Askofu Dallu: Marufuku shule za kanisa katoliki wanafunzi kuendelea na masomo baada ya kupata mimba

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Songea Mhashamu Damian Dallu amesema kuwa anaunga mkono hatua ya Rais John Magufuli kutoruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo, na kusema kuwa shule zinazomilikiwa na Kanisa Katoliki hazitaruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo.

Amesema hayo katika Ibada ya Misa Takatifu ya Upadrisho wa Shemasi Jerome Mtatifikolo, iliyofanyika katika Parokia ya Bikira Maria Afya ya wagonjwa Ilole jimboni Iringa ambapo amebainisha kuwa wanaoshabikia wanaopata mimba kurudi shule wanaharibu utamaduni wa kiafrika na kuchafua heshima ya Taifa.

“Hayo mambo siyo sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika, ni mambo ya kigeni yanayotaka kutuchafulia utamaduni wetu. Nawashangaa eti wanapigania haki ya tendo la ndoa, haki ya wapi hiyo?.

Tutakuwa na shule za namna gani zinazoruhusu mwanafunzi kwenda kulea mtoto kisha arudi tena na akipata mimba nyingine aende tena nyumbani?” Amehoji Askofu Dallu.

Katika hatua nyingine Askofu Dallu amewaasa waamini kufanya maandalizi ya kutosha hasa ya kiroho wanapojiandaa kuingia katika Sakramenti ya Ndoa ili ndoa zao ziwe na mwelekeo wa kiimani zaidi. Amesema kuwa kabla ya kupewa upadri, Shemasi Jerome alihudhuria mafungo ya kiroho ya siku 5 jambo ambalo linapaswa kuigwa na wale wanaojiandaa kupokea Sakramenti ya ndoa badala ya kujikita katika kufanya maandalizi ya kimwili.

“Watu wa familia mnatumia siku ngapi kufanya mafungo kabla ya kufunga ndoa? Au ndiyo ile kufanya maandalizi mengine ya kimwili marefu. Mkumbuke kuwa hata sisi mapadri tunatoka kwenu, matokeo ya kukosa maandalizi ya kutosha kabla ya ndoa ndiyo haya tunayoshuhudia sasa hivi ambapo wanaoishi ndoa kama Sakramenti ni wachache,” ameeleza.

Aidha amesema kuwa watu wanaoishi maisha ya pamoja kwa muda mrefu hadi kuwa na watoto hawastahili kuitwa wachumba kwa kuwa uchumba kielelezo chake ni Maria na Yosefu, na kuwataka kuacha kutumia jina hilo na badala yake wajiite wachumba sugu.

“Ulisikia wapi watu wanaishi uchumba mpaka wanakuwa na wajukuu? Tafuteni jina jingine kuanzia sasa labda mjiite wachumba sugu. Tutapata mapadri na masista wa namna gani? Kielelezo cha uchumba ni Yesu na Maria,” Ameeleza.

Pia amesema kuwa kazi ya karama ni kujenga umoja wa Kanisa na siyo kuligawa, na kumtaka kila mmoja kutumia wito wake kumtajirisha mwingine.
image.jpeg



Chanzo:Gazeti la Kiongozi..
 
Miaka 50 iliyopita ulaya mabinti waliopata mimba nje ya ndoa walipelekwa kwenye nyumba za watawa na kule walipewa ajira ya kufua shuka za wagonjwa kutoka mahospitalin. Walifua na kupiga pasi shuka na pyajama za wagonjwa kwa ujira wa tonge la ugali.

Watoto wao walipo zaliwa waliwekwa kwenye orphanage homes na wengine walikuwa adopted. Wadada wale walikaa mission wengine wakiishia kuolewa na walinzi au madreva wa kanisa kwani ndiyo wanaume pekee walio waona
Huku ndiko tunakoelekea sisi sasa hivi
 
Bendera fata upepo huyu askofu! Badala ya kukemea mambo ya msingi naibuka Na mambo ya ovyo kabisa!

