Askari walinda Amani wa JWTZ wauawa Darfur

Askari wetu kule ni peacekeepers na si peace enforcers. Peace keepers huwa wanakuwa hatarini zaidi kwani hawaruhusiwi kushambulia mpaka watakapoanzwa. Kutokana na hilo mara nyingi huwa wanakuwa victims wa ambush attacks. Hawa ni tofauti na walioenda Kongo kwani wa Kongo ni peace enforcers na wameruhusiwa kushambulia targets hata kama hawajachokozwa mradi objective yao itimie.
 
Tusubiri uthibitisho wa taarifa hizi maana mpaka sasa bado hazijathibitishwa!
 
Hyo ni tetesi hazjathbitika. Tukifanya hivyo kila mtu anazusha yake, basi ujue mantiki wa habari za kweli na uongo hautatofautshwa. Ifke mahal JF iwe ni chanzo cha uhakika wa habari za kweli na uhakika. Na tutafanikiwa kwa kuonyana sisi wenyewe. Au mnapenda ifke mahali habar kabla ya kupostiwa wawe wanazchuja? Tubadlke mkuu. Wengne ndg zetu wapo huko, mtaja tuua kwenye keypad za simu....araaaaagh*"
 
pole kwa taifa letu pamoja na familia za wafiwa kwa kupoteza wapendwa wao.
 
Ivi nini kifanyike kutokana na chuki hii ya raia kwa majeshi yetu? polisi na jeshi ni wakati wenu kutoa majibu au kutafakari mahusiano yenu na raia
 
Najionaga mtanzania zikipigwa wimbo wa taifa, tazama ramani,tanzania tanzania tuu, ila navyo ninaelekea kuniondolea uzalendo kwa sababu ya cloids wameuvamia na kuuchakachua sjui ntabaki na nini ka mtz vinipe uzalendo
 
Habari kutoka vyanzo mbalimbali vilivyoko Sudan vinadai kuwa kulfi kuwa na mapigano makubwa yameyosababisha Askari Saba wa JWTZ kupoteza maisha leo,taarifa zaidi nitawaletea ,nitakavyozithibisha,


kwa kutambuwa umuhimu wa Jeshi la Wananchi, nawapa pole makamanda walioko kwenye mstari wa mbele. japo jeshi letu linatumika kisiasa huku nyumbani, bado moyo wangu unakiri ukweli kuwa Jeshi ni roho ya nchi yoyote huru.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Nyenyere, NasDaz,

..MUNGU awalaze pema peponi askari wetu.

NB:

..msishangae sana comment za hawa wa-Tz wenzetu.

..ndipo CCM ilipoifikisha nchi yetu.

..mind u, hatujaongozwa na chama chochote kile zaidi ya CCM na mzazi wake Tanu.

..hivi mtoto uliyeishi na kumlea miaka yote. halafu akatokea kuwa na tabia zisizokupendeza, je utalaumu watu wa nje, au utajilaumu na kujisaili wewe kama mzazi??

cc: Mag3, Rufiji, Kasheshe, zumbemkuu
 
Last edited by a moderator:
duh hii kama kweli inatisha, RIP wanajeshi wetu, ingawa M23, malawi, rwanda wanatusubiri na wanasilaha nzito na cyo kama mikutano yetu ya CDM au mtwara ambao hatuna silaha.
 
Nyenyere, NasDaz,

..MUNGU awalaze pema peponi askari wetu.

NB:

..msishangae sana comment za hawa wa-Tz wenzetu.

..ndipo CCM ilipoifikisha nchi yetu.

..mind u, hatujaongozwa na chama chochote kile zaidi ya CCM na mzazi wake Tanu.

..hivi mtoto uliyeishi na kumlea miaka yote. halafu akatokea kuwa na tabia zisizokupendeza, je utalaumu watu wa nje, au utajilaumu na kujisaili wewe kama mzazi??

cc: Mag3, Rufiji, Kasheshe, zumbemkuu
R.I.P askari wetu. kuna wakati wa njaa wakulima hutumika, wakati wa vita askari ndo wakati wao, tunawaombea waende salama.
..hivi mtoto uliyeishi na kumlea miaka yote. halafu akatokea kuwa na tabia zisizokupendeza, je utalaumu watu wa nje, au utajilaumu na kujisaili wewe kama mzazi??
mkuu mzazi ndo anatakiwa ajilaumu na aangalie alipokosea wakati wa kumlea mwanae....
sema watoto wa siku hizi nao wamepinda kweli kweli, hiki ni kizazi cha nyoka.....
 
