Askofu Bagonza ajiepushe na upindifu wa kimantiki unaoweza kuzaa taharuki ya kijamii bila uhalali

Ndugu yangu, category mistake ni kosa linalokusaidia kuelewa kiwango duni cha maarifa cha mzungumzaji.
Usilipigie upate. Tusaidiane kusahihisha.
Hapa tunajadili Elimu bibie siyo maoni yetu binafsi, unajua kama lugha inahukumu ? Labda kama hujihusishi na na mambo ya lugha. Shida bandiko lako umeliandika kihisia na falsafa na si uhalisia.

Hapo hakuna kosa ndiyo maana hutakuta andiko hata Moja la lugha linatia dosari kauli hiyo.

Sasa unapigia upatu wewe ambae umeamua kupindisha ukweli kwa makusudi.
 
Kwa ufupi kuna kanuni nne zinazoongoza fikra sahihi za kibindamau:
1. Law of identity
2. Law of excluded middle
3. Law of non-contradiction
4. Law of sufficient reason.

Mengine yote yanaanzia hapo.
Jielimishe
Hujajibu swali nililo kuuliza.
 
Hujasoma hoja yangu.
NImeunga mkono wazo la kubana haki za mahomofiliki walawiti.
NIkatetea haki za mahomofilia wasio walawiti.
Bagonza hatofautishi haya mawili.
Ndio ugomvi wangu na hoja yake
Nimekusoma vizuri nikakuelewa.

Sasa utawatofautisha vipi hao mahofolia wasio walawiti, na wale mahofolia ambao ni walawiti, hasa wanapokuwa kwenye public?

Hawa wote watakuwa na muonekano wa aina moja, kwasababu huo ulawiti hufanywa sirini, mlawiti hana alama usoni.

Hivyo, kitendo chochote cha kuwaacha hao mahofolia [ bila kujali kama ni walawiti au wasio walawiti] wazidi kuenea kwenye jamii, ndio utakuwa mwanzo wa kuiharibu jamii yetu, binafsi nataka makundi yote ya mahofolia yasiachwe, yabanwe.

Bado niko upande wa Askofu Bagonza.

NOTE.

Matumizi yako ya picha ya Bagonza na Lissu ndio unazidi kuiharibu mada yako, unaitoa kwenye usomi na kuipeleka kwenye siasa.

Matokeo yake wachangiaji watakuja na muelekeo wa kisiasa na kupoteza mantiki ya hoja yako ya awali, unapoleta mada kama hizi jitahidi uwe impartial, kwasababu kama ni ushoga, hata CCM upo, na picha zao zipo nyingi mitandaoni.
 
View attachment 2439993
Bagonza akiwa amemkumbatia Lissu Kwenye Uwanja wa Kayanga, Karagwe, 2020

Mwaka 2020 Bagonza alizushiwa zengwe kwamba ni shoga kwa sababu ya kujitokeza hadharani kwenye uwanja wa Kayanga, Karagwe, na kumsalimia Tundu Lissu, kwa kumkumbatia kama wafanyavyo wanyarwanda (kuhobherana).

Katika picha ile Bagonza alikuwa amemkumbatia Lissu na ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikiwa na bandiko "acheni ushoga." Picha yenyewe, maneno hayo mabaya yakiwa yameondolewa hiyo hapo juu:

Kwa ajili ya kunusuru hali, jamaa asiyejulikana aitwaye Kigogo2014 alitafuta picha za viongozi wa CCM wakiwa wanasalimiana kwa kukumbatiana kama alivyofanya Bagonza. Zengwe lililoanzishwa na kamati ya ufundi ya CCM likatulia.

KIgogo2014

Hivyo, nilitarajia kwamba, Bagonza atakuwa miongozi mwa watu watakaopinga tabia ya watu kuvikwa joho la ushoga pasipo ushahidi wa kutosha. Lakini amefanya kinyume.

Leo, kupitia mitandai ya kijamii, Benson Bagonza ameripotiwa kutamka kauli zifuatazo:

"Sikubaliani na wanaodhani ushoga ni tatizo la Ulaya. Hapa kwetu [Tanzania] tayari hali inatisha. Imebaki kidogo mashoga wataunda umoja, watajenga nyumba zao za ibada, na serikali itaufyata. Wataunda chama chao na kuwania uongozi, na serikali itanywea. Tuamke."

Ama Bagonza anatumia neno "ushoga" kumaanisha "ulawiti" au "uhomofilia."

Mtu mmwenye tatizo la uhomofilia anaitwa homofiliki. Sio kila mlawiti ni homofiliki na sio kila homofiliki ni mlawiti.

Yaani kuna mlawiti homofiliki, mlawiti asiye homofiliki, mlawiti homofiliki, na homofiliki asiye mlawiti. Hizi ni kada tatu za watu, lakini Bagonza haonekani kuzitofautisha.

Bagonza anahimiza mapambano dhidi ya makundi yote matatu, na hivyo kuhamasisha uhomofobia katika jamii. Sio sawa.

Hivyo kuna haja ya kujadili mawazo yake ili kusafisha akili za watumiaji wa mitandao ya kijamii. Naanza kwa kuonyesha makosa yake ya kimantiki.

Tatizo la Upindifu wa kimantiki

Upindifu wa kimantiki, yaani logical fallacy, ni kosa la kimantiki ambapo mwongeaji hutunga hoja inayokiuka misingi bora ya usanifu wa hoja na uendeshaji wa mijadala.

Mifano ya upindifu wa kimantiki ni tabia ya kutumia neno lenye maana nyingi bila kueleza maana inayoikusudiwa na mwongeaji (equivocation).

Mfano ni neno "ushoga" lenye maana mbili, yaani "ulawiti" au "uhomofilia."

Uhomofilia ni hali ya mtu kuvutiwa kimapenzi na watu wa jinsia yake. Na "ulawiti" ni tabia ya kufanya ngono kwa kuingiza jenitalia ya kiume kwenye rektamu.

