Askofu Dallu: Marufuku shule za kanisa katoliki wanafunzi kuendelea na masomo baada ya kupata mimba

Kwa askofu, mimba ndio dhambi wala sio uzinzi au uasherati.
Ina maana, ukitumia condom au madawa ya kuzuia mimba endelea na shule.

Ukitoa mimba Sawa endelea na shule

Ukifanya usagaji, endelea na shule

Ukifanya anal sex endelea na shule

Ukiwa mwanaume (huwezi para mimba) endelea na shule.!

Mama Maria (Bikira Maria), angekuwa wa kipindi hiki na amepata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu basi angefukuzwa shule maana kwa umri ule 16yrs angekuwa shuleni bado.

Amenisikitisha sana huyu kiongozi wa kiroho, namfananisha na Mafarisayo wa kipindi cha Yesu. Maana angefukuza kila mwanafunzi anayezini (uasherati), anayeiba, anayesema uongo etc ningemuona wa maana. Maana amri za Mungu hakuna kubwa wala ndogo, na hakuna amri inayosema usibebe Mimba. Na kuhusu kuzini, Yesu aliuliza..... Ina maana huyu mama (binti) alizini peke yake.....?

It is okay kwa raisi kuzungumzia mimba lkn kiongozi wa kiroho anapaswa kuzungumzia uzinzi, wizi, uuaji (and for the case of kanisa Katoliki ni pamoja na matumizi ya vizuia mimba), uongo n.k.
Ni wapi ameruhusu hayo yote uliyoyasema. Sijawahi kusikia kiongozi yeyote akikubali uchafu unaoutaja wewe.
 
Nimeicopy sehemu hii, humu JF.

Nawashangaa sana wananchi, wachumi, viongozi wa dini na wanasiasa wa Tanzania. Naomba tutafakari pamoja yafuatayo na kisha, pamoja na maoni yangu, tujibu maswali yatakayofuata:

Section A (Sehemu ya kwanza)
Phase I (Awamu ya kwanza) (November 2015-June 2017)
Rais: Haiingii akilini kwa nchin yetu kutegemea misaada. Sisi tuna kila kitu, hatupaswi kuendesha nchi yetu kwa kutegemea
misaada. Kwanza hii misaada ina masharti mengi, na masharti mengine yanakwenda kinyume na utamaduni wetu.
Katika kipindi changu cha uongozi sitategemea misaada. Tunatakiwa sisi tukopeshe na kusaidia mataifa mengine na
siyo kusaidiwa. Misaada inatweza utu wetu.

Itikio la wasomi, wachumi, wananchi na wanasiasa: Tanzania tumempata Rais tuliyemhitaji tangu zamani. Tumechoka
na uhuru wa bendera. Tunatakiwa kujitegemea maana tuna kila kitu. Hatuwezi kuendelea kwa kutegemea misaada
ambayo wakati mwingine inatweza utu wetu. Hakuna nchi iliyoendelea duniani kwa kutegemea misaada. Huyu
anayekataa kuongoza nchi kwa kutegemea misaada anatufaa sana! Tumuunge mkono. Tanzania tuna kila raslimali na
ni aibu kutegemea misaada.

Phase II (Awamu ya pili) (July 2017)
Lissu: Nchi inaongozwa kinyume na Katiba. Kuna ukandamizaji mkubwa wa demokrasia nchini. Nchi haifuati mfumo wa vyama vingi. Vyama vya upinzani vinazuiwa kufanya shughuli za siasa. Viongozi wa upinzani wanakamatwa ovyo bila sababu maalumu. Jeshi la polisi, wakuu wa wilaya na mikoa wanatumika kukandamiza demokrasia ya vyama vingi. Mihimili mingine ya dola inadharaulika na kunyimwa uhuru wao. Uhuru wa kutoa maoni nchini umekosekana. Serikali inatumia fedha za kodi zetu na misaada kukandamiza demokrasia. Kwa hali hii tutaomba jumuiya za kimataifa ziinyime Tanzania misaada kwani inatumika vibaya kuminya demokrasia nchini.

Itikio la wasomi, wachumi, wananchi na wanasiasa: Huyu Lissu haitakii mema nchi. Hatuwezi kuendesha nchi na kuwahudumia watu wetu bila misaada toka nje. Mtu anayetaka kukwamisha misaada hatufai, apuuzwe kabisa. Msaada ndio nguzo ya maendeleo yetu. Hivi tukinyimwa misaada ataumia Lissu au Rais? Watakaoumia ni wananchi. Nchi haiwezi kwenda bila misaada.

Swali: Unapata picha gani ya wasomi, wananchi, wanasiasa na wachumi wa Tanzania?

My take: Kinachoungwa mkono Tanzania siyo nguvu ya hoja bali nani katoa hoja.

Section B (Sehemu ya pili)
Phase I (Awamu ya kwanza) (Julai 2015-Juni 2017)
Mkapa: Watanzania acheni kulialia. Watanzania ni wapumbavu na malofa.
Itikio la viongozi wa dini: Kimyaaaaaaaaa

Phase II (Awamu ya pili) (Julai 2017)
Lissu: Nchi inaongozwa kidikteta. Huyu kiongozi wetu ni udikteta. Udikteta uchwara umetamalaki nchini. Tuupinge kwa nguvu zote, viongozi wa dini wapinge na kila mtu kwa nafasi yake apinge maana hakuna aliye salama.

Itikio la viongozi wa dini (hasa kupitia msiba wa mke wa Mwakyembe): Hatutaki lugha za kuudhi na kuwakejeli viongozi wetu. Hatutamuunga mkono anayempinga Rais wetu na kumtolea lugha za kuudhi au matusi. Hiyo tabia ikome.

Swali: Unapata picha gani ya viongozi wa dini nchini?

My take: Tangu enzi na enzi viongozi wa dini (mafarisayo na masadukayo) wamekuwa upande wa tabaka tawala. hawajawahi kuwa upande wa wanyonge. Pia watu hawa hawakemei ubaya wa dhambi bali huangalia nani kafanya dhambi ndipo wakemee.

Nimeipenda sana hii post. Mimi ni mromani mfu. Siku hizi siendi kanisani kutokana na unafiki ninaouna wazi kwa viongozi wetu. Kwenda huko ni kwenda kukwazana tu. Safari hii ni kuhakikisha tunasimamia ukweli na sio kuwategemea viongozi wa dini kwani hao ni baadhi ya watu wanafiki wa kutupwa.
 
Kwa askofu, mimba ndio dhambi wala sio uzinzi au uasherati.
Ina maana, ukitumia condom au madawa ya kuzuia mimba endelea na shule.

Ukitoa mimba Sawa endelea na shule

Ukifanya usagaji, endelea na shule

Ukifanya anal sex endelea na shule

Ukiwa mwanaume (huwezi para mimba) endelea na shule.!

Mama Maria (Bikira Maria), angekuwa wa kipindi hiki na amepata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu basi angefukuzwa shule maana kwa umri ule 16yrs angekuwa shuleni bado.

Amenisikitisha sana huyu kiongozi wa kiroho, namfananisha na Mafarisayo wa kipindi cha Yesu. Maana angefukuza kila mwanafunzi anayezini (uasherati), anayeiba, anayesema uongo etc ningemuona wa maana. Maana amri za Mungu hakuna kubwa wala ndogo, na hakuna amri inayosema usibebe Mimba. Na kuhusu kuzini, Yesu aliuliza..... Ina maana huyu mama (binti) alizini peke yake.....?

