Asante Mungu muumbaji wa Mbingu na Ardhi kwa wema na Rehema zako

Tony Laurent

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
4,728
5,444
Namshukuru Mungu kwa wema wake kwangu. Pamoja na changamoto mbalimbali ninazopitia hapa duniani, bado wema wake ni mkuu mno kwangu.

Ndugu wasomaji wa ujumbe huu, nawasihi tuwe na tabia/desturi ya kumshukuru Mwenyezi Mungu hata kwa kidogo tulichopewa. Shukrani hufungua milango mingine ya baraka zaidi.

Tusiwe watu wa kunung'unika, haijalishi tunapitia mazingira magumu kiasi gani, najua inaweza kuwa vigumu kibinadamu, lakini tunaweza kushinda jaribu la kung'unika kwa kumwomba Mungu atupe moyo wa shukrani na kuendelea kupambana huku tukimtanguliza yeye katika Jina la Yesu Kristo.

Mlale unono na muwe na njozi njema
 
Back
Top Bottom