PatPending
JF-Expert Member
- Aug 17, 2007
- 493
- 109
Wafungiwe leseni wote wale waloogoma. Lema mwenyewe kapenda kwenda gerezani. Sasa hao wa viford wanagoma ili nini?
Uamuzi wa kutoa au kutotoa huduma ni haki halali ya kibinadamu na kikatiba ya hawa waheshimiwa. Ukitafakari vizuri madereva hawa hawagomi kwa sababu Lema ameenda rumande BALI wanagoma kutokana na kuchoshwa kwao na vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na vyombo vya dola dhidi yao. Madereva wa daladala Morogoro pia waligoma kutoa huduma kwa sababu kama hizi mapema mwaka huu.
Vitendo vya daladala kunyanyaswa na askari polisi vimeshamiri sana Tanzania ambapo polisi hufanya daladala kama mashamba yao ya kujivutia fedha za mboga kila siku.
Mgomo kama huu waweza pia kutokea Dar. Ni vyema tukaliangalia tatizo hili kwa upana zaidi badala ya utashi wa kisiasa