Asilimia 40 ya bidhaa nchini ni feki

Asilimia 40 ya bidhaa nchini ni feki

Acha magufuli afanye kazi yake, angalau anaona kauchungu kidogo kwa wa TZ. Tukiongelea nyumba ni theluji ndogo mnooo ukilinganisha na ulafi mkubwa wa wakubwa wengine kila kukicha ni dhuluma kwa wananchi na kukazana kujenga mahekalu.

Kaza BUTI baba Magufuli
 
..mimi ningemshukuru sana Magufuli kama angejutia makosa yake kwa kuuza zile nyumba za serikali.

..halafu ningemuona shujaa kama angeamua kurejesha serikalini nyumba aliyojitwalia ktk zoezi lile.

..waandishi wa habari mkikutana na Magufuli muulizeni kwanini harejeshi nyumba yetu aliyojitwalia?

JokaKuu,
Sometimes I fail to understand you!

Kabla ya kumuuliza Magufuli kuhusu haya uliyoyaorodhesha inabidi tukutume umuulize Mkapa kwa nini aliidhinisha nyumba za serikali ziuzwe?! Kumshutumu Magufuli kwa kosa la Mkapa ni kumuonea tu.

Comments zako ni sawasawa na kusema kwamba kiongozi yeyote hapaswi kufanya kazi yake ama kufanya lolote litakalosifiwa na wananchi kwa sababu tu wanakalia nyumba walizouziwa/kupewa na Serikali! It is not fair at all.
 
ona huyu nae!!!!

uwezo wako wa kufikiri ukoje wewe?

anayo ph.D unataka nini sasa baada ya kujua hilo?

Hiyo Ph.D kaipata lini na wapi? Katika nchi ambayo pamejitokeza mlolongo wa Ph.D feki inabidi kuulizia ameipataje. Au kwa vile hapa kaguswa mumpendae? Kama ni ya halali anastahili pongezi lakini kama ndiyo hizo za vyuo visivyoeleweka, basi integrity yake inatia shaka.

Amandla......
 
Fundi Mchundo!
Let us agree to disagree as usual. You seem to become matured now.
Kama Pombe Magufuli is not creeping cheap politics anatakiwa atumie team work na members wa Baraza la Mawaziri kwani maswala haya yana dimension pana. To be realistic kuna haja ya kuangalia upya sera tuliyokumbatia ya soko huria kichwa kichwa kuanzia enzi za Ruksa kupitia kwa jambazi Mkapa na leo tunaye fisadi Kikwete.
Hivi kwa nini tusirudie zile enzi za kutumia import licence na mipesa kupitishiwa Benki badala ya huu utamaduni wa kubeba cash kufanya transaction zetu. If we go back into the old good days unaomba leseni ya kuagiza vibua inabidi ipitishwe kwenye Wizara ya Vibua of course hutapewa leseni and therefore hapa hutamlaumu TRA wa TFDA wala TBS kwani hapa hakingii hata kiberiti au pipi but because mmekuwa vipofu vibua wapo kwenye ghala Vingunguti halafu Pombe anamnukulia Mama anayeagiza nyavu sheria ambayo she is not even interested kusikiliza. Kwa hapo we need to go back kwenye REGULATATED ECONOMY/MARKETS kwa taarifa yenu those wise people like OBAMA wameshaanza kwani wewe Jakaya na Pombe wako why are you so shy au mmekula yamini na wahindi!!!!

Asante kwa kutambua kuwa Fundi Mchundo sasa is no longer immature. Si kitu kidogo hicho. Bahati mbaya sikumbuki wapi mimi na wewe tume-agree ku-disagree!

BTW, nadhani hawasemi "you seem to have become matured now" isipokuwa "you seem to have matured now" au "you seem to have become mature now". Ni hayo,tu.

Amandla.......
 
Hata kama yalipitishwa na baraza la mawaziri lakini bado yalikuwa ni maamuzi haramu. Kama kweli Magufuli ni kiongozi mwenye maadili bora kama anavyopigiwa debe na watu mbali mbali hapa jukwaani anaweza kuwa mstari wa mbele na kutamka kwamba hayaungi mkono maamuzi ya kuziuza nyumba za Serikali kwa bei poa yaliyofanywa katika awamu ya tatu, hivyo nyumba yake aliyoichukua anaamua kuirudisha Serikalini, kinyume na hayo naye ni miongoni mwa wasio na maadili bora na hafai kama kiongozi wa nchi yetu.
hilo la kuuza nyumba lilikuwa sera ya ccm. Na hoja hapa Nafikiri ni magufuli kukemea watanzania kulishwa chambo.La pili ni kuhoji hicho kiwanda kinachotengeneza kokoro yenye matundu madogo.watanzania kufurahishwa na hatua hizo kuna kosa? Mbona ni kama unamkandamiza mtoa hoja na wanao support wasitumie uhuru wao ku express what they feel is right?That is dirty game
 
Dr. Magufuli ni moja ya viongozi mahiri na shupavu sana, ila wanaompinga hawana sera pengine ni wale wale wasiopenda uongozi makini
swala la nyumba za serikali ni siasa tu na si magufuli kwanza mjadala haupo tena
Nani asiyejua kuwa wanamubania kwa kumpa wizara zisofahamika na badala yake anawaamsha watanzania
angalia walipompeleka wizara ya ardhi walishika adabu na watanzania tungepata maendeleo haraka kwa hati watu wangepata na kupata mikopo kama mitaji leo hii nenda huko ni ovyo , nani alijua hujuma kwenye samaki

Muacheni magufuli wetu achape kazi , mlie tu wenye wivu

Chapa kazi doctor wa ukweli
 
Code:
..mimi ningemshukuru sana Magufuli kama angejutia makosa yake kwa kuuza zile nyumba za serikali.

..halafu ningemuona shujaa kama angeamua kurejesha serikalini nyumba aliyojitwalia ktk zoezi lile.

..waandishi wa habari mkikutana na Magufuli muulizeni kwanini harejeshi nyumba yetu aliyojitwalia?
Code:

OUT OF TOPIC!
icon9.gif
 
hilo la kuuza nyumba lilikuwa sera ya ccm. Na hoja hapa Nafikiri ni magufuli kukemea watanzania kulishwa chambo.La pili ni kuhoji hicho kiwanda kinachotengeneza kokoro yenye matundu madogo.watanzania kufurahishwa na hatua hizo kuna kosa? Mbona ni kama unamkandamiza mtoa hoja na wanao support wasitumie uhuru wao ku express what they feel is right?That is dirty game

Kwani CCM ni Mungu! hakuna mtu yeyote anayeweza kusimama na kuyapinga maamuzi yanayofanywa na CCM au Baraza la Mawaziri? Magufuli angeweza kabisa kuyapinga maamuzi hayo kwa sababu hayakuwa na maslahi yoyote kwa nchi. Kukaa kwake kimya kunaonyesha kwamba aliweka mbele maslahi ya kunufaika kwake kuliko yale ya nchi na hivyo ni mmoja wa mafisadi ambao wameweka mbele maslahi yao kuliko yale ya nchi. Kikwete mlisema hivyo hivyo kwamba ni Kiongozi bora, mkombozi wa Watanzania na pia mkathubutu kumuita eti ni chaguo la Mungu! Sasa tunapiga kelele kwa madudu anayoyafanya karibu kila siku iendayo kwa Mungu.
Always remember that past performance is a good indication of future performance. Magufuli si kiongozi bora na kuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha hilo.
 
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limekamata shehena ya taulo za wanawake bandia maarufu kama Always zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 200.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Basilo Matei, alisema jana kuwa shehena hiyo ilikamatwa juzi nyumbani kwa mfanyabiashara maarufu mjini hapa katika eneo la Baraa, jina tunahifadhi kwa sababu hatufanikiwa kuzungumza naye.

Matei alisema shehena hiyo ina maboksi zaidi ya 10,000 na zinadhaniwa kuingizwa nchini kutoka China na kusambazwa katika maeneo ya biashara kinyemela.

Aidha, Matei alieleza kuwa polisi walifanikiwa kukamata Always hizo bandia baada ya kupata taarifa kutoka kwa kampuni Procter & Gambo Ltd ya jijini Dar es Salaam ambayo ni wakala aliyeruhusiwa kuingiza bidhaa hizo nchini.

