Arusha - Je tunaridhika na utendaji wa Godbless Lema?

Ilikuwa nianze na mambo mengine ila nimeona niahirishe kwanza nichangie hoja yako. Hoja umeifikiria vizuri ila nahisi umeshindwa kuipresent. Unauliza kama mnaridhika na utendaji wa Lema na kama anatimiza majukumu mliyomhitaji ayatimize. Je majukumu mliyompa ni yapi???ungeyataja hapa ili mchangia mada anayetaka kupima utendaji wa Lema imuwie rahisi. Lakini kwa kuficha majukumu mliyomhitaji kuyatimiza unakuwa hujafanya sawa mana huwez pima chochote hapa mana perceptions zetu kwa majukumu ya wabunge zinatofautiana sana na wengi wetu hatujui majukumu ya mbunge. Kimsingi wengi wanadhani mbunge ni mfadhiri, hii si sawa.

Aidha, umesahau kuwa Madiwani walikula kiapo cha kuutumikia Umma wao wenyewe na sio kwa kupitia ushawishi wa Lema. Kumbuka hapo Arusha kuna madiwani hadi wa CCM so ukitaka kumbana Lema kwa utendaji mbovu wa madiwani unakuwa hujamtendea haki. Maana hukumchagua diwani wa CCM kwa kushawishiwa na Lema,madiwani wa CDM ok ingawa napo hupaswi kuliweka hivyo. Kila mtu diwani/mbunge ana majukumu yake aliyoapa kuyasimamia ktk kipindi chake. So mtight kila mtu individually.

Lakini naona central question ulitakiwa kuuliza wanaarusha kama wanaridhika na utendaji wa Serikali ya Kikwete. Kumbuka jukumu la Lema ni kuisimamia serikali, kutunga sheria Bungeni, kuwakilisha interests za wananchi wake bungeni na kuhamasisha/kusimamia shughuli za maendeleo, so kama Serikali haina cha kufanya kwenye maendeleo nadhan kumnyooshea Lema kidole huwa tunakosea sana. Kuna dhana potofu iliyojengeka miongoni mwetu ya kudhania Mbunge ni mfadhiri. Jukumu kubwa la Lema ni kutunga sheria bungeni, nadhani kazi hii ameifanya kwa kuchangia hoja mbalimbali ktk misaada ya sheria mbalimbali kupita wabunge wengi tu pale mjengoni. Kuhusu jukumu lake la kuibana Serikali, hapo ndo usiseme na kwenye maendeleo sina takwimu za kutosha ila kupitia hapa JF tulielezwa he is doing well. Labda utabanaishe majukumu gani mengine zaidi ya haya mlitumana huko mtaani ndo tutaweza kukuelewa otherwise, utaonekana ni mjenga chuki miongoni mwa jamii sifa ambayo ni haipaswi kumilikiwa na kijana wa karne hii.

Kwa heshima naomba kuwasilisha.

Well said kiongozi
 
walau sasa hivi hata manispaa kuna kanidhamu ya uoga kwa hofu ya lema..ile barabara ya njiro tokea nalopa mpaka njiro makaburini wamesema wataanza kuweka lami mwezi wa sita baada ya kuila na sasa lema kawakalia kooni..tutafika tu chaliangu..
 
Tukiwa ni wakazi wa Arusha tunakubaliana kwamba Arusha ni ngome ya CDM. Arusha ni jiji ambalo linaingiza pato la kutosha kwa Taifa. Lakini ndilo jiji pekee Tanzania ambalo halipangiki, halina barabara na wala haijulikani mpango wake wa kesho ni nini. Lakini kwa Mbunge wetu tunaona yuko busy na matukio yatakayomfanya awekwe ndani na polisi ili apate kura za huruma. Swali la kujiuliza
1. Majukumu ya mbunge ni yapi na Lema ametimiza mangapi.
2.Majukumu ya madiwani ni yapi na mbunge amewahamasisha madiwani wake kwa mangapi?
3.Je? tukimlinganisha Lema na Felix Mrema nani atakuwa amefanya mengi kwa maendeleo ya Arusha?
4.Je? Lema ndiye aina ya mbunge tunayemuhitaji?
naomba kuwakilisha
Hivi ulitaka watu wajadili au waendeleze mashambulizi kwa lema maana tayari umesha hukumu sasa unauliza nini sasa....Je uko tayari kufuta maelezo yako ya kipumbavu kama utagundua lema kafanya kazi kumbwa sana kwa muda mfupi kuliko mbunge yoyote kwa miaka 20 iliyopita....hii ukizingazia na hila za serikali ya CCM
 
PakaJimmy,
Yote hayo ulioyaandika yameletwa na Lema Kupitia miradi gani?

kupitia mradi wa kuisimamia serikali kama wajibu wa mbunge.. ingekuwa enzi za felix hizi zingekuwa ni ndoto..ambaye aliweza kupeleka mradi wa maji safi kwenye shamba lake la maua kule chekereni na kuwaacha wananchi na uhaba wa maji..
 
Kitu ambacho ni kigumu kukielewa ni siasa za Lema pamoja na wafuasi wake wa Arusha.

Inasikitisha sana kuona mbunge amepanda juu ya gari huku amelala gari linakwenda mwendo kasi huku wafuasi wake wanashangilia.

Sijui Wananchi na wa kazi wa Arusha wanaitaji nini kutoka kwa Lema.
Tuna hitaji kiboko ya CCM yaani mtu ambae siyo mnafiki.....Ndiyo maana Arusha wana mkubali Lema unalingine
 
mkuu umewashika pabaya wadau wengi sana hapa jamvin. Usitegemee kuna mtu atachangia kwa kumkosoa LEMA ambaye arusha wanamwona kama ndiyo raisi wao.Mungu mtu.

Kiukweli maisha ya arusha ni magumu sana vijana ambao ninguvu kazi wanaishia kunywa gongo(pure),banana,viroba na mbege,bila kusahau bangi.
Wavutaji wa unga ni wachache sana hawana uwezo wa kumudu gharama zake.

Mi ningeomba woote mnaompinga na kumtusi na kumtuhum mwanzisha thread kuwa mchimbi hembu anikeni mazuri yaliyokwisha fanywa na huyo kilema juu ya arusha.
Acheni kupenda vibaya.

Hakuna zuri likosalo kasoro.
Watu wa Arusha wana imani zao na wana amini mungu wao na si Lema ninachokiona hapa ulikusudia kuwatusi watu wa Arusha. Ukiona vijana hawana kazi wamekalia kunywa gongo na kuvuta bangi kwanza tuwapongeze hata kufanikiwa kupata hiyo pesa ya kununua gongo na bangi kwa maisha yalivyo magumu pili hili sikosa la Godbless Lema bali ni la serikali ya CCM amayo ilifunga viwanda vilivyoko hapa Arusha ambavya ni tegemeo kubwa kwa watu wa Arusha mfano General tyre lakini baada ya kuingia Lema sasa tumeanza kupata matumaaini GT imeanza kufanyakazi mbayo kama isingekuwa imefungwa ninaamini ingekuwa inategeneza tyre za africa mashaki na kati na kuna watu wangepata ajira kwenye kiwanda moja kwa moja au kwenye kilimo cha mpira na watu hao nao wangea ajiri watu hoko majumbani....Kwa hiyo basi tumpongeze kwa kufanikisha kiwanda hiki kufanyakazi ila tunamuomba afanye juhudi za kuhakikisha mali walizo uziana wafanya kazi wa zamani wa general tyre kwa bei ya kutupwa zinarudishwa mfano kuuziana gari kwa US$ 100( dola mia moja ) hii haikubaliki kabisa
 
Watu bwana wana wivu wa kike mleta mada wala huishi Arusha ila chokochoko za kumtafuta Lema! Maswali yako hayo ungemuuliza mbunge wako ningekuona wa maana sana!
 
Kwani wabunge ndo wanaojenga bara2 au kuwaletea maendeleo wananchi wa majimbo yao? Hao wa CCM wamefanya nini cha ajabu; mbona inaonekana kama vile hatujui kazi na majukumu ya wabunge! Kazi zote za maendeleo katika jamii hufanywa na Serikali kwa fedha za serikali. sasa kama jimbo halijapelekewa hayo maendeleo mnataka kusema mbunge afanye kwa gharama zake? Kwani bajeti ya serikali inapangwa na mmbunge au serikali kisha kuwasilishwa bungeni, au ni wabunge wanapanga bajeti kisha kuwasilisha serikalini?

Kwa hili tujaribu kushirikisha akili zaidi badal ya ushabiki zaidi.
 
Ndio tatizo la kuchagua wabunge wa majaribio, kama chadema hawatatafuta mtu strong 2015 jimbo linarudi ccm. Huyo lema wampe udiwani tu sana sana maana naona ni muuza sura tu hana mpya.
 
Tuna hitaji kiboko ya CCM yaani mtu ambae siyo mnafiki.....Ndiyo maana Arusha wana mkubali Lema unalingine
Nyie si ndio mnaegawana nae zile posho, utatetea sana huyo jambazi lakini wana arusha wanakiona cha mtema kuni.
 
