Askofu Gwajima atembea tena baada ya kupooza

Askofu Gwajima atembea tena baada ya kupooza

ukila nguruwe lazima akili yako iwe imevulugwa lazima utaamini hata usanii, yesu aliyatoa mapepo akayarusha kwa nguruwe

Naona umekazana ku copy and paste hiyo post yako! Soma kilichoandikwa na kisha u comment. Huwezi kutumia jawabu kwa kila swali!
 
Ila ukimuangalia usoni hasa mashavu, ni wazi ana mgogoro wa afya!
 
Hata siamini kama bado kuna watu wa aina hii hapa duniani,
pure mazingaombweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, nakumbuka uzi mmoja wa Faizafoxy, wajinga ndio waliwao, na kweli dada Faiza
 
Tasnia ya Maigizo Tz inazidi kukua. Hongereni wasanii

Alivyokuwa kiwete mbona mliamini? Madaktari walidhibitisha alipoteza fahamu, na Madaktari wa jeshi walidhibitisha alikuwa na presha juu sana, hilo linaeza leta kupooza hata upofu. Hao nao hamuwaamini? Sasa kwa sababu mungu amemponya, hamuelewi, muujiza umekuwa kikwazo kwenu . "jiwe walilolikataa waashi, limekuwa jiwe kuu la pembeni" kikwazo kwa wasioamini
 
Eh watu msio na imani mna tabu, Yesu alisema "ikiwa hawatamwamini mussa na manabii, hata mtu akifufuka toka wafu hawatamwamini," Na aliyefufuka toka wafu Ni Yesu mwenye injili, na mnashindwa kuamini. Kufumba na kufumbua Gwajima alikuwa kilema, nanyi mliamini na kufurahi ;Kufumba na kufumbua Gwajima mungu amemsimamisha, hapo hamwamini kwa kuwa hata hamjui nguvu ya mungu anayemtumikia. mlitaka abaki kwenye kiti milele. Imeandikwa "hakuna silaha juu ya mtumishi itakayofanikiwa" poleni kwa mioyo yenu isiyoamini, halafu mnadai mnaeza mkaamini ipo pepo mtakayoenda, mnaingia kwa imani gani, na Mungu mwenye nguvu gani? . Kama hana nguvu ya kukuponya, nguvu ya kukupeleka peponi haitoe wapi?

Niambie km Yesu alishawahi kupomorosha matusi kama Gwajima!
 
Maranyingine watu tunatoa majibu kwa feeling za kijinga sasa cha ajabu hapo ni nini?
Mtu alikuwa hatembei sasa anatembea its just simple like that me sielewi mnabishania na kutukana kwa ajili ya nini?

Mnabishania kutembea kwake? Au mnabishania kusema kwamba ametembea kwa uwezo wa MUNGU?

Sometime watu mnabidi mkue na muwe na akili za watu wazima nashindwa kuwacartegorize umri wenu na uelewa wenu sababu me sijaona chochote cha ajabu mpaka kupelekea kukashfiana imani zenu.
 
ushauri wa bure na wa kitaalam,

gwajima asilazimishe kutembea ili aonekane shujaa,anajiumiza sana

kwa kawaida tatizo la stroke au kiharusi likishatokea madhara yake yana pungua kidogo kidogo.

afanye mazoezi kwa utaratibu kidogo kidogo.mild stroke aliyo ipata effect yake inaindoka taratib.

ajitahidi kunywa sawa alizopewa kuzuia attack nyingine na pia ajitahidi kupumzika, akiwa stressed tena sio vizuri kwa afya yake.

asiji over stretch ili watu wamshangilie.apumzike tu.

na msamaha asisahau kuomba kwa askofu anayetambulika duniani kote,askofu pengo

Wewe nawe unaongea nini? Stroke ilikuwa upande mmoja, huwezi kujitahidi kutembea kama nerves hazijatoa signal, ni sawa na kusema taa inajitahidi kuwaka bila umeme . Aliyoipata ni malignant hypertension, a very serious one. Na Mungu amemponya. Ila wewe unawaamini miungu wako sisi madaktari, mungu akifanya unaanza kuona ni uongo halafu jumapili unabeba misale ya waumini kwenda kwenye masinagogi kumsifu Yesu Kristo,. mwaminini mungu..
 
Ilikuwa katika ibada ya pasaka ambapo askofu Gwajima akielezea habari ya kupoteza fahamu. Miguu yake ilitetemeka, akasikika akiwaomba wachungaji wake wamshike mkono wa kuume, akisema nataka kutembea, Yesu nimechoka kukalia kiti cha vilema, heri kufa kuliko kukaa hapo. Nimefufua wafu na kuponya wagonjwa siwezi mimi kukaa hapo. Mara akasema, nasikia sauti inasema 'mimi nimeushinda ulimwengu' akaendelea 'roho wa mungu yu juu yangu' ilikua ni jambo la kupendeza sana, Bishop akaanza kutembea mwenyewe. Hallelujah

Usanii mwingine bwana ...Huyo aliyekuwa anajifanya hawezi kutembea ili kukwepa kuhojiwa na kuja kutembea ili watu waone kapona.....
Watu waliowekwa upofu hawataona kuwa wanapigwa changa ...... Ametumia Polisi kupata kicky...
 
I stand for Jesus, then I stand for Gwajima as God never ever assemed his sarvant and he will never do to him too
 
Hizi sanaa kwa kupitia jina la Mungu, walau basi kidogo tumuogope na kuuheshimu uumbaji wake.

Mungu wangu! umuheshimu Mungu kwa kuamini kuwa hawezi kumponya mtu! Huu udini wenu utawapeleka jehanam, ni wadini lakini nguvu zake hamziamini. Ngoja nijiepushe nanyi
2.Timotheo 3:5 Wenye mfano wa dini, lakini wakizikana nguvu zake, hao pia ujiepushe nao.
 
Alivyokuwa kiwete mbona mliamini? Madaktari walidhibitisha alipoteza fahamu, na Madaktari wa jeshi walidhibitisha alikuwa na presha juu sana, hilo linaeza leta kupooza hata upofu. Hao nao hamuwaamini? Sasa kwa sababu mungu amemponya, hamuelewi, muujiza umekuwa kikwazo kwenu . "jiwe walilolikataa waashi, limekuwa jiwe kuu la pembeni" kikwazo kwa wasioamini

Pole yenu mnaofuata MIUJIZA makanisani ....Haina tofauti na watu wanaoshangaa mazingaomwe ya cheusi chekundu pale mnazi mmoja
 
I stand for Jesus, hence for Gwajima as I know God had never ever assemed his sarvent and i knonw he will never do to him.
 
Niambie km Yesu alishawahi kupomorosha matusi kama Gwajima!

Aporomoshe, asiporomoshe haimzuii kuwa mtumishi wa Mungu, Mwanadamu huanguka bali Mungu haanguki, hivyo anamwinua tu. gwajima sio yesu lakini huitumia mamlaka ya Yesu. Yesu hakutukana lakini Mungu alimfanya Dhambi, vivyo hivyo gwajima mwenye makosa mungu amemwesabia haki kwa kuwa amemwamini yesu, sijui kama utaelewa hili.
2 Wakorintho 5 :21 Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu , ili sisi tupate kuwa haki ya mungu katika yeye
 
Usanii mwingine bwana ...Huyo aliyekuwa anajifanya hawezi kutembea ili kukwepa kuhojiwa na kuja kutembea ili watu waone kapona.....
Watu waliowekwa upofu hawataona kuwa wanapigwa changa ...... Ametumia Polisi kupata kicky...

Asiyeamini hakosi sababu, sasa unamaanisha polisi waliomwita wenyewe, walikusudia kumtengenezea muujiza feki, pia madaktari walidhibitisha pia wametumia taaluma yao kumtengenezea muujiza feki, hapo nimekuelewa
 
Pole yenu mnaofuata MIUJIZA makanisani ....Haina tofauti na watu wanaoshangaa mazingaomwe ya cheusi chekundu pale mnazi mmoja

Hayo ni mawazo yako, lakini kama ni injili ya Yesu aliyefufuka, huwezi itenganisha na miujiza.
Marko 16 :17 - 18
Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio, kwa jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya, watashika nyoka, hata wakinywa kitu cha kufisha hakitawazuru kabisa, wataweka mikono juu ya wagonjwa nao watapata afya.
 
Dah,vituko haviishi duniani.Huyu jamaa nikimuona najisikia kucheka tu,cheki pozi aliloweka kwenye picha ya mwisho hapo. Teh teh teh
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom