Askofu Dallu: Marufuku shule za kanisa katoliki wanafunzi kuendelea na masomo baada ya kupata mimba

JK alisakamwa sana na kanisa kwa sababu ya Uislamu wake. Hii ndio rangi halisi ya hawa Church Fathers.
Wala sio .hawa tatizo lao nikujipendekeza tuu kwa watawala Wa kidunia .ukumbuki ataa Kikwete si hawa hawa walisema Kikwete ni mteule Wa Mungu katuletea ,
 
Sijamwelewa askofu,anaposema "Kielelezo cha uchumba ni Yesu na Maria,"
Ina maana Yesu alimchumbia Maria au? Sio Josefu ndio limchumbia Maria?
Halafu kwa askofu ni sawa kupinga maana yeye hajachaguliwa na mtu kuongoza japo anaongeza nguvu kuwa washauri wa bwana "Pogba" ni kanisa.
Utamaduni wetu ni umaskini,lazima tuuenzi.
Hilo ni kosa la kiuandishi, ni Yosefu na Maria
 
Kwani hawa waromani katoliki wanayajua maandiko matakatifu bibilia kwao wanaiona tu kwa hiyo suala LA kusamehe hata huyo askofu hajui au mkumbo wa kisiasa umemkuta na kusahau msimamo na misingi ya kiutume

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kanisa katoliki limekuwa na shida nyingi sana kwenye eneo hili ambalo askofu anazungumzia. Kuna mapadre na watawa wanahusika moja kwa moja na mimba za wanafunzi. Ni vyema sasa kama kanisa kuishauri serikali namna nzuri na pana ya kuangalia jambo hili. Ni kweli si sahihi watoto kupata ujauzito na kurudi shuleni directly. Kwanza, si sahihi kijamii, kidini nahata kiserikali. Lakini kuna mimba nyingine ukisikia mazingira zilipopatikana utalia machozi... tuwe na a broad outlook of problem!
Mfano yule Binti juzi kati hapa kaenda hospitali kumuuguza mama yake .muhuguzi kamchoma sindano ya usingizi kambaka
 
Yesu alitumia mfano wa mbegu kwamba mbegu haiwezi kuzaa bila kufa kwanza (sijui kwenye biblia ni sehemu gani). Hivyo kumfukuza mmoja itasaidia kuzuia au kupunguza kwa kiasi wengine wasifanye makosa yanayofanana. Kufukuza ni sehemu ya kuboresha nidhamu kwa wengine watakao baki. Tusichukue mifano michache kuangamiza wengi. Na ujue kuna kumsaidia mtu huku ukiwa unaonesha kutoridhika na makosa yake. Naamini kwa asilimia kubwa ikitokea mwanafunzi mmoja katika kundi akipata mimba na akiruhusiwa wengine kupata mimba kuko nje nje. Hivyo kumyima kuendelea hapo inaonesha kabisa kumpa nafasi nzuri ya kujirekebisha kuliko kumuuacha hapo. Mm nina mifano mingi ya watu ambao wanafuata waliowatangulia wakifanya tu uzembe wengine wanaofuata kufuata tabia hiyo.
(Methali 23:13)Proverbs 23:13. Withhold not correction from the child: for if thou beatest him with the rod, he shall not die
Rafiki mpendwa kumbuka wengine wanapata mimba baada ya kubakwa nao je unasemaje? Lakini pia vaa viatu vya hao watoto wa kike uwe mmoja kisha upime mazingira wanayopatia hizo mimba. Lakini pia bado ninaamini kwamba Baba Askofu ametoa maoni yake ya mtu asiyejua changamoto za malezi kwani hajawahi kuwa na familia yeye amejaa theory tu. Mimi kama mzazi na kamwe siwezi kuufuata ushauri wake hata kama ni kiongozi wangu wa kiroho!
 
Tungetaraji kanisa ndilo liwe kielelezo cha "Kusamehe" na kutohesabia hatia mkosaji huyo ambaye ni mtoto lakini inakuwa ni kinyume chake.
Kwanza ni ngumu sana kutoka
.
Ukatoliki sii mila wala utamaduni wa kiafrika.
Ukatoliki ni mila ya ulaya(magharibi) iliyoasisiwa na dola la Rumi ya kale.

Mila na utamaduni wa Kiafrika ni mwanafunzi kupata mimba na kuendelea na masomo eti.?
 
Inawezekana mimba hizo ni tunda la uzinzi, ambayo ni dhambi. Je na wale wanaobakwa je? Wanaorubuniwa na ndugu ili watimiziwe mahitaji ya msingi, ikiwemo elimu? Na wao tunawahukumu? Hata Yesu, alituasa tusamehe saba mara sabini. Hata Yesu yule mwanamke mzinifu alipotaka kupigwa mawe na umati (kitu ambacho ni utamaduni wao) aliwaambia "mwenye dhambi na anyanyue jiwe awe wakwanza kumpiga"... Leo hii, Kanisa lilojengwa kwenye msingi wa mafundisho na maisha ya Yesu Kristo, linawanyanyapaa watoto wa Kanisa, watoto wa Yesu. Hatuwasaidii, tunawazidishia mzigo..wakimbilie wapi kwenye faraja na mafunzo ya kweli kama sio "Kanisani"?
Wanaobakwa ni sehemu ndogo sana ukilinganisha wanaopata mimba na wengine wanatengeneza wenyewe mazingira ya kubakwa. Kama wamerubuniwa wakakubali siyo tu mahitaji ya shule wengine wataendelea kurubuniwa kwa mambo ya starehe.Na wakiruhusu tu waliopata mimba kuendelea kusoma hapo lazima wengine waenende katika njia sawa tu na hiyo. Mfano kama rafiki wa msichana ana mtoto na anasoma na wengine pasipo kutumia jasho kupata nafasi lazima wengine wengi japo siyo wote watatafuta mtoto kwa njia yoyote maana atakuwa anawaringishia wenzake kuonesha kuwa yeye ni wa level nyingine na wenzake watasawazisha kwa kupata mimba.Mm naamini kwa mtu ambaye anajua vizuri akili za watoto wengi wa kike hawezi kukubali waliopata ujauzito kuendelea na shule. Kwaiyo acha tu watafute nafasi kwa jasho ili kuwatofautisha na wengine ambao hawajapewa ujauzito.
 
Kwa askofu, mimba ndio dhambi wala sio uzinzi au uasherati.
Ina maana, ukitumia condom au madawa ya kuzuia mimba endelea na shule.

Ukitoa mimba Sawa endelea na shule

Ukifanya usagaji, endelea na shule

Ukifanya anal sex endelea na shule

Ukiwa mwanaume (huwezi para mimba) endelea na shule.!

Mama Maria (Bikira Maria), angekuwa wa kipindi hiki na amepata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu basi angefukuzwa shule maana kwa umri ule 16yrs angekuwa shuleni bado.

Amenisikitisha sana huyu kiongozi wa kiroho, namfananisha na Mafarisayo wa kipindi cha Yesu. Maana angefukuza kila mwanafunzi anayezini (uasherati), anayeiba, anayesema uongo etc ningemuona wa maana. Maana amri za Mungu hakuna kubwa wala ndogo, na hakuna amri inayosema usibebe Mimba. Na kuhusu kuzini, Yesu aliuliza..... Ina maana huyu mama (binti) alizini peke yake.....?

It is okay kwa raisi kuzungumzia mimba lkn kiongozi wa kiroho anapaswa kuzungumzia uzinzi, wizi, uuaji (and for the case of kanisa Katoliki ni pamoja na matumizi ya vizuia mimba), uongo n.k.
 
Za kuambiwa ongeza na za kwako: Askofu hana mtoto, acha kumsaidia binti yako halafu uone joto lake baadae
Mwanangu atasoma tu hata akifukuzwa. Ndio maana kuna private schools
Lakini kwenye shule zinazoendeshwa na kodi za waTanzania wote hataweza.
 
Rafiki mpendwa kumbuka wengine wanapata mimba baada ya kubakwa nao je unasemaje? Lakini pia vaa viatu vya hao watoto wa kike uwe mmoja kisha upime mazingira wanayopatia hizo mimba. Lakini pia bado ninaamini kwamba Baba Askofu ametoa maoni yake ya mtu asiyejua changamoto za malezi kwani hajawahi kuwa na familia yeye amejaa theory tu. Mimi kama mzazi na kamwe siwezi kuufuata ushauri wake hata kama ni kiongozi wangu wa kiroho!
Kama wewe ni mtu mwenye familia na una watoto wa kike zaidi ya mmoja ikitokea mmoja akapata mtoto ndani ya familia na hakuna hata karipio utakalotoa kuna uwezekano wa wengine kufuata mkondo wa mkubwa.kumkataza asiendelee na masomo hapo alipokuwa ni sehemu ya malipizi ya makosa aliyoyafanya ili ukija kumruhusu kusoma shule za private kama nafasi ipo au kufanya mtihani kama private candidate akiwa amejirekebisha atafaulu kama ana uwezo maana kila akikumbuka makosa yake atajitahidi kwa uwezo wake wote.
 
UNAFKI NI KITU KIBAYA SANA ANGEKUWA NI MUISLAMU WANGEMPINGA KWA NGUVU ZOTE ILA KWA KUWA SAFARI HII NI WA KANISA LAO BASI KILA KITU SAWA

kwenye kula hela za rambirambi wako kimya hatukuona matamko KUJIPENDEKEZA NI KUBAYA SANA

Kwanza punguzeni chuki

Mbili Kanisa halisapoti uzinzi, huruhusiwi kushiriki tendo la ndoa kama hujafunga ndoa Kanisani

So hata kama ukiwa above 18 kwa mafundisho ya Kikristo hauluhusiwi kujamiana

Serikari ndiyo inayotoa relief watu mjamiane angalau mkiwa wote above 18 na si wanafunzi (hii ni kama ka advantage ka nchi yetu Tanzania kuwa secular state)

Kwanza ni ngumu sana kutoka

Mila na utamaduni wa Kiafrika ni mwanafunzi kupata mimba na kuendelea na masomo eti.?
.
Mila zetu afrika ni za kuhurumiana kusaidiana na kuthaminiana. Hivyo katika familia zetu mtoto akimyea mzazi, hatupwi wala kunyimwa haki zake za msingi kama mtoto
 
Kwa askofu, mimba ndio dhambi wala sio uzinzi au uasherati.
Ina maana, ukitumia condom au madawa ya kuzuia mimba endelea na shule.

Ukitoa mimba Sawa endelea na shule

Ukifanya usagaji, endelea na shule

Ukifanya anal sex endelea na shule

Ukiwa mwanaume (huwezi para mimba) endelea na shule.!

Mama Maria (Bikira Maria), angekuwa wa kipindi hiki na amepata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu basi angefukuzwa shule maana kwa umri ule 16yrs angekuwa shuleni bado.

Amenisikitisha sana huyu kiongozi wa kiroho, namfananisha na Mafarisayo wa kipindi cha Yesu. Maana angefukuza kila mwanafunzi anayezini (uasherati), anayeiba, anayesema uongo etc ningemuona wa maana. Maana amri za Mungu hakuna kubwa wala ndogo, na hakuna amri inayosema usibebe Mimba. Na kuhusu kuzini, Yesu aliuliza..... Ina maana huyu mama (binti) alizini peke yake.....?

It is okay kwa raisi kuzungumzia mimba lkn kiongozi wa kiroho anapaswa kuzungumzia uzinzi, wizi, uuaji (and for the case of kanisa Katoliki ni pamoja na matumizi ya vizuia mimba), uongo n.k.

Ulitaka akuorodheshee makosa yote yatakayoweza kumfukuzisha mtoto shule?
Waulize waliosoma seminary watakupa list ndeeeeeeefu hadi utafurahi. Na I can assure you kuna mengine madogo kabisa kuliko uliyoyataja yanamfukuzisha mtoto katika shule za kanisa katoliki.
 
Kwani haya mambo ya mtu kupata mimba asiendelee na shule kaanzisha magufuli?!

Mwanafunzi lazima ajue wajibu wake. Mtoto aende kupata mimba halafu ww uwe unamchekea ndio malezi hayo?!

Tuache unafiki hili sio suala la kuliletea mchezo kabisa
 
Back
Top Bottom