Asilimia 40 ya bidhaa nchini ni feki

Asilimia 40 ya bidhaa nchini ni feki

Original vitu quality mnaweza/mnamudu kununua nyieee

Ova
 
Na bei zake ni fake au orginal ?

Sometimes you get what you buy....
 
Je tutafika? Leo nimesikia kwenye vyombo vya habari kuwa asilimia arobaini ya bidhaa zinazouzwa hapa nchini ni feki, zisikuwa sahihi kwa matumizi ya binadamu. Hii hali imenishtua sana. Kwani ni vigumu watu au watanzania tulio wengi kugundua au kujua kitu ambacho ni FAKE au GENUINE. Zinahitajika juhudi za ziada kuwaokoa wa-Tanzania. Kinyume na hapo tutalipoteza taifa hili.

Cha kujiuliza, hizo bidhaa feki hadi kufikia asilimia arobaini zinaingiaje nchini? TRA wananfanya nini? TBS wanafanya nini? Wafanyakazi mipakani, viwanja vya ndege na bandarini wanafanya kazi gani? Hayo ni maswali ambayo sina majibu la haraka. Je nini kifanyike. Nchi inanuka rushwa. Maisha ya wananchi yapo hatarini.

Kwani TBS bado ipo na ina wafanyakazi wanaopokea mishahara na marupurupu pia?
 
Walikua wanasumbua vitu kutoka mbali kuingia Tanzania wafanyabiashara wengine ambao sio waaminifu wametoka na kitu Original wanapeleka nchi moja jirani ina viwanda vingi wanafyatua vitu feki na vinaingia tuu na kuuzwa kwa bei ya OG baadhi ya bidhaa kupata kibali TBS kwa miezi kadhaa ni kama unalipa kodi sijui wanafikiria nini wakati kutofautisha vitu bado hawajajua...
 
Nimejaribu sana kulinganisha hizi kondoms za roughrider, si kama zilizokuwepo miaka ya nyuma. Hizi za siku hizi kwanza kuzifungua toka kwenye kimfuko chake ni hadi utumie meno au kijiwembe, hazifunguki kirahisi. Pili zinaonekana kama zimebana na kwa kweli hazihimili vishindo kama zile za miaka takriban mitano iliyopita. Hapa nabaki najiuliza kulikoni, wajanja wameamua kujitajirisha kwa kufanya ufisadi wa kutengeneza kondoms feki kwa gharama ya maisha ya watanzania.

Kitu kingine nilicho na wasiwasi nacho ni haya maziwa ya Nido yaliyo na label ya Africa Kusini. Haya nayo siamini kama ni maziwa yanayostahili kutumiwa na watanzania wa leo. Ni kwamba ukiyatia kwenye maji ya moto yanatengeneza vijibonge vidogovidogo, hayayeyuki vizuri. Hata ladha yake inatia shaka. Hapa napo naona wahuni wa kibiashara wameshaingilia soko wanatutengenezea bidhaa feki. TBS mko wapi? Nyie ndiyo tegemeo la afya na maisha yetu pambaneni na hawa wahuni wasiojali maisha ya watu.
Ataa spaghetti tambi ni feki ,sabuni imperial ,detol soap na liquid feki ,dawa malafin,duo-cortexin ya malaria ziko chini ya viwango ni feki tuu ,
 
Hii nchi ni ngumu hata papuchi nyingi zaidi ya 90% ni feki tena feki haswa.!
 
Back
Top Bottom