Wenye akili ndogo bado imekuwa shida kumuelewa, japo kajibu kwa kutumia simple falsafa bora umewasaidia kidogo
Well said mkuu, watu wanacho sahau ni kwamba Askofu hapo anatumia lugha ya kidiplomasia kufikisha ujumbe, Bagonza ni mtu msomi na mwenye hekima sana - wanao msema vibaya wanafikiri ana ambition za kisiasa hasa labda kuwania kiti cha Urais - hiyo si kweli hata kidogo - exposure yake kimataifa inamuwezesha kutathimini mambo na kuona hatari ambayo bado ni latent lakini inaweza kuli-cost Taifa letu dearly eventually.
Askofu Bagonza hawezi kuwa anazungumzia mitungi ya Oxygen bila ya kujiridhisha kwamba kuna tatizo si bure - binafsi hili suala la Taifa letu kujiamini kupitiliza kiasi linapokuja suala la Corona uwa linanitia wasi wasi sana - I may be paranoid lakini ukweli wa mambo ugonjwa huu haukondoka nchini by 100% tusije tukajidanganya.
Kinacho tishia zaidi ni huu ujio wa watalii nchini bila ya kuwekwa karantini kwa wiki mbili tunabaki kutegemea tu upimaji wa joto la mwili mbinu hiyo sio sahihi hata kidogo, wakati baadhi ya Mataifa wamefikia hatua ya kupiga marufuku ndege zinazotoka Uingereza, Merikani na Afrika kusini kutua katika viwanja vyao, sijawahi kusikia Taifa letu linapiga marufuku ujio wa ndege nchini kutoka kwa mataifa tajwa hapo juu.
Tukumbuke kwamba Karagwe inapakana na Rwanda na Uganda Mataifa ambayo yana idadi kubwa ya waathirika - kwa nini amuhoji Askofu Bagonza akaeleza anamaanisha nini anapo toa tahadhali kuhusu ugonjwa wa Corona, je, amekwisha shuhudia incidents ngapi recently - Bagonza hawezi kuwa amekurupuka tu, kuna kitu si bure, ushauri wangu msikilizeni kuliko kumu-dismiss off hand just like that!
Labda swali la kujiuliza hapa kama suala ni ku-overly depend on prayers kutokomeza ugonjwa,je, raia wa Ulaya na Marekani wanao kumbwa na ugonjwa huu kwa wingi, kwani wao hawa amini uwezo mkubwa wa Mungu kupitia kwenye sala? Mbona Vatican imepoteza idadi kubwa ya Mapadri na Watawa wakati wao usali Rozali 24X7?
Bottom line is: Msilikizeni Askofu Bagonza ana ujumbe gani kuliko kuanza kumbeza beza mkifikiri ana malengo ya kisiasa wakati lengo lake ni kutadhalisha Taifa dhidi ya ugonjwa mbaya wa Corona.