Mfano mwingine wa Upindifu wa kimantiki ni kuongelea kitu kilicho kwenye tabaka moja, kwa kukibebesha kimakosa sifa za kitu baki kilicho kwenye tabaka jingine (category mistake).

Mfano, sauti iko katika tabaka la vitu vinavyosikika, wakati harufu iko katika tabaka la vitu vinavyonusika. Lakini, mara nyingi utasikia watu wanasema, "nasikia harufu ya chakula."

Maneno haya yanaiweka dhana ya "harufu" katika kundi moja na dhana ya "sauti." Hili ni kosa la kuchanganya pamoja kada za vitu visivyopaswa kuwekwa pamoja.

Yaani, “we say that one has committed a category mistake when she ascribes, to a certain entity, a property or properties which that entity could not have... [meaning that] one locates some entity in a category it does not belong.” (Bernard Matolino, Personhood in African Philosophy (Dorpspruit: Cluster Publications; 2014, p. 142)

Hivyo, mlawiti homofiliki, mlawiti asiye homofiliki, na homofiliki asiye mlawiti ni kada tatu za watu, kila kada ikiwa na tabia na sifa zake zinazoitofautisha.

Na kwa kawaida hatuwezi kuutambua uhomofilia wa mtu mpaka ajitangaze yeye au afanye matendo ya ulawiti wa jinsia moja.

Kupuuzia ukweli huu ni kufanya kosa la kuchanganya kada za vitu kwa kuvivisha baadhi ya vitu sifa visivyokuwa nazo.

Maana ya kwanza ya ushoga ni uhomofilia

Kwa upande mmoja, kama Bagonza anatumia neno "ushoga" kumaanisha "uhomofilia," ambayo ni sifa ya kimaumbile, kama ulivyo ufupi na urefu, weupe na weusi, ualibino na siualibino, njia pekee ya kupambana, kama anavyopendekeza, na "ushoga" ni kuwaua "mashoga" hao.

Hivyo, Bagonza hapa anahubiri tabia hatari ya uhomofobia. Sijui kama alitafakari vema juu ya uwezekano huu.

Lakini, pia Bagonza anapswa kutoa sababu nzuri ya kupambana na mahomofilia na kuacha kupambana na mazeruzeru, watu wenye tatizo la colour blindness, na matabaka ya pembezoni kama hayo.

Wote hawa wako hivyo kwa sababu za kimaumbile. Hawakuchagua hali zao.

Bagonza anasema kuwa "imebaki kidogo [mahomofiliki] wataunda umoja, watajenga nyumba zao za ibada, ... wataunda chama chao na kuwania uongozi, na serikali itanywea."

Kwa maoni haya ya Bagonza, hata "mahomofilia" wasio na tabia ya kufanya "ulawiti" hawana haki hizi. Kwa kiwango hiki maoni yake nayapinga.

Urefu, ufupi, sauti nene, sauti nyororo, umashoto, umakengeza, uzeruzeru, colour blindness, na ladhalika, ni sifa asilia walizo nazo watu kadhaa.

Lakini watu hawa hawapotezi haki zao za kibayolojia, kisaikosomatika, kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa sababu hiyo pekee.

Huenda Bagonza hauoni ukweli huu kwa sababu anaongea kama mwanateolojia. Lakini, kazi ya kujenga imani ya jamii mseto sio mradi wa wanateolojia pekee, kama nitakavyoeleza hapa chini baadaye.

Maana ya pili ya ushoga ni ulawiti

Kwa upande mwingine, kama Bagonza anatumia neno "ushoga" kumaanisha "ulawiti" kuna maswali ya kitafiti anapswa kutusaidia kuyajibu.

Tangu tupate uhuru tumefanya sensa mara tano. Hakuna takwimu za serikali zinaonyesha idadi ya mashoga nchini.

KIla mwaka serikali kupitia jeshi la Polisi na Idara ya takwimu (NBS) wanatoa takwimu za uhalifu kupitia kitabu kiitwacho TANZANIA IN FIGURES. Huku pia idadi ya mashoga haitajwi.

Lakini takwimu za mwaka 2021 zinaonyesha kuwa yalikuwepo matukio ya ulawiti 1,296.

Taarifa hiyo haisemi kama ulawiti huu ulifanywa dhidi ya wanaume au kama wanawake au kama ulifanywa na mashoga.

Lakini bado Bagonza anasema hakubaliani "na wanaodhani ushoga ni tatizo la Ulaya" kwa sababu tayari "hapa kwetu mbona hali inatisha," anasema.

Bagonza anasema kuwa "imebaki kidogo [walawiti] wataunda umoja, watajenga nyumba zao za ibada, ... wataunda chama chao na kuwania uongozi, na serikali itaufyata. Tuamke"

Kwa maoni ya Bagonza, "mahomofilia" wenye tabia ya kufanya "ulawiti" hawana haki hizi kwa sabavu ya uhalifu wao.

Sawa. Lakini msimamo huu haupaswi kuishia kwa wahalifu wa ulawiti pekee. Kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya kila mwala, iitwayo Tanzania in Figures, kuna makundi mengi ya uhalifu na yote yanapaswa kumulikwa na serikali.

Bagonza angeeleweka sana kama angesema hivi: "imebaki kidogo [wahalifu] wataunda umoja, watajenga nyumba zao za ibada, ... wataunda chama chao na kuwania uongozi, na serikali itaufyata. Tuamke."

Kwa kiwango hiki ningekubaliana naye Bagonza. Hapa kuna wezi, wala rushwa, watu wanaotelekeza watoto mitaani, wafanya biashara ya binadamu, wateka watu, na orodha inaendelea.

Na takwimu halisi za kiserikali kupitia taarifa ya Tanzania in Figures ya kila mwaka, zinaonyesha kuwa baadhi ya watu hawa tayari wana makanisa, wengine ni wamiliki wa vyombo vya habari, wengine ni maaskofu kuanzia makanisa ya kipentekoste hadi Kanisa Katoliki, wengine ni wachungaji, na Bagonza anaujua ukweli huu fika. Hizi hapa:

View attachment 2439942

Lakini bado Bagonza kaamua kuibuka na habari ya "ushoga" isiyo na takwimu za kitafiti.

Angeleweka na kukubalika zaidi kama angesema kuna "mashoga" wangapi kwenye kaya yake, ukoo wake, kijiji/mtaa wake wa Mwisho wa Lami, kata yake ya Kayanga, wilaya yake ya Karagwe na mkoa wake wa Kagera. Hakutoa takwimu zozote katika ngazi hizi.

Hivyo, napenda kumkumbusha kuwa, sifa tata za kimaumbile hazifuti haki za msingi za mahomofilia, maalibino, mashoto, na wenye makengeza, nk.

Sifa hizo ni kama vile haki ya kuishi, kujumuika, kugombea nafasi za kisiasa, kupiga kura, kuabudu, kulindwa na serikali, na haki baki za kibinadamu.

Changamoto ya social constructionism

Kwa maoni yangu, tamko la Bagonza linaambatana na makosa mawili ya kimantiki: equivocation and category mistake.

Bahati mbaya, kwa sehemu kubwa, hadhira inayomsikiliza Bagonza, haina weledi wa kuyabaini haya makosa.

Lakini, kazi ya kujenga imani ya jamii yenye utulivu na amani inapaswa kuongozwa na kanuni bora za usanifu, utetezi na ubomozi wa hoja.

Vinginevyo tutawalisha watu matango pori, na kupanda magugu katika Taifa letu. Sio haki.

Ukisoma vizuri mawazo ya Bagonza utaona kuwa yanaongozwa na kanuni za kambi ya wanazuoni makuwadi wa nadharia ya social constructionism, yaani nadharia za ukweli wa kiontolojia unaotengenezwa na binadamu, kama vile Profesa John Rogers Searle (Amerika).

View attachment 2438877
Profesa John Searle, mtalaama wa social constructionism iliyo msingi wa maadili yanayobadilika kwa sababu ya mazingira na iliyo mbadala kwa social realism iliyo msingi wa maadili yasiyobadilika kwa sababu ya mazingira

Katika maandiko yake, John Rogers Searle’s kuhusu ukweli wa kiontolojia unaotengenezwa na binadamu (social ontology), anatala kanuni kadhaa kuhusiana na ujio wa ukweli wa kijamii (social reality).

Kanuni moja inahusu "collective intentionality," nyingine inahusu "the assignment of status functions," na kanuni ya tatu inahusu "constitutive rules." Ninataka kuongelea hii kanuni ya tatu, ambayo ni kanuni ya kubuni na kutumia alama.

Kanuni hii inasema hivi: watu wanaweza kukaa wakakubaliana kwamba katika mazingira haya (X), kitu hiki (Y) kitakuwa alama inayowakilisha kitu kile (Z), na mapatano haya yatakoma pale watakapokaa tena na kukubaliana kuyabadilisha. (John R. Searle, Speech acts: An essay in the philosophy of language (Cambridge University Press; 1969, p. 34))

Mfano wake muhimu ni jumuiya ya wanampira waliokubaliana kuwa, katika mazigira ya uwanja wa mpira wa miguu (X), mchezaji akipokea mpira wakati anaelekea kufunga kwenye goli la mpizani wake wakati mbele yake hakuna mchezaji wa timu pinzani (Y), basi hilo ni kosa linaitwa offside (Z).

Kanuni hii inafaa kwenye mpira wa miguu pekee, na sio kwenye mpira wa mikono wala kwenye mpira wa kikapu.

Kwa hiyo, ikitokea siku wachezaji wa michezo yote hii wakajikuta wako pamoja kwa ajili ya mchezo mmoja, itabidi waunde kanuni mpya zinazokubalika kwa wote na kuwafaa wote. Ni vivyo hivyo kwenye maisha ya jamii mseto.

Yaani, kanuni zenye kutokana na mchakato wa mapatano ya kijamii (social constructionism) zinaweza kutumika kwenye jamii ya watu wenye imani moja, lakini sio kwenye jamii za leo ambako kuna utitiri wa kifikra (plural society).

Mfano, wakati wa Papa Yohanne Paulo II, baadhi ya viongozi wa Kanisa Katoliki waliweka msimamo kwamba mahunta sio binadamu.

Mfano wa mwathirika ni Padre Selwyn Gross (jina la zamani la kiume) na baadaye Padre Sally Gross (jina jipya la kike), baada ya kubadilisha jinsia yake.

Hivyo, "Padre Sally Gross" aliyekuwa hunta (intersexual), alivuliwa upadre, kwa kuwa wanawake hawana haki ya kuwa mapadre.

Pia alifutiwa ubatizo kwa hoja kwamba mahunta sio binadamu, na hivyo hawana haki ya kubatizwa.

Lakini, sayansi mamboleo inathibitisha mahunta wana kromozomu 46 kama watu baki walioko kwenye ukoo wa homosapiensia.

Yaani kumwondoa Padre Sally kwenye tabaka la binadamu ulikuwa ni uamuzi wenye sura ya "category mistake."

Hivyo, Kanisa Katoliki sasa limejisahihishana halibebi tena mawazo yale potofu kuhusu hulka ya mahunta. Kanuni za maumbile ziliwaleta karibu na ukweli.

Kwa sasa bado Kanisa Katoliki linapambana na fundisho lake tata kwamba "a copulating pair is a biological organism"

Fundisho hili ni zao la mradi wa social constructionism wa miaka ya 1968, na ni fundisho linalopingana na kanuni za kibayolojia na kifalsafa.

Kifalsafa, neno "organism" lina maana tatu. Yaani "biological organism" kama vile binadamu na kondoo; "social organism" kama vile familia na timu a mpira; na "mechanical organism" kama vile gari au saa ya kuhesabu majira.