NasDaz wala huna sababu ya kuvuka mstari kiasi hicho. JWTZ nao wanatakiwa wakatae kutumiwa kisiasa. Kama unataka tuamini kuwa hakuna askari wa JWTZ aliyebaka mwanamke huko Mtwara basi ningetarajia Prof. Lipumba na Mbowe wafunguliwe mashitaka ya kulidhalilisha na kulichafulia jina JWTZ. Hatahivyo sikubaliani na mtazamo wako kuwa kila kinachosemwa na wanasiasa kinakuwa si cha ukweli.

Ukiondoka kwenye hiyo mentality ya kuona kuwa JWTZ ni untouchable ndipo utaweza kuwa mzalendo wa kweli kwa kutambua madhila wanayopata ndugu zako wa Ntwara kwa kutekwa na kuteswa na ushahidi wametoa sasa sijui unataka nini ili ujue kwamba JWTZ inajipaka matope yenyewe.

Hao wajeda tunakula nao maji ya ilala kila siku hadi chwee sasa sijui wewe unataka kumhadaa nani kuwa hawalali... JWTZ kama taasisi ulinzi ndio kazi yao ya msingi sasa wanapoanza kufanya mengine ndipo tunashangaa imekuwaje?
 
Hyo ni tetesi hazjathbitika. Tukifanya hivyo kila mtu anazusha yake, basi ujue mantiki wa habari za kweli na uongo hautatofautshwa. Ifke mahal JF iwe ni chanzo cha uhakika wa habari za kweli na uhakika. Na tutafanikiwa kwa kuonyana sisi wenyewe. Au mnapenda ifke mahali habar kabla ya kupostiwa wawe wanazchuja? Tubadlke mkuu. Wengne ndg zetu wapo huko, mtaja tuua kwenye keypad za simu....araaaaagh*"

Nmewasiliana na mmoja sasa hivi kaniambia ni kweli wapiganaji 7 wamepotea! na wengine majeruhi. R.I.P Fighters
 
Baada ya kusoma post nyingi nimegundua kuwa watu wengi wanachuki na majeshi yetu kana kwamba ni mamluki. Nadhani ni kwa sababu baadhi yao wanajiingiza kwenye siasa. Chuki ya namna hii ni ya hatari kwa mustakabli wa Taifa letu. Duh!

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mkuu NasDaz kama kweli viongozi wetu wanaitakia mema nchi hii basi wanatakiwa wachukue majukumu yao kikamilifu. Hizi comments ni dalili ya wazi kuwa kiwango cha uzalendo miongoni mwa watanzania kinazidi kuporomoka kila siku. Badala ya kuendesha siasa za ushindani wa hoja zenye kuzingatia maslahi ya nchi, viongozi wetu wa vyama vya siasa pamoja na serikali wamekuwa wakifanya bidii ya kupandikiza chuki, utengano na uzalendo kwa vyama vyetu vya siasa kadri kila mmoja anavyounga mkono.

Pia kitendo cha chama tawala kuvitumia vyombo vya dola katika masuala yasiyo na ulazima wa kuvitumia hasa kwenye mizozo ya isiasa ni hatari zaidi kwakuwa wananchi hawana imani na vyombo hivyo. Katika hali kama hii kama wananchi hawaviungi mkono basi ni dalili mbaya sana kwa usalama wa nchi yetu.
Mkuu Mwita Maranya,
Nakubaliana na wewe lakini hakika si busara hata kidogo kupeleka siasa zetu jeshini! Kwanza lazima tufahamu kwamba jeshi lolote duniani ni victim wa mfumo...wao siku zote ni watu wa kupewa amri na kutekeleza!!

