Wale walikuwa CHADEMA wakiandamanaWatu wawili,akiwemo mwanafunzi wa Sekondari,wameuawa kwa kupigwa risasi kama wanyama Wilayani Rufiji mkoani Pwani. Watu hao wameuwawa na Askari wa Wanyamapori. Walidaiwa kuwa ni majangili katika Hifadhi ya Taifa ya Selou(?) kitu ambacho kimekanushwa vikali na wananchi wa sehemu hiyo. Kwa ubabe, wakazivua nguo maiti na kutuma nguo hizo nyumbani kwa marehemu.
Chanzo: ITV(Habari ya saa saba mchana)