Arusha: Zoezi la uokoaji katika uwanja wa ndege lagharimu milioni 18

Restless Hustler

JF-Expert Member
Apr 9, 2017
4,742
17,979
Meneja wa Kiwanja cha Ndege Arusha, Elipid Tesha amesema zoezi la ajali ya ndege kuungua moto katika eneo hilo limefanyika kwa lengo la kuona utayari wa Taasisi za uokoaji namna gani zinaweza kuwahi eneo la tukio na kila mmoja kuweza kutimiza wajibu wake.

Aidha, Elipid amesema zoezi hilo limegharimu zaidi ya Milioni 18 kuandaa na hufanyika kila baada ya miaka miwili.

"Zoezi kama hili linagharimu kiasi kikubwa cha ela kwasababu kuna vikao, maandalizi ya vifaa na inachukua muda inaweza kuchukua hata miezi sita wakati wa kujiandaa"
 
Kuna mjinga mmoja atakuambia. Watanzania tuwe wazalendo.

Nchi bado inahangaika na matundu ya choo ya wanafunzi na madawati lakini kuna watu wanakula milion 18.

Ndiyo maana tozo zimekuwa nyingi sana kumbe kuna watu wanataka kulamba asali
 
Upigaji wa kidezi sana, hao watu wanaona watanzania kwa kuishia darasa la saba ni wajinga kabisa kuchambua hata jambo dogo.
 
Milioni 18 kwenye capacity building ni kitu gani hicho cha kujadili hapa!

Iyo ni hela ya Dinner tu ya Staffs

Tusiwe na mawazo madogo hivo!!

Kujengeana uwezo ni gharama.

Ndege ya Billions ingeokolewa msingeongea.

Poor sight!!
 
Tutamkumbuka sana Magufuli ijapokuwa alikuwa na mazuri na mabaya, lakini ujinga unaoendelea sasa nchini tumerudi kwenye zile enzi ya BUSINESS AS USUAL.

Tutarajie matajiri wachache na maskini wakubwa, ile kauli ya NCHI INAUZWA tutaona vizuri baada ya miaka kumi. Pamojoa na yote hayo Mungu atabakia kuwa Mungu, chochote apandacho mtu ndicho atakachovuna.
 
Meneja wa Kiwanja cha Ndege Arusha, Elipid Tesha amesema zoezi la ajali ya ndege kuungua moto katika eneo hilo limefanyika kwa lengo la kuona utayari wa Taasisi za uokoaji namna gani zinaweza kuwahi eneo la tukio na kila mmoja kuweza kutimiza wajibu wake.

Aidha, Elipid amesema zoezi hilo limegharimu zaidi ya Milioni 18 kuandaa na hufanyika kila baada ya miaka miwili.

"Zoezi kama hili linagharimu kiasi kikubwa cha ela kwasababu kuna vikao, maandalizi ya vifaa na inachukua muda inaweza kuchukua hata miezi sita wakati wa kujiandaa"
Sasa kama ni kujipima utayari halafu wanajiandaa kwa hadi miezi sita, hapo wanapima nini kama sio maigizo? Sijui kama ndege ikianguka hapo itawapa muda wa kujiandaa hata wa dakika 10
 
Back
Top Bottom