Asijidanganye mtu kuwa mbunge wa upinzani anaweza kutimiza ahadi zake za kampeni, atachokifanya zaidi ni kufatilia yaleyale yatakayotimizwa na Serikali iliyopo madarakani, na sera zitakuwa ni za chama tawala.

Cha ziada atakachokifanya ni kupiga porojo tu.

Kumbe wanafuatilia miradi inayotekelezwa, Wewe ulitaka waanzishe miradi yao, Duh nae unajiita Great thinker?
 
asijidanganye mtu kuwa mbunge wa upinzani anaweza kutimiza ahadi zake za kampeni, atachokifanya zaidi ni kufatilia yaleyale yatakayotimizwa na serikali iliyopo madarakani, na sera zitakuwa ni za chama tawala.

Cha ziada atakachokifanya ni kupiga porojo tu.

huenda kukawa na shida ya tafasri ya usimamiaji wa sera.
Mbunge ni mwakilishi wa wananchi,kazi yake ni kuhakikisha serikali inatatua matatizo ya wananchi kama maji,barabara,huduma za afya, hili halihitaji chama tawala bali mahitaji ya wananchi kwani ndo walipa kodi na wala si vinginevyo.
 
Ndio tatizo la kuchagua wabunge wa majaribio, kama chadema hawatatafuta mtu strong 2015 jimbo linarudi ccm. Huyo lema wampe udiwani tu sana sana maana naona ni muuza sura tu hana mpya.

Kama wapiga kura mtakua wewe na familia yako tu ni kweli jimbo litarudi c.c.m 2015 lakini kama wapiga kura ni wana Arusha,basi ushindi wa Lema utakua zaidi ya 2010,tuombe uhai
 
Tukiwa ni wakazi wa Arusha tunakubaliana kwamba Arusha ni ngome ya CDM. Arusha ni jiji ambalo linaingiza pato la kutosha kwa Taifa. Lakini ndilo jiji pekee Tanzania ambalo halipangiki, halina barabara na wala haijulikani mpango wake wa kesho ni nini. Lakini kwa Mbunge wetu tunaona yuko busy na matukio yatakayomfanya awekwe ndani na polisi ili apate kura za huruma. Swali la kujiuliza
1. Majukumu ya mbunge ni yapi na Lema ametimiza mangapi.
2.Majukumu ya madiwani ni yapi na mbunge amewahamasisha madiwani wake kwa mangapi?
3.Je? tukimlinganisha Lema na Felix Mrema nani atakuwa amefanya mengi kwa maendeleo ya Arusha?
4.Je? Lema ndiye aina ya mbunge tunayemuhitaji?
naomba kuwakilisha

Mkuu ulichojaribu kukiainisha hapa kina ukweli kwa mantiki ya kwamba maendeleo ya mji yamedumaa esp.. kwenye eneo la miundo mbinu kama ya barabara.....ila tatizo sio la mbunge ni tatizo la uongozi kwa ujumla wake na hasa hasa baraza la madiwani lenye jukumu la kuisimamia manispaa kwa maana ya watendaji...kilichopo ni kwamba mji wetu hauna vipaumbele kabisa...kwa mfano kiasi cha hela kinachotumika katika kata zaote kutengeneza barabara kwa kiwango cha changarawe/vumbi, kingeekewa vipaumbele na kuachana na huo utaratibu wa kuchimba barabara na kumwaga changarawe kwa gharama kubwa, manispaa ingekuwa na uwezo wa kutengeneza japo kilometa mbili za lami kila mwaka ambazo ni jumla ya km kumi kwa miaka mitano..Jumla ya km 10 itamaanisha barabara karibia zote za hapa mjini zitakuwa zimefanyiwa kazi...kwa hyo madiwani wanatakiwa kukaa na kujadili maendeleo ya mji wa arusha kwa ujumla wake na sio kila mmoja kujadili kata yake....
 
