Askofu anamiliki HAMMER ya 250million!

Status
Not open for further replies.
Gwajiba passport yake imechanwa yuko chini ya uangalizi wa vyombo vya usalama kwa sasa hatuhusiwi kutoka nje ya nchi
 
Kondoo wa sku hizi kweli wabishi! mnamtolea bwana halafu mnahoji matumizi!!!!!??
mimi naona ni haki kabisa mtumishi wa bwana kununua hummer, angenunua lambo ingekuwa balaa! nachotaka kuwaambia waumini wenzangu ni kwamba kama unatoa kwa moyo mmoja hautarudi nyuma kumsengenya mchungaji wako!! na kama unamashaka naye ongea na wazee wa kanisa muwe mnasomewa mapato na matumizi!!! lakini kuongelea nyuma ya mgongo wake na wakina shigongo haina maana, unakuwa ni UNAFKI wa hali ya juu. Na kama unahisi kuipeleka sadaka yako kanisani ni kupoteza, wape maskini wapo barabarani kibao! HAKUNA MTU ananilazimisha kutoa sadaka wala fungu la kumi kanisani.
Ni kweli Amoeba, personally ni muumini wa WAPO kwa miaka mingi tu, sijawahi kumsikia akisema suti hizo ni matunda ya utumishi isipokuwa ni mkewe anamnulia. Mke wake ni msomi mwenye MSC in Finance na wala si mtumishi wa WAPO, Askof pia ni zaidi ya miaka mitatu hapokei mshahara, ni mwandishi wa vitabu, kanda zake za maombezi zinauzwa kama njugu. Gari anayoendeshwa ni mtu tu ameguswa kumpa ikiwa mpya kabisa. Binafsi sishabikii ukwasi wowote, na hata kama napata mshahara zaidi ya milioni siwezi vaa nguo ya laki tano, but kila mtu na taste zake so siwezi kumlaumu kama anapenda nguo na kujenga sehemu local, au ninapenda kuishi sehemu expensive na kuvaa cheap as long as ninatoa fungu langu la Bwana, ninatoa dhabihu na hata yatima na wajane ninawasaidia hat kuchukua na kuishi nae na kumsomesha. Hivyo msiwaseme waumini wote wa hawa wanaenda kwa hiyari yao na utashi wao, binafsi nimebarikiwa sana toka nimeanza nao, na kwakweli sijapungukiwa kitu chochote muhimu. Kama unaona kiongozi haytuko sawa unapaswa kumkemea hata Paulo alimkemea Petro alipokataa kula na wasiotahiriwa na kama husikilizwi na uko sahihi basi unaanza mbele. Sadaka yako pia unamtolea Mungu, mtumishi ni binadamu kama wewe na ana tamaa zake akikosea ni Mungu ndiye atakayemuhukumu, na hata Roho Mtakatifu atakuongoza kujua kuwa huyu mtumishi si mwaminifu na utaondoka. Kama kuna mwenye kutaka taarifa sahihi karibu WAPO Mission hakuna huo usiri wala bureaucracy kama mission nyingine. Barikiweni
 
Binafsi sioni ubaya wa hawa watumishi kuwa na mali, ubaya kwangu ni pale ambapo hawa watumishi siku hizi makanisa yamekuwa sehemu ya biashara, ni kama kurun kampuni, tena hawalipi kodi yoyote,wanatumbukia katika limbwi la utajiri huku waumini wakiswaga miguu na sh100 kumtolea mtu akanunue hummer! why kama wanawathamini waumini hizo hela wakainvest au hata kuwe na saccos then waidentfy wanaohitaji na kuwainua either kibishara au vyovyote?wahubiri hawa huwa wanaongea kwa kiburi cha utajiri,imefika hata wengine kuwagawa waumini kwa misingi ya utoaji,eg wa 1m, lk5,lk1.......hata sh100. wenye kipato zidi hupewa kipaumbele zaidi, hata kuitwa kukaa viti vya mbele! je jesus angefanya hivi tungekuwa wapi? Wahubiri wamekuwa tofauti nowdays,kila mtu ananzisha kanisa simply kumiliki waumini hence hela! Sadaka sio siri ya mtu na Mungu wake tena bali mtu na mwenye kanisa,wahubiri kuweni na kiasi, huo ni ulafi,ulafi,ulafi! na nidhambi, mlafi hatourithi ufalme wa Mungu,
 
Leo kuna mtumishi wa bwana atakaethubutu kugawa nusu ya mali yake awape maskini? Japo mali zinazidi siku baada ya siku!
 
Leo kuna mtumishi wa bwana atakaethubutu kugawa nusu ya mali yake awape maskini? Japo mali zinazidi siku baada ya siku!
Jambo usilolijua! Unafikiri mtu maisha yako yote badala ya kufanya kazi ya mshahara umekazana unawekeza kwenye kuhubiri injili, mwanzo ukiwa chini bila chochote sio kujitolea zaidi ya nusu ya mali yako? Leo hii unafikiri ingekuwa kila mtu anataka kufanya kazi za ofisi au biashara injili ingehubiriwa?? Sasa inapotokea mtu amevutwa na kumtolea mtumishi kitu ili kumrahisishia maisha yake basi kelele agawe kwa maskini, mbona Yesu alikataa mafuta expensive ya Mariamu Magdalena alisema wamwache, na huyo Yuda aliyekuwa anajifanya anawapenda maskini aliishia kupokea vipande 30! Wapi sasa tuwwa wakweli Bwana!
 
Jamani naomba Wakristo msiyumbe kiimani. Kutoa sadaka ni kutimiza maandiko yaliyo katika Biblia. Kama Watumishi wa Bwana wanazitumia vibaya basi Mwenyezi Mungu atashughulika nao. Mkristo endelea kutoa kwa ajili ya kazi ya Bwana na utabarikiwa sana.

Ikiwa unatoa sadaka huku unajua kuwa inatumika vibaya, elewa unatenda dhambi na ipo hukumu juu ya matendo hayo. Fungu la kumi linapaswa kuliwa na mchungaji, wageni, yatima na wajane. je wajane na yatima wanakumbukwa? najua wageni wa wachungaji wengi siku hizi ni ndugu zao na si wapita njia.

Labda tu conclude kuwa uchungaji leo ni kazi kama kazi nyingine na unasomewa na hiyo ndiyo marupurupu
 
Wakati wa yesu hakukuwa na Hummer bali farasi.Mbona htuambiwi alimiliki farasi wangapi?
Kulikuwa na mpaka magari ya farasi, naelewa, lakini alipotaka kuingia Yerusalem alipanda mwanapunda na watu walipmwaga nguo zao, I mean nguo sio mikeke apite juu yake, mbona hakukataza, Mwacheni Mungu aitwe Mungu, kama mtu ni tapeli hapa hapa duniani wataonekana tu, na kaburi klake je uliskia ni la tajiri wa Arimathaya, alikaribishwa chakula na watoza ushuru ina maana ni tajiri pia, Yesu hakubagua watu, so ktk waumini kuna maskini na tajiri huwezi kuchagua
 
Ikiwa unatoa sadaka huku unajua kuwa inatumika vibaya, elewa unatenda dhambi na ipo hukumu juu ya matendo hayo. Fungu la kumi linapaswa kuliwa na mchungaji, wageni, yatima na wajane. je wajane na yatima wanakumbukwa? najua wageni wa wachungaji wengi siku hizi ni ndugu zao na si wapita njia.

Labda tu conclude kuwa uchungaji leo ni kazi kama kazi nyingine na unasomewa na hiyo ndiyo marupurupu
Ndio tunawaambia nenda kawaulize au nenda nyumbani kwao Gamanywa ameishakaa na yatima, wasiojiweza na kuwasomesha wangapi? Lwakatare pia anao wangapi? Kama wana roho isiyojali yatima hata sie waumini ktk makanisa yao tungekuwa hivyo, nasi pia tumesoma na tunauelewa mkubwa tu and we are not desperate and losers like those of Kibwetere, sie tunaelewa kabisa tunachofanya na kizuri zaidi wengi wetu tumeishapitia madhehebu mengine so we know both worlds though we usually do not point our fingers to any other Christian denomination, we know one day God will show them the right way.
 
Kulikuwa na mpaka magari ya farasi, naelewa, lakini alipotaka kuingia Yerusalem alipanda mwanapunda na watu walipmwaga nguo zao, I mean nguo sio mikeke apite juu yake, mbona hakukataza, Mwacheni Mungu aitwe Mungu, kama mtu ni tapeli hapa hapa duniani wataonekana tu, na kaburi klake je uliskia ni la tajiri wa Arimathaya, alikaribishwa chakula na watoza ushuru ina maana ni tajiri pia, Yesu hakubagua watu, so ktk waumini kuna maskini na tajiri huwezi kuchagua

Bado nasisitiza kuwa Bwana Yesu mbaye wachungaji,maaskofu nk wanajaribu kumu emulate kiuongozi hakumiliki punda wala farasi kwa kuwa si mabo ya msingi kwa kiongozi wa kiroho.Unapokuja kanisani na Hummer na waumini wako wako wamekuja kwa miguu utaeleweka kweli?
 
Bado nasisitiza kuwa Bwana Yesu ambaye wachungaji,maaskofu nk wanajaribu kumu emulate kiuongozi hakumiliki punda wala farasi kwa kuwa si mambo ya msingi kwa kiongozi wa kiroho.Unapokuja kanisani na Hummer na waumini wako wako wamekuja kwa miguu utaeleweka kweli?
 
Bado nasisitiza kuwa Bwana Yesu mbaye wachungaji,maaskofu nk wanajaribu kumu emulate kiuongozi hakumiliki punda wala farasi kwa kuwa si mabo ya msingi kwa kiongozi wa kiroho.Unapokuja kanisani na Hummer na waumini wako wako wamekuja kwa miguu utaeleweka kweli?

Siwezi ingia rohoni kwa mtumishi, na nimesema sishabikii ukwasi hata kidogo, ila kama amepewa na hakuwa na gari unataka nini? pengine anatafuta mnunuzi unajuaje? So wakati anasubiri ulitaka apande daladala atukanwe na konda kisha aje kuwahubiria watu amani. Kwa vile ni mtu wa nje huwezi elewa nini kinaendelea kuna kipindi mtumishi anafunga hata kuongea anapunguza hii nimeiona hata RC mission masista wanaita mazoezi ya kiroho, ulitegemea huyu mtumishi atoke kwake na mguu na aje gombania daladala, ndio Yesu hakumiliki lakini kila alipohitaji kitu aliagiza na kilipatikana mf hela ya kodi, chumba cha karamu ya mwisho, samaki na mikate ya kuwapa maskini. But in this era sio watu wote wapo saa zote kujitolea usafiri apande mtumishi ndio kanisa linapotoa au muumini mwenye uwezo anajitolea gari na kumpa, hawajaomba. Jamani na kama unamtumikia Mungu wa kweli, basi hatakupungukia.
 
Hawa wanaojiita wachungaji wanawakwaza sana waumini wao. Wao wanapaswa kuwa mfano kwa kuishi maisha kama ya Yesu Kristo alipokuwa duniani -- maisha ya kawaida, ya kifukara. Na hiyo ndiyo nadhiri wanayoweka wakati wakipakwa mafuta. Lakini masaibu tunayoyaona humu mijini yanafanya wengi tupoteze imani na watumishi hawa wa Mungu. Wengi wao wanajilimbikizia mali na wengine ni wazinzi wakubwa. Kuna taarifa kwamba baadhi ya mapadre (tena Wakatoliki ambao wanapaswa kuishi maisha ya useja) wanatembea na wake za watu na kuzini ovyo na waumini wao wengine. Mapadre wengi sana inasadikika wamekufa kwa AIDS, ugonjwa ambao chanzo chake kikuu ni ngono zembe. Ni aibu!
 
Siwezi ingia rohoni kwa mtumishi, na nimesema sishabikii ukwasi hata kidogo, ila kama amepewa na hakuwa na gari unataka nini? pengine anatafuta mnunuzi unajuaje? So wakati anasubiri ulitaka apande daladala atukanwe na konda kisha aje kuwahubiria watu amani. Kwa vile ni mtu wa nje huwezi elewa nini kinaendelea kuna kipindi mtumishi anafunga hata kuongea anapunguza hii nimeiona hata RC mission masista wanaita mazoezi ya kiroho, ulitegemea huyu mtumishi atoke kwake na mguu na aje gombania daladala, ndio Yesu hakumiliki lakini kila alipohitaji kitu aliagiza na kilipatikana mf hela ya kodi, chumba cha karamu ya mwisho, samaki na mikate ya kuwapa maskini. But in this era sio watu wote wapo saa zote kujitolea usafiri apande mtumishi ndio kanisa linapotoa au muumini mwenye uwezo anajitolea gari na kumpa, hawajaomba. Jamani na kama unamtumikia Mungu wa kweli, basi hatakupungukia.

Tumsifu YESU KRISTO..
 
Hawa wanaojiita wachungaji wanawakwaza sana waumini wao. Wao wanapaswa kuwa mfano kwa kuishi maisha kama ya Yesu Kristo alipokuwa duniani -- maisha ya kawaida, ya kifukara. Na hiyo ndiyo nadhiri wanayoweka wakati wakipakwa mafuta. Lakini masaibu tunayoyaona humu mijini yanafanya wengi tupoteze imani na watumishi hawa wa Mungu. Wengi wao wanajilimbikizia mali na wengine ni wazinzi wakubwa. Kuna taarifa kwamba baadhi ya mapadre (tena Wakatoliki ambao wanapaswa kuishi maisha ya useja) wanatembea na wake za watu na kuzini ovyo na waumini wao wengine. Mapadre wengi sana inasadikika wamekufa kwa AIDS, ugonjwa ambao chanzo chake kikuu ni ngono zembe.

Amen wakati wa Yesu, alikuwepo Yuda pia, na Petro alimkana japo kwa masaa lakini alimweka kuwa kiongozi mkuu, Mungu wetu ni mwema na mwenye rehema ukikosa unatubu anasamehe, jaribu kuwaaambia hao wanaokosa pengine wamejisahau kama Petro, jogoo akiwika watakumbuka na kujuta sana....bado tupo safarini, karibu kundini usiogope!
 
Tatizo ninaloliona kwa hawa Wachungaji, mitume, maaskofu, manabii ni kwamba wanaowakamua ni watu masikini kabisa katika jamii yetu, watu wenye elimu na uelewa mdogo kabisa, wengi wao wanawake wa majumbani na mitaani.
Kuna namna ya kuwadhibiti brainwashers hawa?
 
Oh NO! Don't spoil the game! wengi wao wanapata economical and spitritual refuge! including me! and we don't leave there empty handed so hands off our back please!:D
 
Siwezi ingia rohoni kwa mtumishi, na nimesema sishabikii ukwasi hata kidogo, ila kama amepewa na hakuwa na gari unataka nini? pengine anatafuta mnunuzi unajuaje? So wakati anasubiri ulitaka apande daladala atukanwe na konda kisha aje kuwahubiria watu amani. Kwa vile ni mtu wa nje huwezi elewa nini kinaendelea kuna kipindi mtumishi anafunga hata kuongea anapunguza hii nimeiona hata RC mission masista wanaita mazoezi ya kiroho, ulitegemea huyu mtumishi atoke kwake na mguu na aje gombania daladala, ndio Yesu hakumiliki lakini kila alipohitaji kitu aliagiza na kilipatikana mf hela ya kodi, chumba cha karamu ya mwisho, samaki na mikate ya kuwapa maskini. But in this era sio watu wote wapo saa zote kujitolea usafiri apande mtumishi ndio kanisa linapotoa au muumini mwenye uwezo anajitolea gari na kumpa, hawajaomba. Jamani na kama unamtumikia Mungu wa kweli, basi hatakupungukia.

Hakutakiwa kukubali kupokea gari linalosifika kwa kuchafua mazingira ya dunia hii kwa kufuja mafuta kiasi hicho!kuna magari mengi sana ambayo yangeweza kumfaa kwa kazi zake,zile gari za wamisionari zinafaa sana kwa mazingira magumu,kwa kanisa lake la ki-dar es salaam hata RAV4 ingemtosha!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom