rums
Break news: katibu wa
mkoa wa kinondoni na
kanda maalum ya Dar es
salaam atoa tamko kali
kuhusu mbunge wa Arusha
mjini;
TAMKO HILI HAPA.
MKOA WA KINONDONI
KANDA MAALUM YA DAR
ES SALAAM
Tamko la katibu wa mkoa
wa Kinondoni Kanda Maalum
ya Dar es salaam
Ndugu zangu wanahabari
Nimewaita hapa leo kwa
lengo la kuwapa watanzania
msimamamo wangu na wa
chama ngazi ya mkoa
kuhusu tukio la kukamatwa
na kupelekwa magereza
kwa Mhe. Godbless Lema
Mbunge wa jimbo la Arusha
Mjini.
Imekuwa ikizoeleka kwa
muda mrefu sasa kwamba
waheshimiwa wabunge wa
CHADEMA na wale
wanaaotokana na vyama
vya upinzani wamekuwa
wakinyanyaswa sana kwa
lengo la kuwafanya wajute
kuingia katika siasa za
upinzani Tanzania.
Hii kwa CHADEMA haitokei
tu kwa waheshimiwa
wabunge bali hata kwa
viongozi wa ngazi zote.
Inaonekana kuwa sasa
serikali ya Chama Cha
Mapinduzi imeamua
kutekeleza kwa vitendo
mkakati wa kuwatesa kwa
siri na kwa wazi wale wote
wanaoipinga siasa
kandamizi na
zisizowalazimisha watawala
kuwajibika kwa wananchi.
Mkakati huu umetungwa na
CCM, unasimamiwa na
usalama wa taifa na
unatekelezwa na jeshi la
polisi. Kwa hakika hatuhoji
tena kwamba jeshi la polisi
ni kitengo cha kusimamia
maamuzi na maelekezo ya
CCM badala ya kulinda raia
na mali zao.
Mheshimiwa Godbless kama
mbunge wa wananchi wa
jimbo la Arusha Mjini
amekuwa akifuatwafuatwa
na jeshi la polisi kila mara na
kufanyiwa vitendo vingi vya
udhalilishaji na unyanyasaji
hasa kwa kupitia OCD wa
Arusha Mjini Zuberi.
Mathalani wiki iliyopita siku
ya ijumaa tarehe 28/10/2011
Mhe. Godbless lema akitoka
mahakamani alisindikizwa
na wananchi wake kutoka
mahakamani hadi ofisini
kwake. Wafuasi wake
walipomfikisha ofisini
waliondoka na kurejea
makwao. Huko ofisini
aliwakuta wananchi
wakimsubiri ili awahudumie
kama mbunge wajimbo lao.
Wakati akiongea na
wananchi ghafla polisi
walifika na kuwakamata
wananchi wote waliokuja
kuomba usikivu wa
mbunge na kuwapeleka
kituo kikuu cha polisi.
Mbunge Lema alipokwenda
kituo cha polisi kwa lengo la
kuwawekea dhamana naye
aliwekwa chini ya ulinzi
kwamba eti amefanya
maandamano bila kibali.
Tunahoji: Ni maandamano
yapi hayo ambayo Lema
aliyafanya na wananchi
wake akiwa angali ofisini
kwake? Je maandamano
wanayoyazungumzia ni
kuondoka na wananchi
mahakamani hadi ofisini
kwake? Je kama kuondoka
kwake na wafuasi wake
mahakamani ni kosa
kisheria; Je kwa Mhe Ole
Sendeka alipokuwa akitoka
mahakamani, alikuwa
akiondoka na kundi kubwa
la wafuasi wake na
kusindikizwa na OCD huyu
huyu? Vile vile Mwenyekiti
wa UV-CCM mkoa wa
Arusha amekuwa akienda
kituo kikuu cha polisi
akisidikizwa na kundi
kubwa la wafuasi wake wa
CCM. Polisi hawakuwahi
kuwakamata wala
kuwaonya. Sasa haya yote
yalikuwa maandamano ama
matembezi ya hisani? Maana
Arusha kuna msiba
mkubwa wa CCM
kukataliwa na wananchi.
Kwa hakika tukio la
kukamatwa kwa Mhe Lema,
kupelekwa mahakamani na
hatima ye kupelekwa
gerezani ni ushahidi wa
kutosha kwamba jeshi la
polisi sasa linakamilisha
sehemu kubwa wa wajibu
wake wa kuibaka
demokrasia.
Hata hivyo tunalitaka jeshi la
polisi na serikali ya CCM
wajue kwamba kitendo cha
kumpeleka Lema magereza
ni ushindi tosha katika
harakati za ukombozi wa
taifa hili. Maana hakuna
silaha yoyote duniani ama
jeshi la polisi popote pale
duniani ambavyo viliweza
kushinda vita dhidi ya
ukweli, haki na uwazi.
Ndugu zangu watanzania
Tunawaunga mkono wana
Arusha kwa kumpata
mbunge ambaye anayatetea
maslahi yao kwa mzigo hata
pale inapobidi kwenda
gerezani kwa ajili ya watu
wake na hata ikibidi kifo
anaweza kusimamia hilo.
Alisema Martin Luther King
Jr. 1963 A man who wont
die for something is not fit
to live na akaendelea
kusisitiza Nobody can give
you freedom, nobody can
give you justice or right or
anything. You take
it! (STAND UP; STAND UP 4,
UR RIGHT) Hayo yalikuwa
maono ya bob marley
ambayo aliyaona mwaka wa
1973,baada ya kuwa amekaa
katika mto mmoja huko
jamaica akaona samaki
wanapita katika maji lakini
samaki wakubwa wakawa
wanawaonea samaki
wadogo,hivyo akaona hata
hapa duniani hata wa2 walio
juu wanawaonea watu wa
hali ya chini.
Kwa watu wanaopinga ama
kukejeli maamuzi ya
Godbless lema kukataa
dhamana, Wathubutu
kufanya ziara huko
Mahospitalini wavae sura za
uhasilia wa kibinadamu
wakaone watu waliokuwa
kama wao jinsi
wanavyotaabika kwa
kukosa matibabu ile hali ni
walipa kodi wa taifa hili.
Kwanini Godbless asiende
jela wakati anasimamia
mambo ya msingi na
hayatekelezwi,
tukiandamana tunaonekana
tunavunja sheria ni afadhali
kwenda sehemu
wanayodhani tunaogopa
kuliko kukaa kimya kumbe
hatuogopi. Mungu yupo
upande wetu na tunaelekea
kushinda unyanyaswaji huu.
Kama ambavyo alivyowahi
kusema Martin Luther king
jr, ndivyo tunavyo
wahakikishia wana wa
Arusha, we will work
together; we will stand up
together, we will go to jail
together, until justice runs
down like water. maana
mateso tunayoyapata ni
makubwa kuliko huko
jehanam tusipopajua.
Kwa kuonyesha tuko
pamoja katika harakati hizi
za kudai demokrasia ya
kweli tunampogeza
Godbless lema mbunge wa
Arusha mjini kwa kupeleka
ujumbe kwa watawala
wanaodhani wanaweza
kutumia magereza kama
sehemu ya vitisho
kurudisha harakati zozote
zile nyuma.
Ujumbe huu uwafikie
watawala yakuwa jela
sisehemu ya kumtishia mtu
yeyote Yule mwenye akili
timamu, mpenda haki bali ni
sehemu ya kawaida ambapo
binadamu yeyote Yule
anaweza kwenda.
ASANTENI ASANTENI NA
MUNGU AWABARIKI
WATANZANIA WENZANGU!
Henry J Kilewo
KATIBU (M) Kan