Watu wa Arusha wana imani zao na wana amini mungu wao na si Lema ninachokiona hapa ulikusudia kuwatusi watu wa Arusha. Ukiona vijana hawana kazi wamekalia kunywa gongo na kuvuta bangi kwanza tuwapongeze hata kufanikiwa kupata hiyo pesa ya kununua gongo na bangi kwa maisha yalivyo magumu pili hili sikosa la Godbless Lema bali ni la serikali ya CCM amayo ilifunga viwanda vilivyoko hapa Arusha ambavya ni tegemeo kubwa kwa watu wa Arusha mfano General tyre lakini baada ya kuingia Lema sasa tumeanza kupata matumaaini GT imeanza kufanyakazi mbayo kama isingekuwa imefungwa ninaamini ingekuwa inategeneza tyre za africa mashaki na kati na kuna watu wangepata ajira kwenye kiwanda moja kwa moja au kwenye kilimo cha mpira na watu hao nao wangea ajiri watu hoko majumbani....Kwa hiyo basi tumpongeze kwa kufanikisha kiwanda hiki kufanyakazi ila tunamuomba afanye juhudi za kuhakikisha mali walizo uziana wafanya kazi wa zamani wa general tyre kwa bei ya kutupwa zinarudishwa mfano kuuziana gari kwa US$ 100( dola mia moja ) hii haikubaliki kabisa

hicho ndo tulichokuwa tunataka kukisikia toka kwenu wadau.
Haya zuri la kwanza tushalipata juu ya kiwanda cha general tair.

Mwagen na mazuri mengine siyo kulushiana maneno kama wanamipasho.

Arusha napapenda sana ila life lake limenishinda upatikanaji wa ankra ni mgumu sanaaa.
 
Tukiwa ni wakazi wa Arusha tunakubaliana kwamba Arusha ni ngome ya CDM. Arusha ni jiji ambalo linaingiza pato la kutosha kwa Taifa. Lakini ndilo jiji pekee Tanzania ambalo halipangiki, halina barabara na wala haijulikani mpango wake wa kesho ni nini. Lakini kwa Mbunge wetu tunaona yuko busy na matukio yatakayomfanya awekwe ndani na polisi ili apate kura za huruma. Swali la kujiuliza
1. Majukumu ya mbunge ni yapi na Lema ametimiza mangapi.
2.Majukumu ya madiwani ni yapi na mbunge amewahamasisha madiwani wake kwa mangapi?
3.Je? tukimlinganisha Lema na Felix Mrema nani atakuwa amefanya mengi kwa maendeleo ya Arusha?
4.Je? Lema ndiye aina ya mbunge tunayemuhitaji?
naomba kuwakilisha
Tatizo kubwa la magamba ni uwezo wa kufikiri. Walichoshindwa kukifanya kwa miaka 50 wanataka CDM wakifanye kwa siku 1. Godbless Lema kachaguliwa 31/10/2010 na kuapishwa mwezi mmoja baadae, amewatumikia wananchi miezi 13 tu mpaka sasa. Unamlinganishaje na Mrema aliyetumikia jimbo miaka 10? Mpango mbovu wa jiji si ni zao la Felix Mrema na magamba. Madiwani wengi ni magamba, Meya(By Force) magamba, huyo Lema atapata ushirikiano wa kutosha kweli? Lawama ni kwenu wenyewe kwa kuwa na "Double Standards", Ubunge Mpambanaji madiwani magamba. Tafakari.
 
hivi ni kweli JF kuna vichwa? yaani mbona hamtoi hoja? yaani wote mnadai nina chuki sasa hata kama nina chuki jibuni basi hoja ili ijulikane nina chuki! nina wasiwasi hata hamjui mbunge wenu kawafanyia nini! kama wa CCM hakufanya niambieni wa CDM amefanya nini?halafu swali jingine hivi tulimchagua Lema au CDM?
watu hawawezi kukupa hoja wakati wewe mwenyewe hujatoa hoja,wewe uliyeanzisha ndiye ulitakiwa uanze na hoja.mfano ulitakiwa utoe ulinganifu wa lema na wabunge wa ccm waliotangulia kwamba ndani ya miaka hamsini walifanya nini na lema kafanya nini kwa mwaka mmoja nanusu aliokuwa mbunge.kama hao waliotangulia wangefanya kama unavyotaka lema awe hakika ar ingekuwa moscow.jitahidi kuepuka emotions katika hoja yako,tawaliwa zaidi na reality.
 
Kuna mtu mmoja hapa naungana naye mkono kua endapo Lema angepewa ushirikiano basi jiji hili letu la Arusha tungekua mbali! Ni kweli kabisa lakini pamoja na Lema kutopewa ushirikiano katika kuleta maendeleo lakini tumeshayaona kama PJ alivyoeleweka na ukitaka kujua kwamba serikali ya ccm haipendi maendeleo angalia tokea utawala wa mbunge KINANA hakuna kilichobadilika Arusha, hususani mbunge Felix Mrema hali ni ileile! Ni bora tubaki na huyu kama mnavyomuita eti ni mvuta bangi pamoja na kumkwamisha huko lakini je tujiulize iweje sasa hivi ndio tuaona hali ya mabadiliko jiji la Arusha???
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom