Askofu anamiliki HAMMER ya 250million! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu anamiliki HAMMER ya 250million!

Discussion in 'Celebrities Forum' started by GAMBLER, Jan 16, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2010
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Awali Risasi Jumamosi lilipenyezewa ‘tipu’ juu ya kuwepo kwa Askofu mmoja (jina tunalo), anayemiliki gari aina ya ‘Hammer’ inayokadiriwa kuwa na thamani ya ‘ngawira’ za kitanzania Milioni 250 na ‘ushee’ ambapo uchunguzi ulianza mara moja na kutengeneza kichwa cha habari hii.

  Katika ishu hiyo, baadhi ya waumini walilieleza gazeti hili kuwa, gari hilo analotumia Mtumishi huyo huku akivalia ‘krauni’ ya uaskofu, likitiwa mafuta ya shilingi elfu thelathini (30,000) haliwaki hivyo humlazimu kuweka ‘wese’ la shilingi laki tatu (300,000) ili kukamilisha mizunguko yake ya siku moja.

  Katika nusanusa ya makachero wetu ilibainika kwamba, mbali na baadhi ya watumishi hao kumiliki magari, majumba na vitu vya kifahari, lakini pia mavazi na mfumo wao wa maisha unawashangaza baadhi ya ‘kondoo’ wanaowaongoza.

  Ilisemekana pia kuwa, mmoja wa viongozi hao (naye jina tunalo), amekuwa akitinga madhabahuni na ‘pamba’ za mtoko mmoja zikiwa na thamani ya shilingi laki tano na nusu (550,000) huku akitoa ushuhuda kwa waumini wake kuwa, hayo ni matunda ya kumtumikia Mungu.

  [​IMG]

  Katika chimbua chimbua ya hapa na pale, mapaparazi wetu walitonywa pia kuwa, mmoja wa viongozi hao ambaye yeye hujitambulisha kuwa ni Nabii, akiwa katika harakati zozote barabarani hupewa ‘eskoti’ ya msururu wa magari na ving’ora kama ule wa rais wa nchi.

  Ernest Madewe, ambaye ni muumini wa moja ya makanisa ambayo kiongozi wake yuko kwenye listi hiyo, aliliambia Risasi Jumamosi kuwa, kondoo wa Mungu wamekuwa ‘wakikamuliwa’ fedha bila kujali umasikini unaowakabili.

  Alisema: “Kuna wakati tunajaza fomu maalum za kueleza mali tulizonazo ili kuhakikisha tunatoa fungu la kumi linaloendana na kile tulichonacho bila kujali kuwa kuna baadhi yetu tuko hoi na hatuna kitu.

  [​IMG]

  “Suala la sadaka linapaswa kuwa siri ya mtu na Mungu wake, lakini kinachoshangaza, jamaa wanakaba kupita kiasi.”

  Baadhi ya maaskofu, wachungaji, walimu na manabii wanaosifika kwa kutoa huduma ya kiroho vizuri ni pamoja na Onesmo Ndegi wa Kanisa la Living Water ‘kanisa la makuti’ lililopo Kawe na Mch. Getrude Lwakatare ‘Mama Lwakatare’ wa Kanisa la Assemblies of God la Mikocheni B, yote ya jijini Dar.

  Wengine ni Askofu Zakaria Kakobe wa Kanisa la Full Gospel lenye makao yake makuu pembeni mwa Barabara ya Sam Nujoma, Josephat Mwingira wa Kanisa la Ephata Ministry na Askofu Silvester Gamanywa wa Huduma ya Hakuna Lisilowezekana, nayo ya jijini Dar.

  Listi hiyo ndefu inaungwa na Mch. Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufalme na Ufufuo lililopo Ubungo, Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ wa Ubungo Kibangu na Nabii GeorDavie wa Kanisa la Ngurumo ya Upako lenye makao yake makuu mkoani Arusha.
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  wajinga ndio waliwao......wanaojiita wachungaji wote wezi na matapeli tu.
   
 3. edwinito

  edwinito JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 211
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Josephat gwajima!!!!!!!!!!!! Nyumba ya ufufuo ubungo!
   
 4. edwinito

  edwinito JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 211
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mkuu Magezi TARATIBU BABA!!
   
 5. D

  Darwin JF-Expert Member

  #5
  Jan 16, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Atheist tunasema raha ni hapa hapa duniani.
  Mnataka hizo raha akazilie wapi?
  Mtamuamini kwamba alimuona Yesu kama anatembea na kandamibili?

  Mimi ninavyoona nikwamba huyo askofu alifanya biashara nzuri ambayo nikuwa na mdomo mzuri nakuwatangazia waumini wake maneno mazuri na wakamuamini.
  Baada ya Kuamini ndio sasa Wanajua ukweli

  Kujua = Kitu ulichokua na uhakika nacho
  Kuamini = Kitu ambacho bado kina pande mbili.


  Uamuzi ni kwa waumini wenyewe
   
 6. D

  Darwin JF-Expert Member

  #6
  Jan 16, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Sijaona utapeli wowote hapo.
  Watu walitoa kwa hiari yao
   
 7. m

  matambo JF-Expert Member

  #7
  Jan 16, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  enyi vipofu viongozi wa vipofu mbona mwawatelekeza mbuzi wenu?
  enyi watu wa mshahara msio na huruma na mbuzi wenu?ha ha haa maana on the judgement day pindi hawa mbuzi watakapobaguliwa kuwekwa mkono wa kushoto ninyi ndo mtakaowaoongoza kuelekea jahanum
  hawa ndo watakao misamaha ya kodi ili waweze fanya masuala yao ya kipumbavu

  ooh mola tuongoze kwenye njia iliyonyooka,
   
 8. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #8
  Jan 16, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mnashangaa nini wakati nyinyi mliojaa hiana? mliitoa nchi hii kwa matapeli kuliwa kwa hiari yenu na hamjawahi kuuliza?

  Mbona hamjawashangaa watanzania kwa kuitoa nchi na raslimali zake kwa sisi m kwa ahadi ya maisha bora ambayo hayapo?

  Mbona pia hamjawahi kuwashangaa wanaoichangia kampuni ya bia mabilioni na mabilioni kwa kupewa reward ya ulevi? Kampuni hiyo ni tajiri kwa migongo ya watanzania hawa hawa. Acheni unafiki Bwana.

  Mimi sijali na Ningetamani amiliki hammer 5 hivi huyu mtu wa Mungu.
   
 9. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #9
  Jan 16, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  ndio tatizo lteu wabongo.watu wengi ni brainwash!haya makanisa yote yana prey to the weak.na hypocricy ya wachungaji huwezi kuamini.kama kweli mtu anamiliki Hammer tanzania,tena ni mtu wa kanisa ,hii ni ajabu.

  Bwana asifiwe
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Jan 16, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ajabu iko wapi wewe?

  Nenda uwaone waumini wa mtu huyu, ni watu wenye pesa zao na wanaheshimika mno katika jamii, si wale mazuzu ambao utasema labda wanadanganywa..Ni watu wenye uelewa kuliko wewe!

  Nani aliyewaambia kwa Mungu wetu kuna umasikini?

  Hakuna definition ya umasikini zaidi ya MENDE NA PANYA, mnataka watu wanaomtumikia Mungu aliye hai waishi na funza na Panya ndo muone wanaongea ukweli?

  Acheni fikra mbofumbofu bana, mi naona sawa, ili mradi hakuna malalamiko kanisani kwake,,who are we to judge?
   
 11. M

  Magezi JF-Expert Member

  #11
  Jan 16, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Najua ukweli unauma lakini angalia vijikanisa vilivyojaa mitaani kwetu. Tumeshuudia watu wanajiita wachungaji na wakati huo huo wanahusika na ujambazi wa kutumia silaha.

  Tumeshuudia wachungaji wanapora dhahabu za waamini wao (kakobe), tumeona wachungaji wakiwatoza yatima ada ya laki 7 ktk shule zao (rwakatare). Tumeona pia wachungaji wakipora wake za watu...nk.

  Hapa nashawishika kusema 40% ya vijikanisa vidogo vidogo na wachungaji wake ni matapeli.
   
 12. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #12
  Jan 16, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kwani askofu kuwa na HUMMER kuna tatizo gani
   
 13. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #13
  Jan 16, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kwa Mungu wetu hakuna umasikini na haya ni mambo ya imani. Lakini kuna kitu kinaitwa CONTEXT. Mtumishi wa Mungu kumiliki na kuendesha Hummer TZ ni bonge la alama ya swali. Labda tuiachie dhamira yake iamue. Na hao waumini wake malodi na wenye heshima kubwa katika jamii ya wa-TZ nao ni a big question mark. Halafu ukweli na wanyonge wanaoaminishwa na INJILI YA UTAJIRISHO nao ni wengi pia na hawawezi kulalamika wakiwa na ndoto hiyo "takatifu".
   
 14. M

  Mubii Senior Member

  #14
  Jan 16, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 149
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Jamani naomba Wakristo msiyumbe kiimani. Kutoa sadaka ni kutimiza maandiko yaliyo katika Biblia. Kama Watumishi wa Bwana wanazitumia vibaya basi Mwenyezi Mungu atashughulika nao. Mkristo endelea kutoa kwa ajili ya kazi ya Bwana na utabarikiwa sana.
   
 15. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #15
  Jan 16, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kama kanisa lina watu wenye pesa huoni kuwa kuchangia mafuriko na watu masikini ni bora zaidi mbele ya mungu kuliko kumchagia mchungaji aishi posh life ambayo hayatawasaidia kuuona ufalme wa mungu?

  Nafikiri umefika wakati hivi sasa kuwa na NGOs' regulator itakayotakiwa kufanya kazi chini ya NGO Act 2002. Inatakiwa NGO Act 2002 ifanyiwe ammendment ili kuanzisha Office of NGOs' regulator ambayo ni Professional body kama NBAA itakayokuwa na majukumu yafuatayo

  1. Kusajili NGO zote (sacramental and non-sacramental) baada ya NGOs hizo kuonesha kuwa zipo for Public benefits (pro bono)

  2. Kufuatilia utendaji wa NGOs zote kwa kuwataka kuwa wanafile annual returns zikiwa na maana ya mapato na matumizi yao ambazo ziwe open to the Public kama zinavyofanya Listed companies.

  3. Kuhakikisha kuwa NGOs hizi zina kitu kinaitwa Board of Trustees (Ambayo ni ya kujitolea, no remunerations zaidi ya expenses za kuendeshea shughuli za NGO tu) ambayo ndiyo responsible kwa mapato na matumizi ya NGO na pia iwe accountable to all stakeholders (waumini, interest groups, serikali n.k).

  4. Kuweka wazi kuwa matumizi ya ofisi(administrative costs) zisizidi 20% ya all collections/Income and the rest should go to the purpose of the NGOs

  5. Kupiga marufuku au kuipiga tax NGO yoyote ambayo haita kuwa imesajiriwa au kutekeleza masharti ya usajili.


  Kwa sasa kuachia mambo ya NGO kuwa serikalini katika ofisi ya makamu wa rais ni kuingiza siasa badala ya professionalism. Ukweli ni kwamba NGO zina nafasi kubwa sana ya kutoa huduma za kijamii. Ila watu kama hawa ambao hawapo accountable kwa mtu yoyote kwa sababu tu ni wachungaji, masheikh au wamiliki wa NGO kunaifanya sector nzima mabayo hivi sasa inaitwa "Third sector" baada ya Private sector na Public sector kuwa useless na chaka la wajanja wachache katika kujiendeshea Posh life kwa migongo ya Dini au Kusaidia yatima.
   
 16. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #16
  Jan 16, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Sina kinyongo na mtu kumiliki hammer au meli au ndege hata kama ni kwa gharama ya damu ya watanzania wasio na uwezo wa chakula chenye virutubisho vya damu inayowatoka. NAWAHAKIKISHIA MH MIZINGO PINDA ATAWATANGULIA WENGI WA WALE WANAOJIITA WATUMISHI WA MUNGU KUFUNGULIWA LANGO LA MBINGUNI. HUKU HAWA WATUMISHI WAKIZUILIWA SII TU KULIINGIA BALI HATA KULIKARIBIA.
   
 17. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #17
  Jan 16, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  I gotta be a bishop now, not a bad deal huh?
   
 18. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #18
  Jan 16, 2010
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 933
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  duh, kumbe huko nako kuna dili, ngoja nijipange nianzishe nami kakanisa kadogo!!!
   
 19. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #19
  Jan 16, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mnajua kitu inaitwa 'sudden death'?
  Iam afraid thats what you can face if you dont revisit your dreams!
   
 20. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #20
  Jan 16, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Hakuna gari inaitwa Hammer, lakini kuna gari inaitwa HUMMER.

  Na kuna HUMMER H2,H3, na H5.
  Bei za hizi haziko katika luxurious bracket, hizi ni trekta, gari za kazi.
  Hivyo si kweli kuwa gari hizo utazipata kwa Millioni 250 huo ni uongo!!
  Nimeweka CURRENT prices za gari hizo for your fair decision on the thread!!

  H3  THE MIDSIZE SUV.
  The HUMMER H3 is proof positive that good things can come in small packages. Even if you are a HUMMER. Of course, to belong to the HUMMER SUV family, you not only have to look the part, you also have to live up to the off-road 4x4 reputation that the family made famous. We're proud to say that the H3 does. Fully capable off-road. Totally comfortable on it. HUMMER 100,000-mile/5-year transferable Powertrain Limited Warranty.† OnStar‡ with 1-year Safe and Sound Plan. All standard. STARTING AT $34,135.
  [​IMG]

  H2 SUT  THE H2 SPORT UTILITY TRUCK. Half pickup, half SUV, the SUT’s bold looks, luxurious interior, and unparalleled off-road performance make it 100% HUMMER. With a host of standard features and a durable 72-inch bed, when the midgate is folded down, the SUT is as versatile as it is striking. STARTING AT $62,260*
  [​IMG]

  Haya magari heri ununue Landcruiser VX, na spea zake utapata.
  Hivyo basi aidha habari hii si kweli au huyo mtu wa Mungu katapeliwa!!!!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...