Asanteni sana Uongozi wa Simba SC na Bodi ya Simba SC kutusikiliza 'Wadau' na kuamua kuwa Mchezaji Ousmane Sakho 'hatotemwa' Kikosini

Nimeshangaa mno kuna mtu anasema Lyanga wa Azam anazidiwa na sakho nimeshtuka mno mbona mpira mchezo wa wazi Sana mbona watu wanajitia upofu

Sakho hata kwa Christian zigah wa Biashara united hafiki

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Hawa jamaa hawajui mpila au wanafaidika na 10 % ya mishahara kwa hao wachezaji maana sio kwa utetezi huu wa kishamba
 
Sackho hamna kitu kabisa.
Nashangaa wanavyomsisitiza, mi nimeangalia mechi zote alizocheza na sijaona chochohe. Kwa Peter Banda nimeona kitu flani kizuri kinachoweza kuangaliwa kwakuwa bado mdogo.
Mchezaji wa ukweli hapepewi hata kidogo akiingia uwanjani anakiwasha tu
Sackho si wa kucheza Simba.
Skauti ya Simba haiko vizuri kabisa.
Msimu huu Yanga wametuzidi sana kwa swala la usajiri.
Sawa, ila sidhani kama ni falsafa nzuri kushindana kwenye usajili, matokeo yake ni kuchoma pesa nyingi kwenye zoezi hili bila mafanikio yoyote! Kila timu iende na falsafa yake katika hili na kwa malengo yake, PERIOD!
 
Naomba GENTAMYCINE nianze Kwanza kwa kutoa Pongezi kwa wana Simba SC Wenzangu wote ( hasa tuliopo hapa JamiiForums ) ambao tokea Juzi nilipoanzisha Uzi wa Kuzuia Mshambuliaji Ousmane Papi Sakho ( Raia wa Senegal ) Kuachwa ( Kutemwa ) Kikosini Simba SC kwa pamoja tulipaza Sauti zetu za Kuzuia hilo.

Pia tuupongeze sana huu Mtandao Wetu pendwa wa JamiiForums kwani ni Mtandao ambao una Sauti Kubwa na Ushawishi wa Kimaamuzi hasa ikiaminika kuwa Members wa hapa ni Great Thinkers hasa na wakisema au wakishauri Jambo basi jua kwa 85% huwa ni sahihi na pia lina Mantiki ( Logic ) ndani yake.

Kwa taarifa ambazo nimezipata kutoka kwa Waandamizi Watatu ndani ya Bodi ya Simba SC ni kwamba wamesikiliza Kilio cha wana Simba SC wote ( tunaojua Mpira na wenye Jicho pana la Mchezo wa Soka ) na kuamua kuwa Mshambuliaji na Winga Ousmane Papi Sakho ( ambaye GENTAMYCINE namkubali sana kama ninavyomkubali mno Kiungo Jonas Gerald Mkude ) hatoachwa ( hatotemwa ) kama ilivyokuwa imesemwa au imeenezwa hapo awali.

Hata hivyo wana Simba SC Wenzangu tusichoke Kupaza Sauti zetu kuhusu Mchezaji Sakho kutokuachwa Kikosini kwani Bodi ya Simba SC ina Wajumbe wengi ila mpaka sasa Wajumbe Waandamizi Watatu ( wenye Ushawishi mkubwa kwa Wanachama, Wapenzi na Mashabiki ) wamekataa Sakho Kuachwa ( Kutemwa ) na kutaka avumiliwe kwakuwa alipatwa na Majeruhi na apewe muda zaidi kwani ni Hazina Kubwa kwa aina ya Kipaji cha hali ya Juu alichonacho.

Mwisho nawaomba wale ambao tokea Juzi katika ule Uzi wangu wa Kukataa ( Kupinga ) Sakho asiachwe Simba SC mlikuja Kutudhihaki, Kutusanifu na wengine hata Kututukana tafadhali msiache kufanya bali endeleeni kwani huwa mnatupa Chachu ya Kuimarisha zaidi Fikra zetu pana huku nyie mkiendelea tu kubakia na Uzuzu ( Ujuha ) wenu mliobarikiwa na mtakaokufa nao.

Mshauri Mkuu wa Mwekezaji Mo Dewji na Mshauri Mwandamizi wa Bodi ya Simba SC 'Poti' wangu Crescentius Magori endelea Kutufikishia haya Mawazo yetu huko kwa Wakubwa na Asante kwa kuwa Mmoja wa 'Followers' wangu hapa JamiiForums hivyo naamini nikiwa naandika mambo 'Serious' hapa kuihusu Simba SC yetu huwa unayasoma na Kuyafikisha haraka Uongozini.