It is okay kwa raisi kuzungumzia mimba lkn kiongozi wa kiroho anapaswa kuzungumzia uzinzi, wizi, uuaji (and for the case of kanisa Katoliki ni pamoja na matumizi ya vizuia mimba), uongo n.k.
Ndugu yangu Kaunga aliyeleta uzi atakuwa alichukua tu sehemu ya mahubiri ya askofu. Ukisoma mahubiri yote utakuta una ujumbe zaidi ya mmoja. Na kuhusu tabia za wengi ambao wanapata mimba wao wamesamehe waliowapatia mimba ndo maana hawapatikani unakuta kapewa mimba na mtu ambaye yuko maeneo ya nyumbani yeye anakataa kumtaja , wengine wanapewa mimba na wapita njia kwa uzembe wao. hivyo ni vizuri waitumikie zao la walichotafuta
 
Mtafute Padri akufafanulie tafsiri ya hilo andiko katika muktadha wa msichana kupata mimba akiwa shule ili uelewe. Usipende kukrem na kubeba maandiko kijuujuu.
Ingekuwa rahisi hivyo Mapadri wasingekuwa wanachukua muda mrefu vile kupata Upadri.
Wangekuwa wanapadrishwa baada tu ya kumaliza sunday school.

Watu wasiokuwa na watoto unatarajia watakupa ushauri gani kuhusu watoto? Halafu huwa nawashangaa watu wenye ndoa wanapokosana na wake zao wanakwenda kwa mapadri kusuluhishwa. Hivi mtu hana mke atakushauri nini? Anajua changamoto za kukaa na mke ana anasoma kwenye vitabu tu?
 
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Songea Mhashamu Damian Dallu amesema kuwa anaunga mkono hatua ya Rais John Magufuli kutoruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo, na kusema kuwa shule zinazomilikiwa na Kanisa Katoliki hazitaruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo.

Amesema hayo katika Ibada ya Misa Takatifu ya Upadrisho wa Shemasi Jerome Mtatifikolo, iliyofanyika katika Parokia ya Bikira Maria Afya ya wagonjwa Ilole jimboni Iringa ambapo amebainisha kuwa wanaoshabikia wanaopata mimba kurudi shule wanaharibu utamaduni wa kiafrika na kuchafua heshima ya Taifa.

“Hayo mambo siyo sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika, ni mambo ya kigeni yanayotaka kutuchafulia utamaduni wetu. Nawashangaa eti wanapigania haki ya tendo la ndoa, haki ya wapi hiyo?.

Tutakuwa na shule za namna gani zinazoruhusu mwanafunzi kwenda kulea mtoto kisha arudi tena na akipata mimba nyingine aende tena nyumbani?” Amehoji Askofu Dallu.

Katika hatua nyingine Askofu Dallu amewaasa waamini kufanya maandalizi ya kutosha hasa ya kiroho wanapojiandaa kuingia katika Sakramenti ya Ndoa ili ndoa zao ziwe na mwelekeo wa kiimani zaidi. Amesema kuwa kabla ya kupewa upadri, Shemasi Jerome alihudhuria mafungo ya kiroho ya siku 5 jambo ambalo linapaswa kuigwa na wale wanaojiandaa kupokea Sakramenti ya ndoa badala ya kujikita katika kufanya maandalizi ya kimwili.

“Watu wa familia mnatumia siku ngapi kufanya mafungo kabla ya kufunga ndoa? Au ndiyo ile kufanya maandalizi mengine ya kimwili marefu. Mkumbuke kuwa hata sisi mapadri tunatoka kwenu, matokeo ya kukosa maandalizi ya kutosha kabla ya ndoa ndiyo haya tunayoshuhudia sasa hivi ambapo wanaoishi ndoa kama Sakramenti ni wachache,” ameeleza.

Aidha amesema kuwa watu wanaoishi maisha ya pamoja kwa muda mrefu hadi kuwa na watoto hawastahili kuitwa wachumba kwa kuwa uchumba kielelezo chake ni Maria na Yosefu, na kuwataka kuacha kutumia jina hilo na badala yake wajiite wachumba sugu.

“Ulisikia wapi watu wanaishi uchumba mpaka wanakuwa na wajukuu? Tafuteni jina jingine kuanzia sasa labda mjiite wachumba sugu. Tutapata mapadri na masista wa namna gani? Kielelezo cha uchumba ni Yesu na Maria,” Ameeleza.

