The Supreme Conqueror
JF-Expert Member
- Feb 13, 2017
- 609
- 1,574
Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
____
1. Nyerere alisema taifa hili bila CCM imara, litayumba. Sina hakika kama bado halijayumba.
2. Ili CCM iwe imara inahitaji upinzani imara. Hatuna utamaduni imara wa kukosoana ndani ya chama kimoja na kubaki salama.
3. CCM dhaifu na upinzani dhaifu ni chanzo cha taifa lililojaa machawa, rushwa, uzembe, ukandamizaji na uporaji wa raslimali za nchi.
4. Marais wetu wanatokana na vyama, tusiwategemee sana wawe “neutral” katika masuala ya kisiasa. Chini ya mfumo wa sasa, hata rais mlokole hawezi kuwa neutral.
5. Huu ni mwaka wa uchaguzi. Tamaa ya madaraka ndani ya CCM ni kama yote. Ubinafsi ndani ya upinzani ni kama wote. Nani mwathirika wa hali hii?
6. Mwathirika wa kwanza ni nchi/taifa. Tutakosa uwajibikaji. Na tukifika hapo hata wanaotaka watawale peke yao wataumia. Miradi yote ya kimkakati itakosa ulinzi. Watu watatamani Rais dikteta wa kuumiza chama chake na vyama vingine na atashangiliwa kwa muda kabla ya majuto kwa nchi nzima baadae.
7. Mwathirika wa pili ni CCM. Itakosa chama pinzani imara cha kuiwajibisha. Hivyo CCM Itateka na kuua ili kujilinda. Baada ya kumaliza wapinzani, itajiteka na kujiua yenyewe.
8. Mwathirika wa tatu ni mwananchi. Watakosa mahali pa kwenda kupata haki ya kusikilizwa matatizo na kero zao.
9. Kukosekana kwa uimara wa upinzani kumeifanya CCM na serikali kuua “ugatuzi” wa madaraka na kupeleka madaraka yote Dodoma. Hiki ni kichaka cha mateso kwa wananchi. Mtu anaandika barua Dodoma, haijibiwi. Anafuatilia, anaambiwa rudi wilayani bila majibu. Mamwinyi waliopo Dodoma wanaamini kila mtanzania ana simu na kifurushi cha kutumia mtandao.
10. Anayeshangilia kuzima taa zote na kuwasha moja si Mzalendo. Anayeshangilia upinzani kusambaratika si Mzalendo. Anayetumia fedha kudhoofidha upinzani si Mzalendo. Taifa letu ni kubwa kuliko chama chochote. Taifa kubwa namna hii likiwa na mtazamo mmoja litaangamia.
NB: Migogoro ndani ya upinzani inawanyima wananchi haki ya utetezi na inawanyima watawala haki ya kuwajibishwa.
Hekima ya Wajaluo: Ngedere mchanga aliona msitu unateketea, akashangilia asijue usiku atalala wapi?