Ufanano wake ni kwamba, aina zote tatu ni mifumo yenye sehemu nyingi zinazofanya kazi kwa kushirikiana bila kupingana kwa ajili ya kufanikisha lengo la pamoja.

Tofauti kati ya "biological organism" kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine, "social organism" na "mechanical organism" ni kwamba, wakati "kanuni ya uratibu" iko ndani ya "biological organism," kauni hiyo iko nje ya "social organism" na "mechanical organism"

Tofauti kati ya "biological organism" na "social organism" ni kwamba, kiungo cha mwili wa "biological organism" kikikatwa kinakufa, lakini kiungo cha mwili wa "social organism" kikikatwa hakifi.

Mfano, mchezaji wa mpira wa miguu akipewa kadi nyekundi anaondoka uwanjani na anabaki hai. Lakini, mkono wako ukikatawa unaoza haraka.

Kwa upande mwingine uhai wa "social organism" unaanzia na kukomea kwenye mapatano ya kijamii kati ya wanachama husika. Lakini uhai wa "biological organism" hauko hivyo.

Na "mechanical organism" inaendeshwa na dereva ambaye sio sehemu yake. Mfano kujaza ufunguo kwenye saa ya kamani, kuendesha gari.

Kwa sababu hizi, sasa ulimwengu wa wanasayansi unakubaliana kwamba "a copulating pair is a social organism," na sio "biological organism," kama inavyodaiwa na baadhi ya makuwadi wa "teolojia ya mwili mmoja," yaani, "theology of one bodily union"

Lakini bado mijadala inaendelea na wataalam wa falsafa ya kibayolojia (philosophical biology) hapa wamesaidia sana kuleta mapinduzi ya kifikra yanayotakiwa kuhusiana na swali hili hapa: "what is biological individuality?"

Msingi wa kimetafizikia wa kanuni za maadili asilia, sio nadharia ya ukweli uliofinyangwa na watu na utakaokufa pale watu watakapokubaliana kuukataa (social constructionism), bali nadharia ya ukweli unaogunduliwa na watu na utakaoendelea kuwepo hata kama watu wataukataa (social realism).

Hitimisho na mapendekezo

Kwa hiyo, njia pekee ya kujenga imani ya jamii inayokubalika kwa watu wote katika jamii yenye mapokeo mseto sio kutumia kanuni za social constructionism zinazoanzia kwenye "kanuni za taharuki ya kijamii isiyo na uhalali" (unwarranted moral panic)

Badala yake, tunapaswa kuanzia kwenye kanuni za maadili asilia yanayoweza, na yanayopaswa, kuthibitika kwa njia ya urazini huru miongoni mwa umma mpana (public reason).

Bila kukubaliana na ukweli huu, kazi ya ujenzi wa imani ya jamii yenye imani mseto itakwama, maana mwafaka wa kijamii ni ajenda ya mpito tu.

Mwisho, niseme tu kuwa, katika mradi huu wa kujenga imani ya jamii, wadau wote, yaani wanateolojia, wanasayansi asilia, wanasayansi ya jamii, wanafalsafa, wanasasiolojia, wanahistoria, wanasheria, na wanazuoni baki wanayo nafasi.

Lakini, mchango wa kila mmoja una mipaka inayokamilishwa na michango ya wenzake.

Mfano, kwenye Safina ya Nuhu tunaambiwa kuwa Nuhu aliagizwa kuweka kila kiumbe kwa kuzingatia kanuni ya ME na KE.

Lakini, leo hii sayansi inatwambia kuwa kuna viumbe havina mgawanyo huo wa ME na KE. Mfano ni minyoo. Kwa hiyo, mwandishi wa Agano la Kale hakuwa na habari ya ukweli huu wa viumbe wasio na mgawanyo wa jinsia ya ME na KE.

Na hii maana yeke ni kwamba, wanateolojia wanaofanya udadavuzi kwa kuanzia kwenye Biblia wanahitaji kuelimishwa na wanabayolojia katika suala ya asexual reporoduction. Biblia haina mamlaka katika jambo hili.

Sote tunakamilishana kimaarifa, na hivyo kuna haja ya kuunganisha nguvu katika kufanikisha mradi wa kujenga imani ya jamii yenye utulivu, haki na amani.

Tujenge hoja bila mihemuko wala taharuki.
Nimesoma yote. Ila kwa nini utumie ubongo wako kuona negative tu? Kukumbatiana inaweza kuwa ishara ya upendo. PSYCH-K
 
Sasa utawatofautisha vipi hao mahofolia wasio walawiti, na wale mahofolia ambao ni walawiti, hasa wanapokuwa kwenye public?
HUwezi kuwatofautisha.
Hapo ndipo upiga ramli wa kuwavisha joho ya ushoga watu unapokosa nguvu.
KUna vipimo vya kisayansi vtumike.
Nukta
 
Nimesoma yote. Ila kwa nini utumie ubongo wako kuona negative tu? Kukumbatiana inaweza kuwa ishara ya upendo.
Nakubaliana nawe.
Nami hoja yangu ni kwamba Watanzania wengi wana wepesi wa kutumia fallacy of association kutengeneza sleepery slop argumentszinazojadili ushoga, wakati hilo sio tatizo la kijamii kwetu hapa Tanzania.
 
Matumizi yako ya picha ya Bagonza na Lissu ndio unazidi kuiharibu mada yako, unaitoa kwenye usomi na kuipeleka kwenye siasa.

Matokeo yake wachangiaji watakuja na muelekeo wa kisiasa na kupoteza mantiki ya hoja yako ya awali, unapoleta mada kama hizi jitahidi uwe impartial, kwasababu kama ni ushoga, hata CCM upo, na picha zao zipo nyingi mitandaoni.
Sorry, hujaona ninachotaka ukione kwenye picha hiyo. For sure, picha hii ni mwafaka.
Natumia picha halisi kunyesha uzoba wa kifikra tulio nao Watanzania.
Bahati mbaya hata mwanazuoni kama Bagonza ametumbukia kwenye mtaro huo.
 
ila nawe umetumia neno la kidikiteta la kuwafunga watu midomo "taharuki".
Neno "taharuki sio neno la kidikteta.
NImetafsiri "moral panic" ambayo ni maneno rasmi katikamijadala kama hii.
Bagonza anaelewa vema sana.
 
