Asante Mama Samia kwa utenguzi huu; Ulichelewa kidogo

MUSONI

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
903
682
Hongera Mama kwa jicho kuona huko nishati kuna mengi najua ni mwanzo HONGERA SANA
 

Attachments

  • UTENGUZI JAN 2024.jpg
    UTENGUZI JAN 2024.jpg
    49.1 KB · Views: 3
Mimi nadhani awe anatoa pia na sababu ya kuwatengua hao wateule wake, ili na sisi wananchi tuwe upande wake katika hayo maamuzi yake.
Hizi tenguzi hata hazifuati sheria za utumishi wa UMMA,
Unampa tu ajira bila mkataba ukiamua kumuondoa unamuondoa hata bila kutoa sababu.Nchi hiiiiiii
 
Huyu Mala.....ya wa kisabato ataenda kanisani leo tunamsubiri....amevuruga kanisa sana kuzaa wake za watu pale SDA Magomeni........
 
Mimi nadhani awe anatoa pia na sababu ya kuwatengua hao wateule wake, ili na sisi wananchi tuwe upande wake katika hayo maamuzi yake.
Naunga mkono hoja, kiukweli katiba yetu, sheria zetu, taratibu zetu na kanuni zetu, zinamapungufu makubwa!.

Kwenye presidential appointments powers, rais anaweza kumteua mtu yoyote kwenye nafasi yoyote, bila kutoa sababu yoyote ya appointment hiyo kwa yeyote, na pia anaweza kutengua uteuzi wowote kwa yeyote bila kutakiwa kutoa sababu zozote!.

Mtu akiishateuliwa na rais kwenye public office, huyu sasa ni mtumishi wa watu, japo ni msaidizi wa rais, lakini sio mtumishi wa rais!. Watumishi wa rais ni wale wanaomtumikia yeye ofisini kwake, nyumbani kwake na dereva wake, kama hawapendi anawaondoa tuu bila kutoa sababu yoyote.

Lakini kwa public servants waotumikia public, wakitenguliwa, the public has the right to information kwanini wametenguliwa!.

Baada ya kumtengua Balozi Mulamula, kukatokea vineno... hivyo nikashauri Should We Demand More Right to Information Kwenye Teuzi za Key Posts? Ziwe Endorsed na Bunge With Security of Tenure? Mawaziri Wasiwe Wabunge?

Kwa jinsi ninavyomfahamu huyu jamaa Sijui kafanya nini kustahili kutimuliwa!, ila kwa maoni yangu, huyu jamaa ni mmoja ya majitu very bold pale Wizarani, ambao serikali yetu imebahatika kuwa nao, hili jamaa limesimama wima kusimamia ukweli no matter what!, na kiukweli tulifanikiwa sana kudhibiti makuwadi wa mafuta na kuzuia ma cartels!. Wakati wa upungufu wa mafuta ya petrol, nilifanya nae mahojiano marefu
View: https://youtu.be/s-ZYP33jjww?si=FQJucdhOK-p1gxPh . Kiukweli the guy is smart!, sijui kumetokea nini?!, ila ukiwa mkweli mno, katika corrupt system, sometimes unaonekana kikwazo!. Issues kama hizi ndizo za sisi waandishi makini kuzifanyia IJ.

Tanzania tunajikuta tunapoteza watu wazuri, wachapakazi, waadilifu kwa majungu tuu na fitna ndio maana tunasisitiza, kwenye kuteua, kwasababu kuna sifa na vigezo, sio lazima tuambiwe sababu za fulani kuteuliwa, hata akiwa ni mkwe wa rais, ndugu, jamaa au marafiki, ni sawa tuu alimradi anakidhi vigezo, lakini kwenye kutumbua, lazima tuwe tunaelezwa sababu not necessarily in details.

Japo kuna kitu kinaitwa the right to privacy, but when it comes to public offices and public offices there is no right to privacy besides yale ya nyumbani!, whoever paid by taxpayers money, the taxpayers have the right to information public and private conduct of their leaders because it's there money!.
P
 
Hizi tenguzi hata hazifuati sheria za utumishi wa UMMA,
Unampa tu ajira bila mkataba ukiamua kumuondoa unamuondoa hata bila kutoa sababu.Nchi hiiiiiii
Sheria ya utumishi wa umma inasemaje Kuhusu teuzi za rais?
 
Back
Top Bottom