ASKARI wa JK waua tena...

Watu wawili,akiwemo mwanafunzi wa Sekondari,wameuawa kwa kupigwa risasi kama wanyama Wilayani Rufiji mkoani Pwani. Watu hao wameuwawa na Askari wa Wanyamapori. Walidaiwa kuwa ni majangili katika Hifadhi ya Taifa ya Selou(?) kitu ambacho kimekanushwa vikali na wananchi wa sehemu hiyo. Kwa ubabe, wakazivua nguo maiti na kutuma nguo hizo nyumbani kwa marehemu.

Chanzo: ITV(Habari ya saa saba mchana)
Wale walikuwa CHADEMA wakiandamana
 
Kuna mbunge mmoja mwanamke, simkumbuki jina lake ila nampenda sana. Yeye akisimama bungeni wabunge wenzake wanaanza kucheka kwa kishindo, kuashiria kuwa wanajua kile anachotaka kuzungumza. Cha kwanza ni nanikuu "Mheshimiwa spika, kabla ya salamu naomba nianze na mjusi". wabunge wote vicheko. anaendelea "Mjusi wetu mhe. spika yuko kule Ujerumani. Na huyu mjusi ni muhimu sana, hivi ni lini hayo mabaki ya huyo mjusi yatarudi nyumbani"

Kilio chote cha huyu mheshimiwa kilitia fora pale aliposikia eti Twiga wetu tena wamesafirishwa kwenda huko ughaibuni tena wakiwa hai.

Nampenda sana huyu mbunge, ukimkumbuka nitumie jina lake.
 
Wanakinga ,acha waendelee tu, kwa kuwa wananchi bado hatujaona hii chinjachinja ya hawa 'governing tool' ya ccm ni tatizo
 
Inamaana katika nchi hii maisha ya wanyamapori yanathamani na yanalindwa kuliko maisha ya raia!
 
Wanakinga ,acha waendelee tu, kwa kuwa wananchi bado hatujaona hii chinjachinja ya hawa 'governing tool' ya ccm ni tatizo

Vyombo vya dola wameshajitangazia hali ya hatari, at their own level, lakini wakijua watawala wanaunga mkono maeneo hayo ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, katiba na sheria za nchi, vinginevyo mtu anawezaje kuendelea kufumbia macho na kuvumilia mauaji haya ya raia wasiokuwa na hatia
 
ccm haisamini tena maisha ya waTZ. Baada ya kuwapa waTZ umaskini wa kutupa na huduma hafifu sasa hata uhai wao hauthaminiwi.
 
Watu wawili,akiwemo mwanafunzi wa Sekondari,wameuawa kwa kupigwa risasi kama wanyama Wilayani Rufiji mkoani Pwani. Watu hao wameuwawa na Askari wa Wanyamapori. Walidaiwa kuwa ni majangili katika Hifadhi ya Taifa ya Selou(?) kitu ambacho kimekanushwa vikali na wananchi wa sehemu hiyo. Kwa ubabe, wakazivua nguo maiti na kutuma nguo hizo nyumbani kwa marehemu.

Chanzo: ITV(Habari ya saa saba mchana)

Kichwa cha Habari,"Askari wa JK"

Ukisoma habari,"Askari wa WANYAMAPORI"

hahahahahahahahahahahahaha
 
Shida ni kwamba tunapiga kelele weeeeeeee, "tunauwawa tunauwawa"..kama hatutafanya jambo lolote. TUKAE KIMYA KABISA, TUACHE KELELE ..sasa fikiria mwanafunzi wa Sekondari?!!!

Ujinga huu tunaofanyiwa, bado tunakaa tunasema hatuelewi kwanini wazazi wetu waliteswa na kunyanyaswa na mkoloni?Tena tunawabeza kusema, "wao walikuwa watu wa ajabu sana" ..UAJABU wao una tofauti gani na wetu?

Anyway, POLE kwa wafiwa.
Ninakuunga mkono hippocratessocrates!! lazima tufanye kitu wanyama wote wana tabia ya kujitetea. Hata wale wasio na sumu hutengeneza sumu wakifikishwa kwenye kona. Serikali hii imetufikisha kwenye kona!! lazima tujitetee!! tunakwisha hata kama ni juhudi na majambazi wa mabwepande kuhalalisha utawala wa kijeshi ili kulindwa liwalo na liwe!! hatuwezi kungoja tena!!
 
kwa wataka kusema Dr JK aliwapigia simu hao polisi na kuwapa maagizo wafanye hayo mauaji.? sijaona connection ya Dr JK na habari uliyeleta.....

kesho ukiibiwa utakuja na thread .. mwananchi wa JK kaniibia...

pathetic !
 
Nimeongea na askari mmoja wa ffu, kasema wanasiasa wanaharibu jeshi la polisi 2015 yeye anajifua mazoezi ya kukimbia tu! Anasema hali haitakuwa nzuri ccm itatumia nguvu ya jeshi, vyama vingine ni nguvu ya umma
 
Watu wawili,akiwemo mwanafunzi wa Sekondari,wameuawa kwa kupigwa risasi kama wanyama Wilayani Rufiji mkoani Pwani. Watu hao wameuwawa na Askari wa Wanyamapori. Walidaiwa kuwa ni majangili katika Hifadhi ya Taifa ya Selou(?) kitu ambacho kimekanushwa vikali na wananchi wa sehemu hiyo. Kwa ubabe, wakazivua nguo maiti na kutuma nguo hizo nyumbani kwa marehemu.

Chanzo: ITV(Habari ya saa saba mchana)
Lakini hao (red) hawaelezwi kitu kuhusu CCM. Watu wao wanauliwa lakini kesho itisha uchaguzi hata wa mwenyekiti wa kitongoji wao ni CCM tuu.
 
kwa wataka kusema Dr JK aliwapigia simu hao polisi na kuwapa maagizo wafanye hayo mauaji.? sijaona connection ya Dr JK na habari uliyeleta.....

kesho ukiibiwa utakuja na thread .. mwananchi wa JK kaniibia...

pathetic !

Hapo penye Dr.mnapapenda kwa nini usiseme tu kikwete au rais Kikwete.
 
Hii habari nimeipata kutoka kwa mtu aliyekuwa eneo la tukio.Aliyeuwawa ni mwanafunzi wa kidato cha pili anayesoma shule ya sekondari Mwaseni.Siku ya tukio alikwenda kuvua samaki katika bwawa ambalo lipo eneo la hifadhi.Mara wakasikia mlio wa risasi walivyokimbia kivyao huyu mwanafunzi alitokea katika kambi ya hawa askari poli na akajisalimisha ila KILCHOMKUTA NI KUKABIDHIWA KWA MKUU WA HAWA ASKARI AMBAYE ALITOA AMRI YA KUPIGWA RISASI AKISEMA HAWA MAJANGILI YATATUSUMBUA.
Pia mwanakijiji mmoja katika mlio wa kwanza wa risasi ilikuwa imeshampata moja na kufa papo hapo.

SOURCE: NDUGU YANGU WA KARIBU AMBAYE ANAFUNDISHA MWASENI SEC
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom