Asante Mungu kwa upendo wako usio na kifani

Sep 30, 2018
94
125
Habari zenu wanajamvi.Nawasalimu katika Jina Kuu la Bwana wetu Yesu Kristo lipitalo majina yote.Ni wakati mwingine tena ambao kwa upendeleo Mungu ametupa hapa duniani kuwepo na ni jambo la kumshukuru sana mungu kwa mambo yote ambayo ametutendea katika maisha yetu.Napenda kibinafsi kuongelea kidogo kuhusu maisha yangu japo kwa ufupi kwa sehemu kama ya shukrani kwa Mungu na Ushuhuda ambao ukimpendeza Mungu ukaguse maisha ya wengine ndani na nje ya platform hii.mimi ni mzaliwa wa Arusha kijana mdogo ambaye nimelelewa katika maisha ya dini ya kikristo katika dhehebu X.ninashukuru Mungu kwa kunipa wazazi wenye uwezo na hekima ya kutuongoza katika njia sahihi ya maisha kuwa na upendo na watu wengine na kuwafikiria wengine(being considerate).kwetu nyumbani tupo watano na mimi nikiwa mtoto wa mwisho.maisha yalikuwa yanaenda vizuri kabisa sikuwahi kukosa kanisani either kusali au kufanya usafi na ninakumbuka kun kipindi nikapewa nafasi ya kuwa mfanya usafi kufuta vumbi kwa upande wa viti vya kanisa na mazingira ya ndani kwa ujumla ya kanisa.baada ya kumaliza kidato cha nne nikawa nipo likizo tu sina hili wala lile nikaanza kufikiria kuhusu kuwa na girlfriend kwa kuwa sikuwah kuchukulia serious hii ishu na sikuwa na kazi nying sana za kufanya (an idle mind=devil workshop) so nikamcheki classmate wangu mmoja aliyekuwa mchangamfu na social nikawasiliana naye na kwa kuwa nilishakuwa na mazoea naye kidogo ikafika siku nikamwambia ukweli ila akawa hayupo tayari kwa sababu tofauti tofauti.muda ukaenda tukaenda advanced ila nikiwa na mawazo mengi kichwani kuhusu shule kama kweli nitatoboa + shule nliyochaguliwa haikuwa na status kivile na alishawah ssta kuulizia kama kwa combination yangu mtu atatoboa kweli akaambiwa haiwezekani maana walimu hamna na ni wachache kwa masomo mengine mazingira ya maabara+facilities nyingine sio conducive .bila kusahau kutokuelewana na huyu classmate amabye mimi nillimchukulia serious sana kuliko ilivyotakiwa.nikaingia kwenye dimbwi la mawazo kuhusu shule +mapenzi nikaamua nipambane na kitabu wala skutaka mazoea na side B maana nliona weng hawapo tayar kuwa in serious relationship so nkapambana na shule japo ilikuwa ngumu + mazingira ilinichukua muda kuzoea.kipindi cha advanced kilikuw kipindi kizito katika maisha yangu sijapata kuona kwani nilipata depression(sonona) kuhusu ishu ya masomo yalivyo mazito + hofu niliyoingia nayo shule + mahusiano mabovu mimi na Yule o level classmate ilifikia hadi wakati nikawa nafikiria kucomit suicide(akili za kitoto enzi hizo).marafiki zangu waliokuw wameniona vizuri wakajua kuna tatzo na kuna kipindi nikawaambia kila kitu na nakumbuka mmoja wao aliwahi kuniambia

“kama hujaikubali hii shule + mazingira yake usikae kimya ongea na mzee wako ili mwisho wa siku tusije kukukuta mwenzetu umejitia kitanzi bure”(nikikumbuka hii statement huwa nacheka)

.nikivuta picha nakumbuka watu mbalimbali ikiwemo marafiki zangu wa karibu kabisa mmojawapo alinishauri kuhusu kusali na kumtafuta Mungu pamoja na kujaribu kupunguza mawasiliano na kufocus kwenye mambo mengine ambayo ni positive zaidi…I pray for this brother to be blessed abundantly

Kwani ninaamini maneno yake yalipanda mbegu flani katika moyo wangu moja ikiwa ni kusamehe na kusahau na kuendelea na mambo yenye msingi zaidi katika maisha yangu ikiwemo kumtanguliza Mungu kila hatua.

Advanced nilimaliza lakini sikupata ufaulu wa kunivusha kwenda degree hivyo nafasi iliyobaki ilikuwa kwenda kusomea diploma ya afya kwa kuwa nilikuwa interested nayo from beginning.nilifanikiwa kupata nafasi katika chuo kimoja chenye sifa nzuri na hadhi kwa ishu za afya.kwa wakati wote ambao nimekuwa hapa chuoni mambo mengi nimejifunza sana kuhusu maisha na kuhusu Mungu hasa umuhimu wa kuwa na mahusiano na Mungu katika maisha yetu.ninamshukuru mungu kwa yote aliyonipa mpaka sasa maisha yangu yamebadilika na nina amani ya moyoni na sina wasiwasi wowote tofauti na mwanzo kuhusu future yangu kwani ninajua Mungu anajua mwanzo wangu na mwisho wangu.Mungu wangu huyu kaniepusha na mambo mengi sana sitaweza kuyamaliza hapahapa lakini kiufupi kaniepusha na ajali,magonjwa na kifo kwa ujumla.

Ninakushukuru kwa Baraka zako afya njema,hewa safi ya bure kabisa,ulinzi wa nchi yetu,marafiki na familia zetu kila iitwapo siku,chakula na mahali pa kulala.Ninakushukuru Ee Baba wa Mianga ya Mbinguni kwa kuwa hata nilipokuwa katika lindi la mawazo ulifanyika kuwa kitambaa na ukanifuta machozi,ulikuwa faraja yangu katika yote niliyopitia pamoja na upweke moyoni mwangu ulinitia nguvu wewe mwenyewe kwa roho yako na kwa kupitia marafiki na watu mbalimbali uliowatumia kwa utukufu wa Jina lako iwe kwa ushauri au maombi Ee Mungu ninakuomba ukawabariki katika hatua zao zote kulingana na mapenzi yako.

Jina la Bwana Yesu Kristo,Jina pekee Linalookoa,Jina lenye Uzima Na Baraka Tele,Jina kuu lipitalo yote ,Jina Lenye Nguvu kupita yote Libarikiwe Milele.AMINA
 
Sep 30, 2018
94
125
Kwa umri wako ni muujiza kutambua umuhimu wa Mungu katika maisha yako
Ni habari njema sana hii mimi nimeisoma natamani watoto wangu nao watembee katika neema kama hii.
Nashukuru umeandika kitu chanya uwe mwanga hapo ulipo kwa njia tofauti najua utatumika kumvunia Mungu nafsi hapo chuoni ulipo.
amina kabisa mkuu.ni maombi yangu Mungu aniongoze nitumike vyema kwa utukufu wake na nikiangalia nyuma hata hapa nilipo nisingeweza kupiga hatua hata moja kama Mungu hakuwa nami.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom