Asanteni sana Uongozi wa Simba SC na Bodi ya Simba SC kutusikiliza 'Wadau' na kuamua kuwa Mchezaji Ousmane Sakho 'hatotemwa' Kikosini

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,551
108,888
Naomba GENTAMYCINE nianze Kwanza kwa kutoa Pongezi kwa wana Simba SC Wenzangu wote ( hasa tuliopo hapa JamiiForums ) ambao tokea Juzi nilipoanzisha Uzi wa Kuzuia Mshambuliaji Ousmane Papi Sakho ( Raia wa Senegal ) Kuachwa ( Kutemwa ) Kikosini Simba SC kwa pamoja tulipaza Sauti zetu za Kuzuia hilo.

Pia tuupongeze sana huu Mtandao Wetu pendwa wa JamiiForums kwani ni Mtandao ambao una Sauti Kubwa na Ushawishi wa Kimaamuzi hasa ikiaminika kuwa Members wa hapa ni Great Thinkers hasa na wakisema au wakishauri Jambo basi jua kwa 85% huwa ni sahihi na pia lina Mantiki ( Logic ) ndani yake.

Kwa taarifa ambazo nimezipata kutoka kwa Waandamizi Watatu ndani ya Bodi ya Simba SC ni kwamba wamesikiliza Kilio cha wana Simba SC wote ( tunaojua Mpira na wenye Jicho pana la Mchezo wa Soka ) na kuamua kuwa Mshambuliaji na Winga Ousmane Papi Sakho ( ambaye GENTAMYCINE namkubali sana kama ninavyomkubali mno Kiungo Jonas Gerald Mkude ) hatoachwa ( hatotemwa ) kama ilivyokuwa imesemwa au imeenezwa hapo awali.

Hata hivyo wana Simba SC Wenzangu tusichoke Kupaza Sauti zetu kuhusu Mchezaji Sakho kutokuachwa Kikosini kwani Bodi ya Simba SC ina Wajumbe wengi ila mpaka sasa Wajumbe Waandamizi Watatu ( wenye Ushawishi mkubwa kwa Wanachama, Wapenzi na Mashabiki ) wamekataa Sakho Kuachwa ( Kutemwa ) na kutaka avumiliwe kwakuwa alipatwa na Majeruhi na apewe muda zaidi kwani ni Hazina Kubwa kwa aina ya Kipaji cha hali ya Juu alichonacho.

Mwisho nawaomba wale ambao tokea Juzi katika ule Uzi wangu wa Kukataa ( Kupinga ) Sakho asiachwe Simba SC mlikuja Kutudhihaki, Kutusanifu na wengine hata Kututukana tafadhali msiache kufanya bali endeleeni kwani huwa mnatupa Chachu ya Kuimarisha zaidi Fikra zetu pana huku nyie mkiendelea tu kubakia na Uzuzu ( Ujuha ) wenu mliobarikiwa na mtakaokufa nao.

Mshauri Mkuu wa Mwekezaji Mo Dewji na Mshauri Mwandamizi wa Bodi ya Simba SC 'Poti' wangu Crescentius Magori endelea Kutufikishia haya Mawazo yetu huko kwa Wakubwa na Asante kwa kuwa Mmoja wa 'Followers' wangu hapa JamiiForums hivyo naamini nikiwa naandika mambo 'Serious' hapa kuihusu Simba SC yetu huwa unayasoma na Kuyafikisha haraka Uongozini.

Muacheni Duncan Nyoni, Peter Banda, Pascal Wawa na Chris Mugalu, ila Thadeo Lwanga, Saido Kanoute na Ousmane Sakho msiwaache lakini mpeni ONYO KALI na la Mwisho Bernard Morrison kuwa wana Simba SC hatutaki na tena tumechoka na 'Mbwembwe' zake za ndani na nje ya Uwanja bali tunataka acheze Mpira, awe na Ufanisi, asiwe Mbinafsi na asipende Kucheza na Jukwaa bali tunataka KAZI KAZI Kikosini na siyo Upuuzi na Utoto wake.

Na binafsi nisifiche au kuwa MNAFIKI kuwa SIMKUBALI na NIMESHAMCHOKA kwani Bernard Morrison anatumia Nguvu Kubwa kuutaka 'Ufalme' ambao bado hana ndani ya Kikosi cha Simba SC na hataki Kujifunza ni kwanini Emanuel Okwi au Clatous Chama waliupata na walifanya nini ndani ya Simba SC wakawa 'Wafalme' ambao leo kila mwana Simba SC anawakumbuka na tunafurahi Kubahatika kuwa nao.
 
Daah hapo kwa Morrison umeongea point kubwa Sana. Huyu mchezaji Kuna muda najiuliza benchi la ufundi linamwogopa? Maana Kuna siku anakua na Mambo ya hovyo Sana uwanjan.

Huyu aambiwe ukweli kuwa mpira wa showoff Simba hawautaki wanataka upige kazi ya maana na kuwa serious kwa kila game ,pia ubinafs apunguze na chenga nyingi zisizo na ulazima aache Mara moja ,panabobid kutoa pass atoe asitake kucheza mpira wa peke ake.

Pia Aambiwe kuwa ukitemwa saiz na Simba asifikir anaweza kurud Tena Yanga ,maana yanga hawana hamu nae ,so hata akitemwa Simba labda aende Azam huko ambako najua hatakuwa na madhara ,na bahat mbaya kwake wachezaj wa ndan wameshaanza kumsoma aina ya uchezaj wake .
 
Naomba GENTAMYCINE nianze Kwanza kwa kutoa Pongezi kwa wana Simba SC Wenzangu wote ( hasa tuliopo hapa JamiiForums ) ambao tokea Juzi nilipoanzisha Uzi wa Kuzuia Mshambuliaji Ousmane Papi Sakho ( Raia wa Senegal ) Kuachwa ( Kutemwa ) Kikosini Simba SC kwa pamoja tulipaza Sauti zetu za Kuzuia hilo...
Huyu ndie mchezaji alieperform vyema pre-season leo wanataka kumuacha......Angeenda Azam maji tungeita mma
 
Naomba GENTAMYCINE nianze Kwanza kwa kutoa Pongezi kwa wana Simba SC Wenzangu wote ( hasa tuliopo hapa JamiiForums ) ambao tokea Juzi nilipoanzisha Uzi wa Kuzuia Mshambuliaji Ousmane Papi Sakho ( Raia wa Senegal ) Kuachwa ( Kutemwa ) Kikosini Simba SC kwa pamoja tulipaza Sauti zetu za Kuzuia hilo...
Mimi mengine nakuachia na mashabiki wenzio, lakini la Morrison nakuunga mkono 100/100. Niliwahi kumsema vibaya siku alipovua nguo nikaambulia kuitwa Yanga.

Binafsi nilishaachana na ushabiki wa vilabu nikabaki ni ushabiki wa mpira, lakini Morrison ni kirusi. Klabu ya Man City ilihitaji sana huduma za mshambuliaji Mario Balloteli lakini vitendo vyake vilipoanza kushusha hadhi ya timu alifurushwa na kulazimika kuingia gharama za kumtafuta Kun Aguero.
 
mmna machale kweli kweli, mngemwacha tuu, sisi 'chawa' tulikuwa tuna mdaka pale terminal 3 kabla hajapanda ndege kurudi kwao….

na mkidanganyika tuu mka mwacha huyo msenegali, baada ya miezi3 hamta amini macho yenu……….
 
Naomba GENTAMYCINE nianze Kwanza kwa kutoa Pongezi kwa wana Simba SC Wenzangu wote ( hasa tuliopo hapa JamiiForums ) ambao tokea Juzi nilipoanzisha Uzi wa Kuzuia Mshambuliaji Ousmane Papi Sakho ( Raia wa Senegal ) Kuachwa ( Kutemwa ) Kikosini Simba SC kwa pamoja tulipaza Sauti zetu za Kuzuia hilo...
Ujumbe mzuri Sana mkuu. Una jicho la kuona wachezaji wenye vipaji kama nilivyo mimi.
 
NATEGEMEA BAADA YA SIKU KAZAA KULETA UZI WA KUOMBA SAKHO AFUKUZWE ATA CLIP ZAKE UKO ALIKOTOKA ALIKUWA ANAFANYA VIZURI MAZOEZINI TU SIO MATCH IN SHORT HIS TRANSFER IS INTERNAL ROBBERY JAMAA HAFIKI HATA UWEZO WA RASHID JUMA TIME WILL TELL
Sackho hamna kitu kabisa.

Nashangaa wanavyomsisitiza, mi nimeangalia mechi zote alizocheza na sijaona chochohe. Kwa Peter Banda nimeona kitu flani kizuri kinachoweza kuangaliwa kwakuwa bado mdogo.

Mchezaji wa ukweli hapepewi hata kidogo akiingia uwanjani anakiwasha tu.

Sackho si wa kucheza Simba.

Skauti ya Simba haiko vizuri kabisa.

Msimu huu Yanga wametuzidi sana kwa swala la usajiri.
 
Back
Top Bottom