Alisema kampuni hiyo iligundua bidhaa hizo feki kujaa sokoni.

“Tulipata taarifa na tukaifanyia kazi na baadaye tukaweza kukamata shehena ya bidhaa hizo zikiwa zimehifadhiwa katika gahala nyumbani kwa mtuhumiwa,” alisema Matei

Kamanda Matei alieleza kuwa pamoja na kukamatwa kwa Always hizo mfanyabiashara huyo hakupatikana nyumbani kwake na ilielezwa kuwa yupo safarini nje ya nchi.

Nipashe ilitafuta wataalamu wa mambo ya afya ambao walibainisha bidhaa feki za aina hiyo kusababisha maambukizi ya magonjwa ya zinaa pamoja na fangasi ambao ni hatari kwa afya ya uzazi.

Daktari Baraka Mkongo alitaja magonjwa hayo kuwa ni (UTI) ambayo wadudu hushambulia mfumo wa mkojo hatimaye kwenye viungo vya ndani vya uzazi.

Mkongo alieleza kuwa athari za maambukizo hayo ni mbaya kwani huweza kuambukiza haraka na hata wakati mwingine huleta mitafaruku ndani ya familia kwani humbukiza haraka wakati wa kufanya tendo la ndoa.

“Wakati mwingine ndoa zinaweza kuvunjika kwani mathalani mke akiambukizwa halafu amwambukize mume atamtuhumu mke wake kutembea nje ya ndoa au wakati mwingine wote wawili hutuhumiana na kuleta balaa katika ndoa,” alisema Dk. Mkongo.

Kumekuwa na wimbi la kuingizwa nchini kwa bidhaa feki kutoka China, nyingi zikiletwa na wafanyabiashara wenye tamaa ya kupata faida ya haraka haraka.

Miongoni mwa bidhaa hizo zikiwa na thamani ya mabilioni zimekuwa zikiteketezwa nchini baada ya kumatwa nchini kufuatia operesheni zinazoendeshwa na Mamlaka za Chakula na Dawa (TDFA), Shirika la Viwango nchini (TBS) wakishirikiana Tume ya Ushindani wa Kibiashara (TFCC).
 
Mmmh jamani!!!!!!tutapona kweli?yani mm niliwahi kupata uti,nikawa naogopa toilet za job,yani nikiingia naanza na usafi kwanza zen shida zangu but watu wengi job wanalalamika uti(ladies)kumbe ni chines product?eeeeeeeeeeeeh mungu
jeshi la polisi mkoani arusha limekamata shehena ya taulo za wanawake bandia maarufu kama always zenye thamani ya zaidi ya sh. Milioni 200.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, basilo matei, alisema jana kuwa shehena hiyo ilikamatwa juzi nyumbani kwa mfanyabiashara maarufu mjini hapa katika eneo la baraa, jina tunahifadhi kwa sababu hatufanikiwa kuzungumza naye.

Matei alisema shehena hiyo ina maboksi zaidi ya 10,000 na zinadhaniwa kuingizwa nchini kutoka china na kusambazwa katika maeneo ya biashara kinyemela.

Aidha, matei alieleza kuwa polisi walifanikiwa kukamata always hizo bandia baada ya kupata taarifa kutoka kwa kampuni procter & gambo ltd ya jijini dar es salaam ambayo ni wakala aliyeruhusiwa kuingiza bidhaa hizo nchini.

Alisema kampuni hiyo iligundua bidhaa hizo feki kujaa sokoni.

“tulipata taarifa na tukaifanyia kazi na baadaye tukaweza kukamata shehena ya bidhaa hizo zikiwa zimehifadhiwa katika gahala nyumbani kwa mtuhumiwa,” alisema matei

kamanda matei alieleza kuwa pamoja na kukamatwa kwa always hizo mfanyabiashara huyo hakupatikana nyumbani kwake na ilielezwa kuwa yupo safarini nje ya nchi.

Nipashe ilitafuta wataalamu wa mambo ya afya ambao walibainisha bidhaa feki za aina hiyo kusababisha maambukizi ya magonjwa ya zinaa pamoja na fangasi ambao ni hatari kwa afya ya uzazi.

Daktari baraka mkongo alitaja magonjwa hayo kuwa ni (uti) ambayo wadudu hushambulia mfumo wa mkojo hatimaye kwenye viungo vya ndani vya uzazi.

Mkongo alieleza kuwa athari za maambukizo hayo ni mbaya kwani huweza kuambukiza haraka na hata wakati mwingine huleta mitafaruku ndani ya familia kwani humbukiza haraka wakati wa kufanya tendo la ndoa.

“wakati mwingine ndoa zinaweza kuvunjika kwani mathalani mke akiambukizwa halafu amwambukize mume atamtuhumu mke wake kutembea nje ya ndoa au wakati mwingine wote wawili hutuhumiana na kuleta balaa katika ndoa,” alisema dk. Mkongo.

Kumekuwa na wimbi la kuingizwa nchini kwa bidhaa feki kutoka china, nyingi zikiletwa na wafanyabiashara wenye tamaa ya kupata faida ya haraka haraka.

Miongoni mwa bidhaa hizo zikiwa na thamani ya mabilioni zimekuwa zikiteketezwa nchini baada ya kumatwa nchini kufuatia operesheni zinazoendeshwa na mamlaka za chakula na dawa (tdfa), shirika la viwango nchini (tbs) wakishirikiana tume ya ushindani wa kibiashara (tfcc).
 
Wana ndugu hii imenishtua sana sana nasema imentishha
labda kwa wanaweza kufwatlia kuna wachina pale tabatawako
mwisho karibu na shell ya oilcom wao wanajitangaza wanachimba
visima;mzee wangu mmmoja marehemu mungu amalaze pema peponi alienda kulippa nikawa shahidi;nilipofika wamechukua jumba kubwa limejaa
always tupu za rangi ya dhambarau;watananzia kama 8 3 kila chumba wanazifunga;atakaeitaji kuwafwatiliia ani pm
nikamuuliza zimetoka wapi akadai china
loh eee mola tusaidie awa watu wanaribu uchi wa wake zetuwalaaniwe maisha;zingine nasikia unawashwa mpaka unashaa alafu ukisex na mumeo
fasta nae anaagiza mti wa kujikuna
jamani serikali mtakuwa lini makini?
 
Mmmh jamani!!!!!!tutapona kweli?yani mm niliwahi kupata uti,nikawa naogopa toilet za job,yani nikiingia naanza na usafi kwanza zen shida zangu but watu wengi job wanalalamika uti(ladies)kumbe ni chines product?eeeeeeeeeeeeh mungu

hizo fake mbona zimetoka kitambo tu, zina harufu kali cjui mi perfume....khaaa! uwe unatumia stay free mami....na pole kwa UTI.
 
Wana ndugu hii imenishtua sana sana nasema imentishha
labda kwa wanaweza kufwatlia kuna wachina pale tabatawako
mwisho karibu na shell ya oilcom wao wanajitangaza wanachimba
visima;mzee wangu mmmoja marehemu mungu amalaze pema peponi alienda kulippa nikawa shahidi;nilipofika wamechukua jumba kubwa limejaa
always tupu za rangi ya dhambarau;watananzia kama 8 3 kila chumba wanazifunga;atakaeitaji kuwafwatiliia ani pm
nikamuuliza zimetoka wapi akadai china
loh eee mola tusaidie awa watu wanaribu uchi wa wake zetuwalaaniwe maisha;zingine nasikia unawashwa mpaka unashaa alafu ukisex na mumeo
fasta nae anaagiza mti wa kujikuna
jamani serikali mtakuwa lini makini?

wengi zimewaletea fungus.
 
mwanahalisi ikiwa unamapenzi mema na wake zetu wataarifu TFDA au TBS nitakuona wa maana sana. Vinginevyo unaleta uzushi.
 
hivi kwa nini dada zetu ss mnunue za kichina? tumieni zingine kama vipi.
 
tunasubiri watoto ''wa-kichina'' sasa!......
 
Baaaaaaaaaaasi tumeumia kama ndo hivi ...

hizo mbona ni ovyo cku nyingi tu, cover yake ya juu sio soft so inachubua sana, wakayafanya mapana mno, yaani hayana quality kabisa, walivyoweka na ile cjui perfume, mweh unashangaa mtu utawekaje huko chini li harufu likali vile...
 
Back
Top Bottom