Pia amesema kuwa kazi ya karama ni kujenga umoja wa Kanisa na siyo kuligawa, na kumtaka kila mmoja kutumia wito wake kumtajirisha mwingine.
View attachment 547182

Chanzo:Gazeti la Kiongozi..
Anasema haya kama kutekeleza amri ya Mungu ama kumuunga mkono rais,km ni kwa kumtumikia Mungu mbona hakuyasema haya mapema,
Anna hii ya viongozi inafanya watu watufikilie vibaya ss wakatoliki,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wasiokuwa na watoto unatarajia watakupa ushauri gani kuhusu watoto? Halafu huwa nawashangaa watu wenye ndoa wanapokosana na wake zao wanakwenda kwa mapadri kusuluhishwa. Hivi mtu hana mke atakushauri nini? Anajua changamoto za kukaa na mke ana anasoma kwenye vitabu tu?
Unaelewa kwa nini Padre anaitwa FATHER?
 
Uzuri mamlaka ya Askofu ni ndani ya jimbo lake na ni kwa shule ambazo ziko chini ya kanisa..for other private schools wenye uwezo watawasomesha

sidhani kama kuna mzazi anapenda mtoto wake kupata mimba akiwa shuleni
 
.
Kosa kwao sii kula,
Kosa ni ujauzito na ndoo maana wanalawiti kuikwepa dhambi ya mimba
Usihukumu mtu kwa kosa alilofanya mwingine. Kila mtu auchukue mzigo wake mwenyewe. Watu kama nyinyi ndo mnajifanya wakamilifu machoni pa Mungu. Na mkienda kwenye biblia mnachukua tu sehemu na kutafsiri kwa uelewa wenu
 
Kama wewe ni mtu mwenye familia na una watoto wa kike zaidi ya mmoja ikitokea mmoja akapata mtoto ndani ya familia na hakuna hata karipio utakalotoa kuna uwezekano wa wengine kufuata mkondo wa mkubwa.kumkataza asiendelee na masomo hapo alipokuwa ni sehemu ya malipizi ya makosa aliyoyafanya ili ukija kumruhusu kusoma shule za private kama nafasi ipo au kufanya mtihani kama private candidate akiwa amejirekebisha atafaulu kama ana uwezo maana kila akikumbuka makosa yake atajitahidi kwa uwezo wake wote.
Yap! Umenielewa na nimekuelewa pia. Ikitokea binti amepata mimba lazima hatua stahiki zichukuliwe ili atambue na kujutia kosa, halafu mpe nafasi kwani atakuwa amejifnza kitu fulani, ndio maana nimeshtushwa na msimamo wa baba Askofu uliokinyume na biblia kwani hakuna kosa lisilo na msamaha kama asemavyo Isaya 1.18 " Hata dhambi zenu zikiwa nyekundu, zitafanywa kuwa nyeupe kama theluji; hata zikiwa nyekundu kama kitambaa chekundu; zitakuwa kama sufu".
 
Usihukumu mtu kwa kosa alilofanya mwingine. Kila mtu auchukue mzigo wake mwenyewe. Watu kama nyinyi ndo mnajifanya wakamilifu machoni pa Mungu. Na mkienda kwenye biblia mnachukua tu sehemu na kutafsiri kwa uelewa wenu
.
Mbona sasa huyu kasisi wa kikatoliki kamhukumu msichana mwanafunzi aliyebakwa kwa kosa lisilokua lake?
Kanisa linapaswa kuwa makini sana na kujiepusha na ushabiki wa kisiasa. Takimko la askofu halikuzingatia weledi kwani kama isingelikua ni kusukumwa na mhemko wa ushabiki ange specify badala ya ku generalize issue yote.
 
Maaskofu wamesahau maandiko ya kuhukumu???
Ndo maana nilibaki kuisoma Biblia tu na sio kwenda kanisani kwa unafki na ujinga wa hawa maaskofu uchwara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaelewa kwa nini Padre anaitwa FATHER?

Mkuu ili kuheshimu imani na kutokuwakwaza wengine hebu tuliache tu hilo. Mimi ni mromani mfu, sitaki kuzunguma mengi wakati sijui yote bali nina ufahamu wa kutosha kuhusu dhehebu hilo. Kuna mengine kuyaweka hapa tutapunguza imani za wengi. Huyo askofu tunamstahi tu na awe na hekima kwani hata ada za shule zao tunaona zinavyoumiza hata hao waumini wao.
 
Yap! Umenielewa na nimekuelewa pia. Ikitokea binti amepata mimba lazima hatua stahiki zichukuliwe ili atambue na kujutia kosa, halafu mpe nafasi kwani atakuwa amejifnza kitu fulani, ndio maana nimeshtushwa na msimamo wa baba Askofu uliokinyume na biblia kwani hakuna kosa lisilo na msamaha kama asemavyo Isaya 1.18 " Hata dhambi zenu zikiwa nyekundu, zitafanywa kuwa nyeupe kama theluji; hata zikiwa nyekundu kama kitambaa chekundu; zitakuwa kama sufu".
Ni kweli mheshimiwa lakini ujue ili dhambi isamehewe lazima hatua zinazohitajika kwaajili ya kusamahewa dhambi zichukuliwe. Huwezi kuomba msamaha wakati unafikiria kuendelea na kosa. Tatizo kwa hawa dada zangu na wadogo zangu wa kike hawaoneshi ushirikiano ili kila mtu atumikie stahili zake. Sijaona sehemu kwenye biblia ambayo inakataa mahakama ila zipo sehemu zinazokataza hukumu za upendeleo kama ile ya ya mwanamke kuhukumiwa kutokana na uzinzi na kuwaacha aliozini nao.ukitumia hiyo sheria ya nchi haina upendeleo lakini watoto wa kike hawaoneshi ushirikiano.
 
Akisema kama kiongozi wa shule nitamuelewa, lkn akisema kama kiongozi wa kiroho, mimba haijawahi kuwa dhambi hata siku moja. Ni sawa na kutibu homa na kuacha malaria au infection yoyote. Maana sio infections zote zinaleta homa. Je wasagaji wataadhibiwaje, maana hakuna mimba itakayoonekana.

Je mdada akihamia shule yake watampima kama alishawahi kuzaa huko alipotoka? Siasa awaachie wana siasa.

Ndugu yangu Kaunga aliyeleta uzi atakuwa alichukua tu sehemu ya mahubiri ya askofu. Ukisoma mahubiri yote utakuta una ujumbe zaidi ya mmoja. Na kuhusu tabia za wengi ambao wanapata mimba wao wamesamehe waliowapatia mimba ndo maana hawapatikani unakuta kapewa mimba na mtu ambaye yuko maeneo ya nyumbani yeye anakataa kumtaja , wengine wanapewa mimba na wapita njia kwa uzembe wao. hivyo ni vizuri waitumikie zao la walichotafuta
 
.
Mbona sasa huyu kasisi wa kikatoliki kamhukumu msichana mwanafunzi aliyebakwa kwa kosa lisilokua lake?
Kanisa linapaswa kuwa makini sana na kujiepusha na ushabiki wa kisiasa. Takimko la askofu halikuzingatia weledi kwani kama isingelikua ni kusukumwa na mhemko wa ushabiki ange specify badala ya ku generalize issue yote.
Ukisema wataruhusiwa waliobakwa hapo ujue kila mmoja atakayepata mimba atasema amebakwa na hamjui aliyembaka. Unatakiwa uangalie baadae itakuwaje. Nikuulize kidogo kwa uelewa wako nijibu kama watoto wa kike waliopata mimba wakiruhisiwa je, na kifungo cha miaka 30 jela kwa aliyeshirikiana na huyo msichana ifutwe?
 
Back
Top Bottom