View attachment 2439993
Bagonza akiwa amemkumbatia Lissu Kwenye Uwanja wa Kayanga, Karagwe, 2020

Mwaka 2020 Bagonza alizushiwa zengwe kwamba ni shoga kwa sababu ya kujitokeza hadharani kwenye uwanja wa Kayanga, Karagwe, na kumsalimia Tundu Lissu, kwa kumkumbatia kama wafanyavyo wanyarwanda (kuhobherana).

Katika picha ile Bagonza alikuwa amemkumbatia Lissu na ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikiwa na bandiko "acheni ushoga." Picha yenyewe, maneno hayo mabaya yakiwa yameondolewa hiyo hapo juu:

Kwa ajili ya kunusuru hali, jamaa asiyejulikana aitwaye Kigogo2014 alitafuta picha za viongozi wa CCM wakiwa wanasalimiana kwa kukumbatiana kama alivyofanya Bagonza. Zengwe lililoanzishwa na kamati ya ufundi ya CCM likatulia.

KIgogo2014

Hivyo, nilitarajia kwamba, Bagonza atakuwa miongozi mwa watu watakaopinga tabia ya watu kuvikwa joho la ushoga pasipo ushahidi wa kutosha. Lakini amefanya kinyume.

Leo, kupitia mitandai ya kijamii, Benson Bagonza ameripotiwa kutamka kauli zifuatazo:

"Sikubaliani na wanaodhani ushoga ni tatizo la Ulaya. Hapa kwetu [Tanzania] tayari hali inatisha. Imebaki kidogo mashoga wataunda umoja, watajenga nyumba zao za ibada, na serikali itaufyata. Wataunda chama chao na kuwania uongozi, na serikali itanywea. Tuamke."

Ama Bagonza anatumia neno "ushoga" kumaanisha "ulawiti" au "uhomofilia."

Mtu mmwenye tatizo la uhomofilia anaitwa homofiliki. Sio kila mlawiti ni homofiliki na sio kila homofiliki ni mlawiti.

Yaani kuna mlawiti homofiliki, mlawiti asiye homofiliki, mlawiti homofiliki, na homofiliki asiye mlawiti. Hizi ni kada tatu za watu, lakini Bagonza haonekani kuzitofautisha.

Bagonza anahimiza mapambano dhidi ya makundi yote matatu, na hivyo kuhamasisha uhomofobia katika jamii. Sio sawa.

Hivyo kuna haja ya kujadili mawazo yake ili kusafisha akili za watumiaji wa mitandao ya kijamii. Naanza kwa kuonyesha makosa yake ya kimantiki.

Tatizo la Upindifu wa kimantiki

Upindifu wa kimantiki, yaani logical fallacy, ni kosa la kimantiki ambapo mwongeaji hutunga hoja inayokiuka misingi bora ya usanifu wa hoja na uendeshaji wa mijadala.

Mifano ya upindifu wa kimantiki ni tabia ya kutumia neno lenye maana nyingi bila kueleza maana inayoikusudiwa na mwongeaji (equivocation).

Mfano ni neno "ushoga" lenye maana mbili, yaani "ulawiti" au "uhomofilia."

Uhomofilia ni hali ya mtu kuvutiwa kimapenzi na watu wa jinsia yake. Na "ulawiti" ni tabia ya kufanya ngono kwa kuingiza jenitalia ya kiume kwenye rektamu.

Mfano mwingine wa Upindifu wa kimantiki ni kuongelea kitu kilicho kwenye tabaka moja, kwa kukibebesha kimakosa sifa za kitu baki kilicho kwenye tabaka jingine (category mistake).

Mfano, sauti iko katika tabaka la vitu vinavyosikika, wakati harufu iko katika tabaka la vitu vinavyonusika. Lakini, mara nyingi utasikia watu wanasema, "nasikia harufu ya chakula."

Maneno haya yanaiweka dhana ya "harufu" katika kundi moja na dhana ya "sauti." Hili ni kosa la kuchanganya pamoja kada za vitu visivyopaswa kuwekwa pamoja.

Yaani, “we say that one has committed a category mistake when she ascribes, to a certain entity, a property or properties which that entity could not have... [meaning that] one locates some entity in a category it does not belong.” (Bernard Matolino, Personhood in African Philosophy (Dorpspruit: Cluster Publications; 2014, p. 142)

Hivyo, mlawiti homofiliki, mlawiti asiye homofiliki, na homofiliki asiye mlawiti ni kada tatu za watu, kila kada ikiwa na tabia na sifa zake zinazoitofautisha.

Na kwa kawaida hatuwezi kuutambua uhomofilia wa mtu mpaka ajitangaze yeye au afanye matendo ya ulawiti wa jinsia moja.

Kupuuzia ukweli huu ni kufanya kosa la kuchanganya kada za vitu kwa kuvivisha baadhi ya vitu sifa visivyokuwa nazo.

Maana ya kwanza ya ushoga ni uhomofilia

Kwa upande mmoja, kama Bagonza anatumia neno "ushoga" kumaanisha "uhomofilia," ambayo ni sifa ya kimaumbile, kama ulivyo ufupi na urefu, weupe na weusi, ualibino na siualibino, njia pekee ya kupambana, kama anavyopendekeza, na "ushoga" ni kuwaua "mashoga" hao.

Hivyo, Bagonza hapa anahubiri tabia hatari ya uhomofobia. Sijui kama alitafakari vema juu ya uwezekano huu.

Lakini, pia Bagonza anapswa kutoa sababu nzuri ya kupambana na mahomofilia na kuacha kupambana na mazeruzeru, watu wenye tatizo la colour blindness, na matabaka ya pembezoni kama hayo.

Wote hawa wako hivyo kwa sababu za kimaumbile. Hawakuchagua hali zao.

Bagonza anasema kuwa "imebaki kidogo [mahomofiliki] wataunda umoja, watajenga nyumba zao za ibada, ... wataunda chama chao na kuwania uongozi, na serikali itanywea."

Kwa maoni haya ya Bagonza, hata "mahomofilia" wasio na tabia ya kufanya "ulawiti" hawana haki hizi. Kwa kiwango hiki maoni yake nayapinga.

Urefu, ufupi, sauti nene, sauti nyororo, umashoto, umakengeza, uzeruzeru, colour blindness, na ladhalika, ni sifa asilia walizo nazo watu kadhaa.

Lakini watu hawa hawapotezi haki zao za kibayolojia, kisaikosomatika, kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa sababu hiyo pekee.

Huenda Bagonza hauoni ukweli huu kwa sababu anaongea kama mwanateolojia. Lakini, kazi ya kujenga imani ya jamii mseto sio mradi wa wanateolojia pekee, kama nitakavyoeleza hapa chini baadaye.

Maana ya pili ya ushoga ni ulawiti

Kwa upande mwingine, kama Bagonza anatumia neno "ushoga" kumaanisha "ulawiti" kuna maswali ya kitafiti anapswa kutusaidia kuyajibu.

Tangu tupate uhuru tumefanya sensa mara tano. Hakuna takwimu za serikali zinaonyesha idadi ya mashoga nchini.

KIla mwaka serikali kupitia jeshi la Polisi na Idara ya takwimu (NBS) wanatoa takwimu za uhalifu kupitia kitabu kiitwacho TANZANIA IN FIGURES. Huku pia idadi ya mashoga haitajwi.

Lakini takwimu za mwaka 2021 zinaonyesha kuwa yalikuwepo matukio ya ulawiti 1,296.

Taarifa hiyo haisemi kama ulawiti huu ulifanywa dhidi ya wanaume au kama wanawake au kama ulifanywa na mashoga.

Lakini bado Bagonza anasema hakubaliani "na wanaodhani ushoga ni tatizo la Ulaya" kwa sababu tayari "hapa kwetu mbona hali inatisha," anasema.

Bagonza anasema kuwa "imebaki kidogo [walawiti] wataunda umoja, watajenga nyumba zao za ibada, ... wataunda chama chao na kuwania uongozi, na serikali itaufyata. Tuamke"

Kwa maoni ya Bagonza, "mahomofilia" wenye tabia ya kufanya "ulawiti" hawana haki hizi kwa sabavu ya uhalifu wao.

Sawa. Lakini msimamo huu haupaswi kuishia kwa wahalifu wa ulawiti pekee. Kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya kila mwala, iitwayo Tanzania in Figures, kuna makundi mengi ya uhalifu na yote yanapaswa kumulikwa na serikali.

Bagonza angeeleweka sana kama angesema hivi: "imebaki kidogo [wahalifu] wataunda umoja, watajenga nyumba zao za ibada, ... wataunda chama chao na kuwania uongozi, na serikali itaufyata. Tuamke."

Kwa kiwango hiki ningekubaliana naye Bagonza. Hapa kuna wezi, wala rushwa, watu wanaotelekeza watoto mitaani, wafanya biashara ya binadamu, wateka watu, na orodha inaendelea.

Na takwimu halisi za kiserikali kupitia taarifa ya Tanzania in Figures ya kila mwaka, zinaonyesha kuwa baadhi ya watu hawa tayari wana makanisa, wengine ni wamiliki wa vyombo vya habari, wengine ni maaskofu kuanzia makanisa ya kipentekoste hadi Kanisa Katoliki, wengine ni wachungaji, na Bagonza anaujua ukweli huu fika. Hizi hapa:

View attachment 2439942

Lakini bado Bagonza kaamua kuibuka na habari ya "ushoga" isiyo na takwimu za kitafiti.

Angeleweka na kukubalika zaidi kama angesema kuna "mashoga" wangapi kwenye kaya yake, ukoo wake, kijiji/mtaa wake wa Mwisho wa Lami, kata yake ya Kayanga, wilaya yake ya Karagwe na mkoa wake wa Kagera. Hakutoa takwimu zozote katika ngazi hizi.

Hivyo, napenda kumkumbusha kuwa, sifa tata za kimaumbile hazifuti haki za msingi za mahomofilia, maalibino, mashoto, na wenye makengeza, nk.

Sifa hizo ni kama vile haki ya kuishi, kujumuika, kugombea nafasi za kisiasa, kupiga kura, kuabudu, kulindwa na serikali, na haki baki za kibinadamu.

Changamoto ya social constructionism

Kwa maoni yangu, tamko la Bagonza linaambatana na makosa mawili ya kimantiki: equivocation and category mistake.

Bahati mbaya, kwa sehemu kubwa, hadhira inayomsikiliza Bagonza, haina weledi wa kuyabaini haya makosa.

Lakini, kazi ya kujenga imani ya jamii yenye utulivu na amani inapaswa kuongozwa na kanuni bora za usanifu, utetezi na ubomozi wa hoja.

Vinginevyo tutawalisha watu matango pori, na kupanda magugu katika Taifa letu. Sio haki.

Ukisoma vizuri mawazo ya Bagonza utaona kuwa yanaongozwa na kanuni za kambi ya wanazuoni makuwadi wa nadharia ya social constructionism, yaani nadharia za ukweli wa kiontolojia unaotengenezwa na binadamu, kama vile Profesa John Rogers Searle (Amerika).

View attachment 2438877
Profesa John Searle, mtalaama wa social constructionism iliyo msingi wa maadili yanayobadilika kwa sababu ya mazingira na iliyo mbadala kwa social realism iliyo msingi wa maadili yasiyobadilika kwa sababu ya mazingira

Katika maandiko yake, John Rogers Searle’s kuhusu ukweli wa kiontolojia unaotengenezwa na binadamu (social ontology), anatala kanuni kadhaa kuhusiana na ujio wa ukweli wa kijamii (social reality).

Kanuni moja inahusu "collective intentionality," nyingine inahusu "the assignment of status functions," na kanuni ya tatu inahusu "constitutive rules." Ninataka kuongelea hii kanuni ya tatu, ambayo ni kanuni ya kubuni na kutumia alama.

Kanuni hii inasema hivi: watu wanaweza kukaa wakakubaliana kwamba katika mazingira haya (X), kitu hiki (Y) kitakuwa alama inayowakilisha kitu kile (Z), na mapatano haya yatakoma pale watakapokaa tena na kukubaliana kuyabadilisha. (John R. Searle, Speech acts: An essay in the philosophy of language (Cambridge University Press; 1969, p. 34))

Mfano wake muhimu ni jumuiya ya wanampira waliokubaliana kuwa, katika mazigira ya uwanja wa mpira wa miguu (X), mchezaji akipokea mpira wakati anaelekea kufunga kwenye goli la mpizani wake wakati mbele yake hakuna mchezaji wa timu pinzani (Y), basi hilo ni kosa linaitwa offside (Z).

Kanuni hii inafaa kwenye mpira wa miguu pekee, na sio kwenye mpira wa mikono wala kwenye mpira wa kikapu.

Kwa hiyo, ikitokea siku wachezaji wa michezo yote hii wakajikuta wako pamoja kwa ajili ya mchezo mmoja, itabidi waunde kanuni mpya zinazokubalika kwa wote na kuwafaa wote. Ni vivyo hivyo kwenye maisha ya jamii mseto.

Yaani, kanuni zenye kutokana na mchakato wa mapatano ya kijamii (social constructionism) zinaweza kutumika kwenye jamii ya watu wenye imani moja, lakini sio kwenye jamii za leo ambako kuna utitiri wa kifikra (plural society).

Mfano, wakati wa Papa Yohanne Paulo II, baadhi ya viongozi wa Kanisa Katoliki waliweka msimamo kwamba mahunta sio binadamu.

Mfano wa mwathirika ni Padre Selwyn Gross (jina la zamani la kiume) na baadaye Padre Sally Gross (jina jipya la kike), baada ya kubadilisha jinsia yake.

Hivyo, "Padre Sally Gross" aliyekuwa hunta (intersexual), alivuliwa upadre, kwa kuwa wanawake hawana haki ya kuwa mapadre.

Pia alifutiwa ubatizo kwa hoja kwamba mahunta sio binadamu, na hivyo hawana haki ya kubatizwa.

Lakini, sayansi mamboleo inathibitisha mahunta wana kromozomu 46 kama watu baki walioko kwenye ukoo wa homosapiensia.

Yaani kumwondoa Padre Sally kwenye tabaka la binadamu ulikuwa ni uamuzi wenye sura ya "category mistake."

Hivyo, Kanisa Katoliki sasa limejisahihishana halibebi tena mawazo yale potofu kuhusu hulka ya mahunta. Kanuni za maumbile ziliwaleta karibu na ukweli.

Kwa sasa bado Kanisa Katoliki linapambana na fundisho lake tata kwamba "a copulating pair is a biological organism"

Fundisho hili ni zao la mradi wa social constructionism wa miaka ya 1968, na ni fundisho linalopingana na kanuni za kibayolojia na kifalsafa.

Kifalsafa, neno "organism" lina maana tatu. Yaani "biological organism" kama vile binadamu na kondoo; "social organism" kama vile familia na timu a mpira; na "mechanical organism" kama vile gari au saa ya kuhesabu majira.

Ufanano wake ni kwamba, aina zote tatu ni mifumo yenye sehemu nyingi zinazofanya kazi kwa kushirikiana bila kupingana kwa ajili ya kufanikisha lengo la pamoja.

Tofauti kati ya "biological organism" kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine, "social organism" na "mechanical organism" ni kwamba, wakati "kanuni ya uratibu" iko ndani ya "biological organism," kauni hiyo iko nje ya "social organism" na "mechanical organism"

Tofauti kati ya "biological organism" na "social organism" ni kwamba, kiungo cha mwili wa "biological organism" kikikatwa kinakufa, lakini kiungo cha mwili wa "social organism" kikikatwa hakifi.

Mfano, mchezaji wa mpira wa miguu akipewa kadi nyekundi anaondoka uwanjani na anabaki hai. Lakini, mkono wako ukikatawa unaoza haraka.

Kwa upande mwingine uhai wa "social organism" unaanzia na kukomea kwenye mapatano ya kijamii kati ya wanachama husika. Lakini uhai wa "biological organism" hauko hivyo.

Na "mechanical organism" inaendeshwa na dereva ambaye sio sehemu yake. Mfano kujaza ufunguo kwenye saa ya kamani, kuendesha gari.

Kwa sababu hizi, sasa ulimwengu wa wanasayansi unakubaliana kwamba "a copulating pair is a social organism," na sio "biological organism," kama inavyodaiwa na baadhi ya makuwadi wa "teolojia ya mwili mmoja," yaani, "theology of one bodily union"

Lakini bado mijadala inaendelea na wataalam wa falsafa ya kibayolojia (philosophical biology) hapa wamesaidia sana kuleta mapinduzi ya kifikra yanayotakiwa kuhusiana na swali hili hapa: "what is biological individuality?"

Msingi wa kimetafizikia wa kanuni za maadili asilia, sio nadharia ya ukweli uliofinyangwa na watu na utakaokufa pale watu watakapokubaliana kuukataa (social constructionism), bali nadharia ya ukweli unaogunduliwa na watu na utakaoendelea kuwepo hata kama watu wataukataa (social realism).

Hitimisho na mapendekezo

Kwa hiyo, njia pekee ya kujenga imani ya jamii inayokubalika kwa watu wote katika jamii yenye mapokeo mseto sio kutumia kanuni za social constructionism zinazoanzia kwenye "kanuni za taharuki ya kijamii isiyo na uhalali" (unwarranted moral panic)

Badala yake, tunapaswa kuanzia kwenye kanuni za maadili asilia yanayoweza, na yanayopaswa, kuthibitika kwa njia ya urazini huru miongoni mwa umma mpana (public reason).

Bila kukubaliana na ukweli huu, kazi ya ujenzi wa imani ya jamii yenye imani mseto itakwama, maana mwafaka wa kijamii ni ajenda ya mpito tu.

Mwisho, niseme tu kuwa, katika mradi huu wa kujenga imani ya jamii, wadau wote, yaani wanateolojia, wanasayansi asilia, wanasayansi ya jamii, wanafalsafa, wanasasiolojia, wanahistoria, wanasheria, walei, makasisi, na wanazuoni baki wanayo nafasi.

Lakini, mchango wa kila mmoja una mipaka inayokamilishwa na michango ya wenzake.

Mfano, kwenye Safina ya Nuhu tunaambiwa kuwa Nuhu aliagizwa kuweka kila kiumbe kwa kuzingatia kanuni ya ME na KE.

Lakini, leo hii sayansi inatwambia kuwa kuna viumbe havina mgawanyo huo wa ME na KE. Mfano ni minyoo. Kwa hiyo, mwandishi wa Agano la Kale hakuwa na habari ya ukweli huu wa viumbe wasio na mgawanyo wa jinsia ya ME na KE.

Na hii maana yeke ni kwamba, wanateolojia wanaofanya udadavuzi kwa kuanzia kwenye Biblia wanahitaji kuelimishwa na wanabayolojia katika suala ya asexual reporoduction. Biblia haina mamlaka katika jambo hili.

Sote tunakamilishana kimaarifa, na hivyo kuna haja ya kuunganisha nguvu katika kufanikisha mradi wa kujenga imani ya jamii yenye utulivu, haki na amani.

Tujenge hoja bila mihemuko wala taharuki.
Huyu Askofu, tangu alipounganan na yule Askofu wa Konde ambaye ni mwizi na kuwa na matatizo mengi, simuweki maanani sana.
Ni mchumia tumbo kama wengine.
 
Upindifu wa kimantiki kwenye public discourse ni kosa kubwa.
Kauli mfagio (unsupportee claims) kwenye midahalo ni kosa kubwa.
Sawa...

Japo sijui alikuwa anaongea akiwa wapi, lakini kama alichokiongea kililenga umma wote kwa ujumla wake, bado nasema hakuna kosa kwa sababu ujumbe wa kuwa "ushoga ni kosa la kimaadili" katika jamii yetu umefika na kueleweka vyema...

Hilo la kutafuta "makosa ya kimantiki" ni la kwenu wana taaluma mnapotaka kupeleka paper mbele ya jopo la wana - taaluma ili kufanyiwa assessment ya PhD yako...

Jamii inahitaji ujumbe ulio straight forward ktk lugha rahisi na ya kueleweka..

Mfano;

✓ Iambie jamii kuwa wizi ni mbaya na hatari ili mtu aepuke hata kufikiri tu kuchukua kitu kisicho chake...

AU

✓ Au, waambie straight forward kumuua (kumwaga) damu ya mwenzako ni dhambi mbele ya Mungu na ni kosa la kimaadili pia. Usiingize mambo ya sijui kuna kuua bila kukusudia ama kukusudia..

Hayo ni ya baadae huko mbeleni kama ikilazimu kuchunguza tukio fulani la mauaji. Lakini all in all, uuaji kwa ujumla wake ni kosa...!!

Sioni kosa la ujumbe wa Askofu Bagonza. Sisi wengine tumemwelewa...
 
Neno "taharuki sio neno la kidikteta.
NImetafsiri "moral panic" ambayo ni maneno rasmi katikamijadala kama hii.
Bagonza anaelewa vema sana.
Taharuki kwa tafsiri ya kimtaani mi keosi, si neno la mjadala ni neno la kumshutumu mtu kwa kutaka watu wachanganyikiwe na kusababisha vurugu, neno hili lilikuwa maarufu wakati wa mwendazake dhidi ya wabaya wao na nchi za kidikiteta dhidi ya wapinga udikiteta.
 
Sorry, picha hii ni mwafaka.
Tena kuna picha nyingine inamwinyesha Lissue akiwa anaonekana kuteuliwa kuwa mwakilishi wa Mashoga Afrika.
Natumia picha halisi kunyesha uzoba wa kifikra tulio nao Watanzania.
Bahati mbaya hata mwanazuoni kama Bagonza ametumbukia kwenye mtaro huo.
Ndio maana nilipata mashaka na sababu hasa ya kuanzisha hili bandiko lako, mwanzo uliliegemeza kielimu, lakini sasa naanza kuona unapoteza muelekeo na kwenda kwenye siasa, jambo ambalo bado nakusisitiza UNAKOSEA.

Na, unaposema unatumia picha halisi kuonesha uzoba wa waAfrica, sijui kwanini hasa utumie picha ya aina/mtu mmoja kuonesha huo uzoba, napata mashaka na nia yako, hasa nikizingatia wapo wengine, toka vyama vingine, wanaostahili kutolewa mfano kama huo wa uzoba tena waliojipambanua kwa uwazi zaidi, lakini unawaficha.

Hebu niambie;

- Lini na wapi, Lissu aliwahi kuteuliwa kuwa mwakilishi wa mashoga Afrika? hapa napenda nione na hiyo picha nyingine ya Lissu unayodai unayo.

- Inawezekana vipi mtu unayemwita mwakilishi wa mashoga Afrika akawa na familia?
 
Sorry, picha hii ni mwafaka.
Tena kuna picha nyingine inamwinyesha Lissue akiwa anaonekana kuteuliwa kuwa mwakilishi wa Mashoga Afrika.
Natumia picha halisi kunyesha uzoba wa kifikra tulio nao Watanzania.
Mmh! Kumbe ndiye mwakilishi wao?🤔
 
Back
Top Bottom