ARUSHA: Msomi Chuo Kikuu Makumira ajinyonga kwa mtandio

ARUSHA: Msomi Chuo Kikuu Makumira ajinyonga kwa mtandio

Ooh maskini, kama ndo hivyo basi labda alipata stress za kumpoteza mtoto wake. Nafuta kauli yangu...R.i.p dada

Ndio hivo arobaini toka kuzaliwa mtoto wake nilienda tukala msosi fresh ghafla mwezi wa tatu likizo napata taarifa yule mtoto ameumwa kafarik, Juz juzi Tu hapo nmewazungusha mjini na kuwarudisha hpa makumira , JAna nae ametuacha alikuaga hana shida na mtu uyu dada,
 
Rest in peace dear, sijui yaliyokukuta mpaka ukaamua hivyo... ulale salama.
 
Itakuwa msongo wa mawazo, ila yote uamuzi huu haukuwa sahihi maana wanaobaki ndo wanapata machungu na sio muhusika.

kuweni wawazi kidogo wakuu pale yakiwafika shingoni, pia watu mpunguze dhihaka na kejeli maana kuna watu yakiwafika wanakimbilia/tunakimbiliq huku. kujua tutapata ahueni ila unakutana na majibu ya hovyo unaamua kuwahi kiwanja tu.
 
dah nimesikitika sana kwa uamuzi uliochukua lucy, r.i.p
 
*TANZIA*

Kwa niaba ya Uongozi wa
Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, na Serikali ya Wanafunzi (TUMASO) *Wizara ya Afya* inasikitika kutangaza kifo cha mwanafunzi
*Luciana Richard Olotu* kilichotokea tarehe 07.05.2018.

Kwa masikitiko na majonzi makubwa, marehemu majira ya saa 11 jioni alikutwa amejinyonga bafuni.

Hadi police walipofika na kuuchukua mwili kwenda kuuhifadhi ktk Hospitali ya Mt. Meru, sababu ya maamuzi ya kujinyonga hazijajulikani bado. Jeshi la Police linaendelea na uchunguzi.

Marehemu alikuwa mwaka wa pili ktk Kitivo cha Humanity and Social Science program ya BAED.

Uongozi unatoa pole Kwa mshtuko na simanzi ya kupotelewa na wanafunzi
*Luciana Richard Olotu*

Wizara itaendelea kutoa taarifa kuhusu taratibu zitakazofuata.

*Cc* .
1. Dean of Students
2. Rais wa Tumaso
3. Waziri Mkuu
4. Speaker wa Bunge

[emoji767]WIZARA YA HABARI TUMASO 2017_18View attachment 769594
Malaika wa kifo anapokuwa na nguvu kuzidi utashi wako
 
Ndio hivo arobaini toka kuzaliwa mtoto wake nilienda tukala msosi fresh ghafla mwezi wa tatu likizo napata taarifa yule mtoto ameumwa kafarik, Juz juzi Tu hapo nmewazungusha mjini na kuwarudisha hpa makumira , JAna nae ametuacha alikuaga hana shida na mtu uyu dada,
Pole sana.
 
Back
Top Bottom