Askofu Bagonza: Kuna kitu hakiko sawa

Askofu Bagonza: Kuna kitu hakiko sawa

Majirani wema huzaa watoto wanaofanana kwa sababu ya kuhusiana vizuri.
Hapa baba askofu BAGONZA nitakuja Karagwe kuomba ufafanuzi zaidi, unamaanisha nini?

Kwamba mqjirani wakipendana sana wanachepukiana?

Lkn kwa ujumla baba askofu nakupongeza Sana wewe na askofu Mwamakula kwa juhudi zenu za kupambana na jiwe.
 
Daah.....naona shetani leo unahubiria watu JF kuhalalisha kutowepo corona Tanzania? Nani asiyekujua hapa jamvini hata unene haya?
 
Usikute kayaongea haya kwenye ibada ya watu zaidi ya 200 na wote hawajavaa mask na bado wamesongamana kwenye kutoa sadaka alaf bado anashindwa kumtukuza Munga kwa hilo yeye analeta janja janja za siasa.
Huo ni waraka siyo mahubiri kanisani.
 
Hapa baba askofu BAGONZA nitakuja Karagwe kuomba ufafanuzi zaidi, unamaanisha nini?

Kwamba mqjirani wakipendana sana wanachepukiana?

Lkn kwa ujumla baba askofu nakupongeza Sana wewe na askofu Mwamakula kwa juhudi zenu za kupambana na jiwe.
Uganda (Mu7), PK na JPM ni majirani wanaofanana kwa sasa so lazima wazae watoto ukatili, mauaji, unyanyasaji , ufisadi nk
 
Mimi huwa sisikilizi siasa za kusema hakuna korona, kwa uspesho gani haswa? kama tuna huo utakatifu si basi tuwaommee Dunia yote?

Ila naunga mkono Watu kuendelea na shughuli zao mambo ya kufungiana ni kuongeza tu matatizo na wala si kupunguza.

Tuendelee na a zile hatua za kujikinga kama kunawa mikono, kukwepa mikusanyiko isiyo ya lazima...kwenye daladala fungueni vioo hewa iingie.
Yani haukubali siasa ya kwamba Tanzania hakuna corona ila hapo hapo unakubali siasa ya kwamba watu waendelea na shughuli zao kama kawaida kwamba tuendelee kujazana kwenye madaladala,kujazana kwenye nyumba za ibada,masokoni na kwenye misiba na sherehe.

Hapo ni sawa na kukubali kuwepo corona Tz kinadharia ila kivitendo haukubali kuwepo corona Tz.
 
Kwa Sasa ukivaa barakoa hadharani unaeza tiwa korokoroni
Hakuna ndugu yangu taasisi kibao huingii ofisin bila barakoa

Nimeshuhudia Shule moja ya sekondari nilipeleka mtoto nikazuiwa ikabidi ninunue barakoa wanauza hapo Bei balaa

Na pia nilikua na shida ya kwenda kwenye ofisi ya RPC mojawapo(Makao makuu ya Polisi mkoa) nikazuiwa ikabidi ninunue kabarakoa uchwara kwa mmama yupo anauza kwa bei balaa

Nikajifunza sasa hivi natembea na barakoa yangu maalum mfukoni kama leso vile

Usisikilize maneno. Watu wanajilinda
 
Yani haukubali siasa ya kwamba Tanzania hakuna corona ila hapo hapo unakubali siasa ya kwamba watu waendelea na shughuli zao kama kawaida kwamba tuendelee kujazana kwenye madaladala,kujazana kwenye nyumba za ibada,masokoni na kwenye misiba na sherehe.

Hapo ni sawa na kukubali kuwepo corona Tz kinadharia ila kivitendo haukubali kuwepo corona Tz.
Kama umenielewa vizuri ni kwamba corona ipo kama ilivyo sehemu nyingine.

Ila shughuli ziendelee, na kuendelea na shughuli ina maanisha huwezi kukwepa kupanda daladala iliyojaa n.k...ila kama una njia za kukwepa hayo basi fanya hivyo ukikumbuka kichwani kwamba corona ipo.

Kwa mfano kama una uwezo wa kupata mahitaji ikiwemo chakula bila kutoka ndani basi fanya hivyo.
 
Ndio limekuwa suala la watu binafsi kuvaa hizo barakoa,nakumbuka pale muhimbili ilikuwa upiti pale getini bila barakoa ila sasa unapita tu.
 
Mkuu anaposema hatuna korona anataka tu 'wanyonge' tusiwe na hofu

Anachokosea ni kutosisitiza 'wanyonge' kuchukua tahadhali
 
Bagonza f. Ponda.jpeg
 
Bagonza anachomaanisha Corona bado ipo Tanzania, nakubaliana nae; ila yeye katumia njia ndefu kufikisha ujumbe wake.
Njia fupi haitakiwi na wakubwa,, angeishia matatani! Ana uelewa wa kutosha wa aongee nini na wapi!
 
Hii ni uthibitisho wa wazi kuwa ASkofu Bagonza ni mpagani sio Mkristo

Corona na Mungu haviwezi kuwa mahali pamoja Mungu

Lipagani hili Askofu kwa hiyo hata mbinguni kwaweza kuwa na Corona?
Kuna mahali katika Biblia Mungu alikuwa anazungumza na shetani
 
huyu jamaa si mtumishi wa Mungu,ni mtu fulani mwenye nia za kisiasa na ukosoaji ila hajui anasema nini;

mtumishi gani wa Mungu kila siku unashusha mioyo ya watu ili kuwafanya wakose amani?,kama ameona korona ipo na imempata si aendelee kuamini ipo tu na sio kuanza kuaminisha na wengine wawe kama yeye?,

vipi kwanini asiunge mkono njia za yule wa chama kile moja kwa moja kama askofu miwani?

Bangonza,mimi najua wewe sio mtumishi wa Mungu,kwa sababu haubariki lolote kwenye nchi uiishiyo,sikuzuii kukosoa,bali simama na ukweli muda wote bila kuwa mbaguzi;

Mimi hapa sina chama,si mpinzani sio CCM,Maghufuli akifanya mema nampongeza,akifanya mabaya nakosoa,na sioni ubaya kwa hilo,vipi unadhani katika hili la korona huyu Rais hakufanya jambo kubwa sana kwa kuwatoa raia hofu juu ya janga hili?,na kama korona ipo kwa kiasi hiki cha uandishi wako,sema vifo na chukulia hali yetu kwanza katika uhalisia wake;

kama huu ugonjwa ungekuwepo hadi leo,sidhani kama siri isingefichuka;

askofu,unajivunjia heshima ya umri wako,mimi sikuheshimu kama mtumishi bali kutokana na umri wako;
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom