Arusha - Je tunaridhika na utendaji wa Godbless Lema?


hivi ni kweli JF kuna vichwa? yaani mbona hamtoi hoja? yaani wote mnadai nina chuki sasa hata kama nina chuki jibuni basi hoja ili ijulikane nina chuki! nina wasiwasi hata hamjui mbunge wenu kawafanyia nini! kama wa CCM hakufanya niambieni wa CDM amefanya nini?halafu swali jingine hivi tulimchagua Lema au CDM?


Nionavyo hapo, una chuki binafsi.Nikuulize, unajua Felix Mrema alikuwa Mbunge muda gani?Ukiwa na majibu ujiulize yafuatayo
1: Alichokifanya,
2: Wabunge wa CCM wengi wanatekeleza yapi kama si Serikali tuliyoipa dhamana ya kutatua matatizo ya Watanzania.
3: Lema amekuwa mbunge kwa muda gani. Ukipata jibu, jiulize ni mangapi anayoweza kuyafanya yy kama yeye zaidi ya kufwatilia Mipango mikakati ya Serikali.
4: Kazi (majukumu) hasa za mbunge zaidi ya kuisimamia na kuiambia serikali matatizo ya wananchi wake.

Kama nikipata majibu hapo juu, moja bada ya moja niseme yafuatayo.Uongozi ni dhamana kwa kulinda na kutetea raslimali za wanyonge.Unapokuwa na uongozi madhubuti lazima gurudumu la maendeleo lisonge mbele.Hasa nini maana ya UTAWALA BORA.Je ni kuweka siasa mbele,ama kuwa na mikakati ambayo ni endelevu?.Ni bora kuwa na fikra za kimaendeleo zaidi kwa kuwa rasilimali tunayo isipokuwa "Poor ACCOUNTABILITY". "If the Goverment is 100% accountable we will see efficiency and effectively performance".Siasa ni siasa, ila tunaitaji mabadiliko ya dhati kupata maendeleo na kumwangalia mtu ama chama iwe CDM,CCM ama chochote kile si hoja ila Uwezo, Fikra endelevu na uwezo wa kuishauri na kutekeleza majukumu yake ndani ya Mikango mikakati ya Serikali.Tunaitaji kuwa na uongozi thabiti ili kusimamia raslimali tulizonazo na si kelele za kumwangalia LEMA kafanya nini ndani mwaka na nusu ss toka awe Mbunge.




Tunaitaji Fikra Endelevu na Mabadiliko ya kweli.
 
we Mpinga Uonevu watukane Wabunge 100 wa Magamba usimtukane mbunge wetu Lema..
Wana Jamvi mtakua hamjanielewa haaa lol
 
Tukiwa ni wakazi wa Arusha tunakubaliana kwamba Arusha ni ngome ya CDM. Arusha ni jiji ambalo linaingiza pato la kutosha kwa Taifa. Lakini ndilo jiji pekee Tanzania ambalo halipangiki, halina barabara na wala haijulikani mpango wake wa kesho ni nini. Lakini kwa Mbunge wetu tunaona yuko busy na matukio yatakayomfanya awekwe ndani na polisi ili apate kura za huruma. Swali la kujiuliza
1. Majukumu ya mbunge ni yapi na Lema ametimiza mangapi.
2.Majukumu ya madiwani ni yapi na mbunge amewahamasisha madiwani wake kwa mangapi?
3.Je? tukimlinganisha Lema na Felix Mrema nani atakuwa amefanya mengi kwa maendeleo ya Arusha?
4.Je? Lema ndiye aina ya mbunge tunayemuhitaji?
naomba kuwakilisha

Ni vizuri tusichange kazi za ubunge na zile za serikali. Mbunge ni mwakilishi wa wananchi kwenye chombo cha kutunga sheria (legislature), serikali (rais, cabinet etc) wanakuwa kwenye upande utendaji. Serikali inakusanya kodi, inapokea misaada, inapanga na kutekeleza (implement) miradi mbalimbali kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Mbunge sio afisa miradi, sio mpanga miji, sio mchimba visima vya maji, sio mjenga barabara. Pamoja na kwamba siku hizi watu wengi wanaonekana kudai mambo niliyotaja toka kwa mbunge lakini sio sahihi. Mbunge anatakiwa awakilishe kero za wananchi kwenye bunge/asimamie utekelezaji wa serikali (mkusanya kodi toka kwa wananchi).

Kama mbunge (e.g Lema) anatakuwa ndiye mjenga barabara basi hakuna haja ya kuwa na mkuu wa mkoa, mkuregenzi, Meya, na hata waziri wa ujenzi (i.e Magufuli).

Ingekuwa vema kama kwenye katiba mpya majukumu ya ubunge na serikali yakaandikwa in bold na iwe marufuku kwa wabunge kujigeuza afisa miradi. Nasema hili kwa sababu wabunge wamekuwa busy wanaomba hela badala ya kufanya kazi yao ya kusimamia serikali isifuje fedha za umma! Kama wabunge wangefanya kazi yao vizuri leo hii tusingekuwa na EPA, Rada, Meremeta. Kwa kuwapiga marufuku wabunge kuchanganya mambo tunaweza kuona mabadiliko kwenye usimamizi wao kwa serikali maana wanajua kama wataiachia serikali ifuje hela za wananchi basi miradi mingi kwenye majimbo yao itakufa.
 
