Fakhi Jumaa
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 239
- 47
You are absolutely right!!!
Sasa sisi wananchi kwa akili zetu tujiulize, Je tunadhani hao wanajeshi wakipigwa wakaisha hao wavamizi watakuwa wanatugawia keki na juisi mitaani ee? Vita ni unyama jamani. Kwanza hawa watu yawezekana hata wao hawapewa tu amri kufanya yote hayo ila kwa kuwa kuna wakubwa wao wanawapa amri ya kwenda watakataa? Tukumbuke hawa ni kaka zetu, dada zetu, mama zetu na wengine wadogo zetu, Je kama wao wadogo wanapewa amri na mabosi wao (kama tunavyosikia jeshini ni amri moja) atawezaje kukataa au kugoma?. Hivi mtu unaandika eti "Safi sana kama wamekufa tena ilitakiwa wafe wengi" kwani? Kweli tunahitaji zaidi ya maombi ili tufungue macho,Jamani ee tukivamiwa hapa halafu jeshi likaisha raia ndo tunaobaki, sasa unadhani Mnyarwanda akija hapa atashindwa kuwabaka dada zangu asowajua? This is extremely pathetic. Unafurahia mtu kufa? It it?