Kama wewe ndo askofu kanisa katoriki lina hasara kubwa! Ulikuwa wapi kukemea tangia zamani muumini wenumkuu anaibuka bila kujua Na wewe unafata mkumbo kwa kujikomba!!!,!!

Kikwete kipindi hicho mlimshambulia sana, sijui nikwasababu ya dinini yake!!! Leo Hii hali ya nchi nimbaya kila nyanja mnajifanya mabubu kisa jamaa ni muuni wenu!!! Msaraba mkubwa unafiki umekujaa!
 
Tungetaraji kanisa ndilo liwe kielelezo cha "Kusamehe" na kutohesabia hatia mkosaji huyo ambaye ni mtoto lakini inakuwa ni kinyume chake.
Askofu yuko sahihi. Je watoto wanaopata mimba kwani wako kwenye ndoa?kusema waendelee na masomo ni kusema waendelee na uzinzi japo kuna wazinzi sugu ambao hawapati mimba .
 
Miaka 50 iliyopita ulaya mabinti waliopata mimba nje ya ndoa walipelekwa kwenye nyumba za watawa na kule walipewa ajira ya kufua shuka za wagonjwa kutoka mahospitalin. Walijua na kupiga pasi shuka na pyajama za wagonjwa kwa ujiracwa tonge la ugali.

Watoto wao walipozakiwa waliwekwa kwenye orphanage homes na wengine walikuwa adopted. Wadada wale walikaa mission wa engine wakiishia kuolewa na walinzi au madreva wa kabisa kwani ndiyo wanaume pekee walio waona
Umeandika nn
 
Sijamwelewa askofu,anaposema "Kielelezo cha uchumba ni Yesu na Maria,"
Ina maana Yesu alimchumbia Maria au? Sio Josefu ndio limchumbia Maria?
Halafu kwa askofu ni sawa kupinga maana yeye hajachaguliwa na mtu kuongoza japo anaongeza nguvu kuwa washauri wa bwana "Pogba" ni kanisa.
Utamaduni wetu ni umaskini,lazima tuuenzi.
 
Mimi ni mkatoliki na hivyo sikubaliani kabisa na matamko ya huyu askofu kwa sababu anapotosha watu sabb ya kiherehere cha mtafuta kiki kwa piki2 ukisoma kitabu cha maandiko matakatifu cha mathayo 18; 21-35 inaelekeza wazi ni jinsi gani wanadamu wanavyopaswa kusamehana na kumwachia mungu atoe hukumu kwa matendo mabaya.
 
Hivi seminarini kuna kuaga na msamaha kwa mwanafunzi anaekosea ?
Maana nijuavyo hawa jamaa ukilizua tu out bila huruma.
Wako wanaodeka eti wapewe huruma. Yesu alisema jiurumieni nyinyi kwanza, unataka huruma wakati wewe mwanzo ulishindwa kujiurumia ...si wehu huu!!!???
 
Kumuunga mkono Rais hakuja wahi kumuacha mtu salama.

Nukuu. "Wakenya nyinyi mmeendelea sana kuliko nchi zingine za Africa mashariki! kwa hiyo msibaguane mmepiga hatua"
 
Unafiki ni kwa kila Mwanadamu, namuunga mkono askofu kwa maana ametoa tamko kwa niaba ya kanisa jimboni mwake ambao yy ni mtawala.
Ni sawasawa Hata mm ndani ya utawala wa NYUMBA ni kwangu binti zangu ntawaambia hivyohivo Hata nyingi watoto wenu, wadogo zenu na majirani zenu mtawaambia hivyo hivyo tuache unafiki .
Plan B baada ya binti kutiwa mimba hayo ni mengine. Yaani kanisa lishabikie mimba zitokanazo na zinaa au kanisa lishabikie matumizi ya kondom hapana kila kitu na wakati wake watoto wasubiri wakati utafika.
 
Back
Top Bottom