Hili ni jukwaa la great thinkers....kwa heshima ya jukwaa hili tuwe tunatoa uchambuzi wenye hoja.Mfano kuhusu Mh.Lema,huyu ni mbunge kama wabunge wengine...kazi yake kuu kikatiba ni kuwakilisha kero za wananchi wake serikalini kupitia bunge,kushiriki katika utungaji wa sheria za nchi na kusimamia shughuli za serikali....sasa masuala kama ya kupata ajira,huu sio mzigo wake..ndo maana Lowassa huiambia serikali kuwa hili ni bomu.
Kuhusu suala la barabara halmashauri nyingi kwa sasa hazijapewa fedha japo wanajaribu lakini tunataka mbunge ajenge hizi roads kwa fungu lake.
Kabla ya kumfikiria mbunge fikiria kwanza serikali iliyopo madarakani na mfumo mzima wa uongozi wa juu!
 
Ilikuwa nianze na mambo mengine ila nimeona niahirishe kwanza nichangie hoja yako. Hoja umeifikiria vizuri ila nahisi umeshindwa kuipresent. Unauliza kama mnaridhika na utendaji wa Lema na kama anatimiza majukumu mliyomhitaji ayatimize. Je majukumu mliyompa ni yapi???ungeyataja hapa ili mchangia mada anayetaka kupima utendaji wa Lema imuwie rahisi. Lakini kwa kuficha majukumu mliyomhitaji kuyatimiza unakuwa hujafanya sawa mana huwez pima chochote hapa mana perceptions zetu kwa majukumu ya wabunge zinatofautiana sana na wengi wetu hatujui majukumu ya mbunge. Kimsingi wengi wanadhani mbunge ni mfadhiri, hii si sawa.

Aidha, umesahau kuwa Madiwani walikula kiapo cha kuutumikia Umma wao wenyewe na sio kwa kupitia ushawishi wa Lema. Kumbuka hapo Arusha kuna madiwani hadi wa CCM so ukitaka kumbana Lema kwa utendaji mbovu wa madiwani unakuwa hujamtendea haki. Maana hukumchagua diwani wa CCM kwa kushawishiwa na Lema,madiwani wa CDM ok ingawa napo hupaswi kuliweka hivyo. Kila mtu diwani/mbunge ana majukumu yake aliyoapa kuyasimamia ktk kipindi chake. So mtight kila mtu individually.

Lakini naona central question ulitakiwa kuuliza wanaarusha kama wanaridhika na utendaji wa Serikali ya Kikwete. Kumbuka jukumu la Lema ni kuisimamia serikali, kutunga sheria Bungeni, kuwakilisha interests za wananchi wake bungeni na kuhamasisha/kusimamia shughuli za maendeleo, so kama Serikali haina cha kufanya kwenye maendeleo nadhan kumnyooshea Lema kidole huwa tunakosea sana. Kuna dhana potofu iliyojengeka miongoni mwetu ya kudhania Mbunge ni mfadhiri. Jukumu kubwa la Lema ni kutunga sheria bungeni, nadhani kazi hii ameifanya kwa kuchangia hoja mbalimbali ktk misaada ya sheria mbalimbali kupita wabunge wengi tu pale mjengoni. Kuhusu jukumu lake la kuibana Serikali, hapo ndo usiseme na kwenye maendeleo sina takwimu za kutosha ila kupitia hapa JF tulielezwa he is doing well. Labda utabanaishe majukumu gani mengine zaidi ya haya mlitumana huko mtaani ndo tutaweza kukuelewa otherwise, utaonekana ni mjenga chuki miongoni mwa jamii sifa ambayo ni haipaswi kumilikiwa na kijana wa karne hii.

Kwa heshima naomba kuwasilisha.

nakukubali. hata hiyo JF SENIOR EXPERT naona wamekupunja unatakiwa upande zaidi!
 
Afanye nini lema kwisha habari yake hajui ashike wapi kama hujui angalia alivyoharibu kampeni Arumeru chadema imedorola kama uji wa jana. Mwanzo huo utasikia kimbunga kingine muda si mrefu. CCM oyee
 
swali la kujiuliza je hizo barabara zimeanza wakati wa Lema au zilikuwepo miaka yote? Je ni kwanini ccm hataki kuachia umeya wa mji? Wanajua kwamba kila maamuzi ya bajeti unafanywa kwa maamuzi ya baraza la madiwani na mwisho wanapiga kula kipi cha kufanya. Madiwani wa CDM wapo diluted tayari kwani madiwani 5 wapo agaist na chama na sitarajii kama watapiga kura infavour of cdm. La msingi ni kwamba kwa arusha kuna tatizo la ufisadi ndio maana ccm wametoa macho na hawakubali kushindwa hata kidogo na wanakwamisha makusudi maendeleo ili aonelane hafai na nzuri zaidi wananchi wenye uelewa wanalijua hilo lkn hawapendi kuonewa hata kidogo. Hvyo nadhani mkwamisha maendeleo ni ccm kwa kuwa ana ajenda ya siri nyuma yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom