Nikikumbuka tulikotoka, ugumu wa maisha kisiasa na uhalisia wa maisha ya mtu mmoja mmoja, nashawishika kumkubali Samia hadharani bila hata haya wala soni.
Watanzania tuna mengi ya kuridhika kupitia huyu mama kwa kuangalia rekodi za hapo nyuma, ambapo watu wengine waliishi kwa hofu, kutokana pengine na itikadi zao, misimamo tofauti na pengine hata chuki binafsi.
Aidha nakubaliana nae juu ya mabadiliko kadhaa ya sheria zetu zinazohusu namna bora ya uendeshaji siasa zetu, na kwa kweli huu ni mwanzo mzuri kwa demokrasia yetu. Hongera Rais, ni mwanzo mzuri.