Fidelisfcm
JF-Expert Member
- May 27, 2017
- 293
- 101
Ni wapi ameruhusu hayo yote uliyoyasema. Sijawahi kusikia kiongozi yeyote akikubali uchafu unaoutaja wewe.Kwa askofu, mimba ndio dhambi wala sio uzinzi au uasherati.
Ina maana, ukitumia condom au madawa ya kuzuia mimba endelea na shule.
Ukitoa mimba Sawa endelea na shule
Ukifanya usagaji, endelea na shule
Ukifanya anal sex endelea na shule
Ukiwa mwanaume (huwezi para mimba) endelea na shule.!
Mama Maria (Bikira Maria), angekuwa wa kipindi hiki na amepata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu basi angefukuzwa shule maana kwa umri ule 16yrs angekuwa shuleni bado.
Amenisikitisha sana huyu kiongozi wa kiroho, namfananisha na Mafarisayo wa kipindi cha Yesu. Maana angefukuza kila mwanafunzi anayezini (uasherati), anayeiba, anayesema uongo etc ningemuona wa maana. Maana amri za Mungu hakuna kubwa wala ndogo, na hakuna amri inayosema usibebe Mimba. Na kuhusu kuzini, Yesu aliuliza..... Ina maana huyu mama (binti) alizini peke yake.....?
It is okay kwa raisi kuzungumzia mimba lkn kiongozi wa kiroho anapaswa kuzungumzia uzinzi, wizi, uuaji (and for the case of kanisa Katoliki ni pamoja na matumizi ya vizuia mimba), uongo n.k.