Mtanzania Edward Erihard (31) Mkazi wa Dodoma anashikiliwa na Polisi Mkoani Manyara kwa kosa la kusafirisha kinyume na sheria Wahamiaji 20 Raia wa Ethiopia.

Akiongea Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara ACP Lucas Mwakatundu amesema tukio hilo limetokea March 23 2024 ambapo gari hilo limekamatwa katika kizuizi barabara ya Arusha Babati eneo la Minjingu likiwa na Wahamiaji ishirini Raia wa Ethiopia kwenye gari namba T.774 BDL Land Cruiser likiwa na bendera ya Chama cha Mapinduzi CCM.

“Gari hili V8 lilikuwa na Bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kwenye upekuzi tulipoona sura tofauti na Watanzania ilibidi tuweke gari pembeni na baadae kuwashusha tukakuta wapo Wahamiaji 20 kwenye gari V8 na wote uelekeo wao ni kusini mwa Afrika wakitokea usawa wa Arusha, Dereva wa gari hili ni Mkazi wa Dodoma tunamshikilia mpaka sasa na kesho tunatarajia kuwakabidhi Uhamiaji”


Chanzo: Ayo TV
Nashindwa kuona walikaa vipi watu 20 kwenye V8.😂🤣
 
Sasa kwani wahamiaji si wanaweza kujitambulisha kama wakimbizi ili kukwepa kesi ya uhamiaji haram
Mhamiaji ni yule anaeingia kwenye nchi kama walivyoingia Wahindi na waarabu na mataifa mengi ili kuja kuishi na kuomba resident permit

Hapo kwenye ukimbizi ni mtu alieingia aidha kinyemela au kujilipua borders na kusema yeye ni mkimbizi kutoka nchi fulani na anahitaji hifadhi
Kama ukisema wewe ni mhamiaji utaulizwa maswali na hapo kama una passport maana wengine hawana passport kabisa wakiogopa kurudishwa walikotoka
 
Back
Top Bottom