? Sasa kwa sababu mungu amemponya, hamuelewi, muujiza umekuwa kikwazo kwenu . "jiwe walilolikataa waashi, limekuwa jiwe kuu la pembeni" kikwazo kwa wasioamini

yaani wewe kijana kabisa ambae unafaa kuwatoa kweye ujinga watu wazima na wazee yaani wewe ndio punguani wa kwanza sijui wanao watajifunza nini kutoka kwako kichwa maji ww

#Zitto
 
Waliangukialo watapasuka vipandevipande na liwaangukialo litawasaga tikitiki. Hakika Yesu adumu wa kuaminiwa na wengi tunamkiri na kumwamini kuwa ni bwana na Mungu alimfufua kutoka kwa wafu
 
yote n vema
hakuna mwenye akili yoyote yule anayeweza amni.....
Kama na ujasiri wa kumtukana pengo......watawala wanavyodai aliyemjeruhi dr.ulimboka alitokea kwenye kanisa lake((((((kwa mujibu wa kova)))))))))))))))

mbona hajawahi hata siku moja kukubali wala kukanusha

yesu siku hizi amekuwa mtaji...ukiweza cheza vizuri karata yako inalipa saanaaa

Aliyemjeruhi Dr ulimboka kutokea kanisa Lake sio issue. Msaliti wa Yesu alitokea katikati yake, aliyemkata sikio mtu kwa upanga na yesu akaliunga alikuwa Peter
 
Ilikuwa katika ibada ya pasaka ambapo askofu Gwajima akielezea habari ya kupoteza fahamu. Miguu yake ilitetemeka, akasikika akiwaomba wachungaji wake wamshike mkono wa kuume, akisema nataka kutembea, Yesu nimechoka kukalia kiti cha vilema, heri kufa kuliko kukaa hapo. Nimefufua wafu na kuponya wagonjwa siwezi mimi kukaa hapo. Mara akasema, nasikia sauti inasema 'mimi nimeushinda ulimwengu' akaendelea 'roho wa mungu yu juu yangu' ilikua ni jambo la kupendeza sana, Bishop akaanza kutembea mwenyewe. Hallelujah

Msamaha wa pengo ndio umemfanya apone. Pengo ni mtumishi wa mungu kweli kweli! Akuna dini duniani inayofundisha kutukana kama alivyofanya gwajima.
 
Bible inaongelea kuhusu makanisa ya private ??

Luka 9:49 Bwana tulimwona mtu akitoa pepo kwa jina lako, tukamkataza kwa sababu hatuandamani naye.
50. Yesu akasema, msimkataze kwa sababu yeye asiye kinyume chenu yu upande wenu
 
Watanzania tutaelemika lini na kuwaacha kuwapelekea pesa (sadaka) wasanii kama hawa .Hili nalo linahitaji akili kulipambanua kweli kuwa jamaa ni Tapeli Ujinga wetu utatafanya watumwa daima
 
yaani wewe kijana kabisa ambae unafaa kuwatoa kweye ujinga watu wazima na wazee yaani wewe ndio punguani wa kwanza sijui wanao watajifunza nini kutoka kwako kichwa maji ww

#Zitto

Umekosa hoja, niache niendelee na wasiochoka
 
Kutokumjua Mungu na uweza wake ni ujinga, Kutokumwamini ni upumbavu ulio pitiliza!!
Bwn Yesu kuna watu hawaamini hata leo kama alikufa akafufuka!!Mambo ya Mungu ni makubwa kwa akili za kibinadamu
huwezi kuyajua!!
Acha matusi, jifunze neno!!
 
mkuu,wameshashindikana hao,bora jamaa liendelee kukamua pesa

kama una judge ukristo kutokana na haya makanisa ya kisasa utapotea...ila jamaa burudani sana...nimecheki hizo picha nimecheka sana...na ana wafuasi wa kutosha...hahahaa
 
Ndugu yangu nimepokea ujumbe huu hapa chini 👇 kutoka CHRAGG! Tafadhali tuzingatie hili! Beginning of quote! 👉 "This is a very serious warning from UNDP Dar! Beware on Friday 10.04.15, Suspected Somalian terrorist attacks in Dar, Mwanza, Arusha and Mbeya.Try to avoid public gathering places on that day especially hotels. UN Security warning. Pls take extra care and avoid public gathering places. Forward this message to all your friends.". End of message. Tusipuuzie hili. Mungu atulinde! Mungu iokoe Tanzania!
 
Msamaha wa pengo ndio umemfanya apone. Pengo ni mtumishi wa mungu kweli kweli! Akuna dini duniani inayofundisha kutukana kama alivyofanya gwajima.

Amepona kanisani kwake, si kwa pengo, kwanza Catholic hamponyagi wagonjwa, ndio mnaitaga Padre awatie upako wa wafu, mnaambiwa wa kifo chema, halafu mnaitikia amen huku mnalia. Yesu alisema "fufueni wafu, ponyeni wagonjwa, toeni pepo" hakusema wapeni kifo chema... Haloo! Bwana awe nanyiiii!.... Nirudishie huo mbaraka
 
sasa atulie ili kufanya kazi za dini atakuwa na maisha marefu ni ushauri wangu.
 
Amepona kanisani kwake, si kwa pengo, kwanza Catholic hamponyagi wagonjwa, ndio mnaitaga Padre awatie upako wa wafu, mnaambiwa wa kifo chema, halafu mnaitikia amen huku mnalia. Yesu alisema "fufueni wafu, ponyeni wagonjwa, toeni pepo" hakusema wapeni kifo chema... Haloo! Bwana awe nanyiiii!.... Nirudishie huo mbaraka

Gwajima nabii wa uongo....nani alimpa huo uaskofu.?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom