Askari Polisi kutumia silaha za moto za Automatiki (SMG, ASSAULT RIFLES) siyo sahihi, ni silaha za Kivita

Makamura

JF-Expert Member
May 19, 2022
356
550
Hizi bunduki za Automatiki zenye risasi nyingi kama 30+ ni silaha mahususi za Kivita sio za kulinda Raia au Kupigia Doria

Riffle.jpg

Ukiangalia Nchi za wenzetu Police wanatumia Hand Gun kama Pistol ndogo kama Bereta na Glock kwasababu hizi hazina Impact kubwa ukipigwa katika mwili. Ila hizi Mashine Gun ni ngumu kuishi baada ya kupigwa kwasababu ina Impact kubwa sana unapopigwa nayo. Tujikumbushe kwa yaliowahi tokea

Glock.jpg

Naomba Mamlaka Husika iangazie hili na kulipa uzito ili kuepusha athari za hapa na pale
 
The late mwangosi aliuawa kwa bunduki ya bomu la machozi tu.

Sijui unafahamu nini kuhusu silaha za kivita,ila hiyo silaha vitani inamhusu askari mmoja tu,ambaye matumizi yake hayatofautiani na haya ya askari wa polisi, labda siku ukiwaona na kifaru bank utahoji, hiyo ni silaha ndogo sana ya kivita. Lakini silaha bora sana kwa matumizi yasiyo ya kivita.ndio maana ili kuizatiti zaidi sheria ikakataa kabisa umiliki wa silaha yoyote auto kwa taasisi isiyo ya kulinda usalama na ya kiserikali.

Polisi hawawezi kuwa na vipistol peke yake ambavyo hata watu wenye hela ya kununua iphones wanavyo.
 
Wazo zuri.

Maana ni amani pale ambapo watu uwezo wa kudhuriana ni mdogo.

Hata kama ni amani zaidi pale hatudhuriani hata kidogo. Lakini tuwe wakweli tufanye kinachowezekana tupunguze uwezo wa kudhuriana

Majambazi wasimiliki auto machines, na mapolisi wasimiliki auto machines✌. Nnajitolea kuwa mwenyekiti wa hii nationwide disarmament ya majambazi na polisi 😂😂
 
Bahati nzuri au mbaya unaweza kuwa jambazi halafu ukaomba kuwa mwenyekiti wa amani pasipo silaha 😎
 
Hizo ni nchi za wenzetu na hizo ni tamaduni zao. Nasi kama taifa tunaonesha utofauti wetu, kuwa inawezekana askari polisi kutumia AK 47 na SMG na mambo yakawa Sawa tu.

Pia mfano lile tukio la Hamza imagine wawe saba, utaweza kuwatuliza kwa pistol?
 
SMG ni sawa kutumika mana hujui muda wala siku mwana wa jambazi atakapokuvamia, unaweza ukawa upo sehemu yenye amani kumbe hapo hapo jambazi nae anataka kufanya maajabu yake
 
Hizi bunduki za Automatiki zenye risasi nyingi kama 30+ ni silaha mahususi za Kivita sio za kulinda Raia au Kupigia Doria

Ukiangalia Nchi za wenzetu Police wanatumia Hand Gun kama Pistol ndogo kama Bereta na Glock kwasababu hizi hazina Impact kubwa ukipigwa katika mwili. Ila hizi Mashine Gun ni ngumu kuishi baada ya kupigwa kwasababu ina Impact kubwa sana unapopigwa nayo. Tujikumbushe kwa yaliowahi tokea

Naomba Mamlaka Husika iangazie hili na kulipa uzito ili kuepusha athari za hapa na pale
Ukiwa ni mtu ambaye hujawahi kukutana na majambazi wenye SMG na AK47 utatoa ushauri kama huu. Lakini ukikutana na changamoto kubwa ya kukabiliana na jambazi mwenye zana za kisasa na silaha za kivita naamini utatoa ushauri wa kutumia silaha Kali zaidi ya hizi wanazotumia askari polisi za Sasa. Cha msingi ni kuangalia katika kupunguza pengo la maskini na tajiri ndipo watu kujitoa mhanga wa kununua silaha za kivita na kutoka nchi zenye makundi ya waasi na kuja kuzitumia kutafuta fedha kwa nguvu na kutumia silaha! Endelea kuomba mungu siku Moja usishuhudie tukio Hilo na wewe uwe ni miongoni mwa watu waliokuwa wanalengwa kuibiwa na hao wenye silaha maana utaomba kwa lugha zote, dini zote na utakumbuka yote mabaya na mazuri ulofanya, familia yako,mkeo,watoto,mali zako, na mengi ulofanya mpaka wa huo tukio hilo linakutokea maana hutaamini kama watafanikiwa kuwaua wote ili wewe na wenzako mpone maana umetoka kutafuta kihalali na wenzako wanatumia njia ya mkato!!
 
watu wanashindwa kuelewa wanadhani matukio ni kusubiri au kujaribu. Polisi wapo kwa ajili ya kulinda raia na mali zao sasa sioni kwa nini watu wanakuwa na wasiwasi wa silaha wanazutumia kulindia. Unadhani adui aje na silaha kubwa atasubiri polisi na pisto yake au aende badili silaha? Polisi wapo na silaha hizo ili kuwa muda wote tayari kwa mapambano.Ni wajibu wa polisi kuhakikisha ulinzi unakuwepo muda wote hivo kuwa na silaha kubwa ni sawa kabisa. Na hii siyo Tanzania tu kama mdau alivyosema hata nchi za wenzetu wanatumia silaha kubwa pia sema tunatofautiana kulingana na wenzetu wanatengeneza wenyewe sisi tunaagiza nje.Uzuri wa SMG au AK47 inauwezo wa kupiga risasi moja moja au zaid ya moja kwa sekunde. Hii inamsaidia askari kumshambulia adui kulingana na atakavyoona inafaa na pia inauwezo wa kupiga mbali na pia kutumia risasi nyingi bila kupata madhara ya joto kwenye chemba. Pisto ni silaha ambayo inahitaji ukaribu na adui na kumvizia hasa kwa kumdhuru au kuua inapotegemea. umbali hauzidi mita 200. Short Gun shida yake ni ngumu kumlenga mtu mmoja hasa anapokuwa kwenye umati wa watu sababu risasi yake inasambaa inapotoka kwenye chemba zidi ya mita 5 inakawaida ya kusambaa. smg au ak47 unaweza mlenga adui bila dhuru waliopo pembeni kwa kutumia mtoko wa risasi moja moja.
1.jpg
2.jpg
3.jpg
4.jpg
5.jpg
5.jpg
7.jpg
8.jpg
9.jpg
10.jpg
9.jpg
 
Attachments

  • 6.jpg
    6.jpg
    12.4 KB · Views: 1
Ukiwa ni mtu ambaye hujawahi kukutana na majambazi wenye SMG na AK47 utatoa ushauri kama huu. Lakini ukikutana na changamoto kubwa ya kukabiliana na jambazi mwenye zana za kisasa na silaha za kivita naamini utatoa ushauri wa kutumia silaha Kali zaidi ya hizi wanazotumia askari polisi za Sasa. Cha msingi ni kuangalia katika kupunguza pengo la maskini na tajiri ndipo watu kujitoa mhanga wa kununua silaha za kivita na kutoka nchi zenye makundi ya waasi na kuja kuzitumia kutafuta fedha kwa nguvu na kutumia silaha! Endelea kuomba mungu siku Moja usishuhudie tukio Hilo na wewe uwe ni miongoni mwa watu waliokuwa wanalengwa kuibiwa na hao wenye silaha maana utaomba kwa lugha zote, dini zote na utakumbuka yote mabaya na mazuri ulofanya, familia yako,mkeo,watoto,mali zako, na mengi ulofanya mpaka wa huo tukio hilo linakutokea maana hutaamini kama watafanikiwa kuwaua wote ili wewe na wenzako mpone maana umetoka kutafuta kihalali na wenzako wanatumia njia ya mkato!!
Point hapa nikupunguza gepu kati ya tajiri na maskini, nchi yeyote yenye uhalifu mwingi ukifatilia utakuta matajiri ni wengi na maskini ni wengi vilivile

Napia nchi yenye uhalifu mdogo utakuta watu wa kipato cha kati ni wengi kuliko matajiri na maskini. Kama maskini ni wachache utakuta uhalifu ni mdogo maana hata matajiri wanahesabika.
 
Back
Top Bottom