ALEX PETER
Senior Member
- Jan 17, 2012
- 117
- 23
tukiwa ni wakazi wa arusha tunakubaliana kwamba arusha ni ngome ya cdm. Arusha ni jiji ambalo linaingiza pato la kutosha kwa taifa. Lakini ndilo jiji pekee tanzania ambalo halipangiki, halina barabara na wala haijulikani mpango wake wa kesho ni nini. Lakini kwa mbunge wetu tunaona yuko busy na matukio yatakayomfanya awekwe ndani na polisi ili apate kura za huruma. Swali la kujiuliza
1. Majukumu ya mbunge ni yapi na lema ametimiza mangapi.
2.majukumu ya madiwani ni yapi na mbunge amewahamasisha madiwani wake kwa mangapi?
3.je? Tukimlinganisha lema na felix mrema nani atakuwa amefanya mengi kwa maendeleo ya arusha?
4.je? Lema ndiye aina ya mbunge tunayemuhitaji?
Naomba kuwakilisha
mbona hoja zako hazijajitosholeza moja umeshindwa kuonesha wazi ni kwa vp lema siyo aina ya mbunge anayehitajika either kwa kutuonesha sifa za mbunge ambaye tunamuhitaji pamoja na sifa alizonazo lema ambazo zinamtofautisha na aina ya mbunge ambaye tunamuhitaji.
Mbili umeshindwa kuweka wazi data ulizonazo juu ya utendaji wa lema ukilinganisha na data za utendaji za mbunge anayehitajika.
Tatu umeshindwa kuthibitisha uwezo wa kusimamia ahadi alizoahidi lema ukilinganisha na mbunge unayemuhitaji umeshindwa kuwathibitishi wana jf mbunge bora ni yupi badala yake umetuachi home work tukufanyie hatuwezi kuwa taifa la majungu tofauti zetu za kiitikadi zisifanye tuhukumu hata pasipo hukumika umeona wapi lema amesema anaenda polisi ili kusudi apate kura za huruma kutoka kwa wananchi je ni mara ngapi lema ameenda polisi? Je waraka aliouandika kipindi yuko mahabusu pamoja na sababu zake uliusoma?