Muacheni Duncan Nyoni, Peter Banda, Pascal Wawa na Chris Mugalu, ila Thadeo Lwanga, Saido Kanoute na Ousmane Sakho msiwaache lakini mpeni ONYO KALI na la Mwisho Bernard Morrison kuwa wana Simba SC hatutaki na tena tumechoka na 'Mbwembwe' zake za ndani na nje ya Uwanja bali tunataka acheze Mpira, awe na Ufanisi, asiwe Mbinafsi na asipende Kucheza na Jukwaa bali tunataka KAZI KAZI Kikosini na siyo Upuuzi na Utoto wake.

Na binafsi nisifiche au kuwa MNAFIKI kuwa SIMKUBALI na NIMESHAMCHOKA kwani Bernard Morrison anatumia Nguvu Kubwa kuutaka 'Ufalme' ambao bado hana ndani ya Kikosi cha Simba SC na hataki Kujifunza ni kwanini Emanuel Okwi au Clatous Chama waliupata na walifanya nini ndani ya Simba SC wakawa 'Wafalme' ambao leo kila mwana Simba SC anawakumbuka na tunafurahi Kubahatika kuwa nao.
Yaani Mugalu aachwe?🙄
 
Simbaa wapunguze kulogana?miongoni wa Wachezaji,Tena Mchezaji ukiwa mgeni halafu unafanya vema ni kulogwa ukose namba Hizi ndio akili za Watanzania Kuuwana Viwango.
Eti Thadeo lwanga anataka kuachwa...?
 
Simbaa wapunguze kulogana?miongoni wa Wachezaji,Tena Mchezaji ukiwa mgeni halafu unafanya vema ni kulogwa ukose namba Hizi ndio akili za Watanzania Kuuwana Viwango.
Eti Thadeo lwanga anataka kuachwa...?
Kiufundi Thadeo Lwanga hatufai Simba SC hasa huko tunakoelekea Kimataifa kwani ana Rafu za Kijinga ambazo kwa Waamuzi ( Referees ) wa Kimataifa na Wakubwa atakuwa anatugharimu lakini pia ni Mzito hana Kasi hasa Timu ikiwa inashambuliwa.

Akiachwa nitapongeza na hakutokuwa na Pengo hasa ukizingatia Mwanangu mwenyewe Jonas Gerald Mkude amesharejea tena safari hii ametakata kabisa na ameshatengeneza 'Chemistry' nzuri na Mwamba Saido Kanoute wakiwa pamoja na Punda Muzamiri Yasini.
 
Kiufundi Thadeo Lwanga hatufai Simba SC hasa huko tunakoelekea Kimataifa kwani ana Rafu za Kijinga ambazo kwa Waamuzi ( Referees ) wa Kimataifa na Wakubwa atakuwa anatugharimu lakini pia ni Mzito hana Kasi hasa Timu ikiwa inashambuliwa.

Akiachwa nitapongeza na hakutokuwa na Pengo hasa ukizingatia Mwanangu mwenyewe Jonas Gerald Mkude amesharejea tena safari hii ametakata kabisa na ameshatengeneza 'Chemistry' nzuri na Mwamba Saido Kanoute wakiwa pamoja na Punda Muzamiri Yasini.
Ngoja niulize kwa nia na lengo la kuelewa hayo juu ya Thadeo Lwanga. Hivi kwa mfumo wa kocha aliyondoka SSC juzi juzi, Thadeo Lwanga alikuwa akicheza kama nani - Attacking or Defending Midfielder!? Kasi ya mchezaji inategemea na nafasi achezayo, kama ni Attaking au Defending Midfielder, sasa Lwanga yuko nafasi gani kati ya hizo? Tukijua hilo, then tutajua kama anahitajika awe na mwepesi, mzito au awe na spidi. Nawasilisha!
 
Asante ila tabia yangu hii ya Uhalisia huu ulioutaja ndiyo unanifanya nichukiwe na nipigwe 'Zengwe' na Wapuuzi ( Hopeless ) kadhaa ( japo siyo Wote ) hapa Jamvini na hata nje ya Mtandao huu wa JamiiForums.
Anaekuchukia wewe kwa kua na uthubutu wa kusema mawazo yako inapaswa ajichukie yeye kwanza. Una jeuri (sorry kwakutumia neno hili) na uthubutu kamili usio na shaka kwenye kile unachoamini. Endelea kua wewe, anaechukia uandikacho ni ana matatizo.
 
Morrison na yeye atupishe,ana utoto mwingi ,anatafuta Kadi za kijinga
Mimi ndiyo siyo tu Simkubali lakini pia Simpendi ndani ya Kikosi cha Simba SC kwani ana Upuuzi wa 95% na Ufanisi wa 5% tu Kiuchezaji.
 
Back
Top Bottom