Pili, si busara hata kidogo vitendo vya utovu wa nidhamu vinavyofanywa na mwanajeshi mmoja mmoja iwe ndo sababu ya kukashifu na kudharau jeshi lote! Hata kama sitetei, lakini huu utovu wa nidhamu haupo JWTZ tu, bali kwenye majeshi yote duniani hata yale kutoka nchi zinazojiona wao ndo kila kitu! Anaweza kutokea mpuuzi akasema wanajeshi wa hizo nchi wanafanya utovu wa nidhamu nje ya nchi lakini utovu wa nidhamu ni utovu wa nidhamu tu; uwe umefanyia mwezini au juani! Lakini kitu kibaya zaidi, sisi utovu wa nidhamu unaotufanya tuwahukumu askari wetu ni utovu wa nidhamu unaoripotiwa na wanasiasa kama akina Mwita Maranya! Lakini kwa bahati wanasiasa credibility yenu ya mdomo nayo ni ya kutia shaka!! Lakini potelea mbali, hata kama ni kweli, bado si busara hata kidogo kuhukumu jeshi zima kiasi cha mtu mtu kufurahia inapotokea wapiganaji wetu wameuawa! Hili halina justification hata kidogo vinginevyo itabidi tunukuu maneno ya Bwana Yesu yasemayo "anayejiona hana dhambi, basi na awe wa kwanza kurusha jiwe...!"

Kama nilivyopata kusema hapo awali, hiki kiburi tunachopata kuingia online hivi sasa na kuwashambulia wanajesh wetu kimeletwa na hao hao! Watu usiku tunakoroma, wala hatufahamu kwamba wanajeshi wanakesha mipakani kulinda usalam....hatufahamu hili; wakati sisi tunakoroma wengine wako Bar basi tunazani na wao ndo hivyo hivyo!
 
Last edited by a moderator:
Pumzikeni kwa amani makamanda na familia zote walipoteza waume zao na wake zao.mnapozama na sisi tunazama na mnopo panda na sisi tuna panda.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Hali hii inasikitisha. Niliwahi kucomment kwenye thread inayosema JK IWill Hit You. Nilisema kuwa hata kama lolote likitokea, mf. vita, kwa miaka ya leo serikali isitegemee ushirikiano kama ule wa enzi za Vita ya Kagera.
 
Nyenyere, NasDaz,

..MUNGU awalaze pema peponi askari wetu.

NB:

..msishangae sana comment za hawa wa-Tz wenzetu.

..ndipo CCM ilipoifikisha nchi yetu.

..mind u, hatujaongozwa na chama chochote kile zaidi ya CCM na mzazi wake Tanu.

..hivi mtoto uliyeishi na kumlea miaka yote. halafu akatokea kuwa na tabia zisizokupendeza, je utalaumu watu wa nje, au utajilaumu na kujisaili wewe kama mzazi??

cc: Mag3, Rufiji, Kasheshe, zumbemkuu
Mkuu wangu JokaKuu,
Mimi lazima zinashangaze tu....
Hapa ndipo ilipotufikisha CCM lakini sio TPDF! CCM ni CCM na TPDF ni CCM! Na kama ulivyosema, kama mtoto nimemlea mwenyewe na bado anaonesha tabia za ajabu za ajabu, ni mimi ndie natakiwa kujitazama upya!! Sino kosa la vijana wa JWTZ ambao wao wanapokea amri nenda huku, nenda kule nao ni lazima watekeleze! Uhuni wa mwanajeshi mmoja mmoja mmoja katu hauwezi kunifanya nidhihaki jeshi zima! Wacha watu waipasue CCM wapendavyo, na katu hutanikuta hata siku moja nakuja hapa kuitetea CCM labda nione jambo linalosemwa ni la uongo ulio dhahiri! Lakini linapokuja suala la kulidhihaki jeshi kwa sababu tu ya chuki zetu na CCM, hakika ni jamb lisilokubalika! Tena hii hali ya kuwananga kila wakati inaweza kuwafanya wajione katu hawawezi kuwa salama mikononi mwa upinzani....hili si jambo zuri hata kidogo kwa mustakabali wa upinzani!! Hii ndo pale unakuta mahali kiongozi amechaguliwa lakini amekaa ikulu siku mbili tatu, watu wanachukua nchi....ni kwavile wanajiona hawatakuwa salama na uongozi uliopo! Hii haimanishi kwamba jeshi wakifanya mafyongo watu wasiseme lakini sio kwa staili hii ya kuwaona kwamba nao na CCM ni wale wale tu kiasi cha watu kufurahia wanaposikia wameuawa!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom