Patriote
JF-Expert Member
- Jul 13, 2011
- 1,718
- 1,047
Tukiwa ni wakazi wa Arusha tunakubaliana kwamba Arusha ni ngome ya CDM. Arusha ni jiji ambalo linaingiza pato la kutosha kwa Taifa. Lakini ndilo jiji pekee Tanzania ambalo halipangiki, halina barabara na wala haijulikani mpango wake wa kesho ni nini. Lakini kwa Mbunge wetu tunaona yuko busy na matukio yatakayomfanya awekwe ndani na polisi ili apate kura za huruma. Swali la kujiuliza
1. Majukumu ya mbunge ni yapi na Lema ametimiza mangapi.
2.Majukumu ya madiwani ni yapi na mbunge amewahamasisha madiwani wake kwa mangapi?
3.Je? tukimlinganisha Lema na Felix Mrema nani atakuwa amefanya mengi kwa maendeleo ya Arusha?
4.Je? Lema ndiye aina ya mbunge tunayemuhitaji?
naomba kuwakilisha
Ilikuwa nianze na mambo mengine ila nimeona niahirishe kwanza nichangie hoja yako. Hoja umeifikiria vizuri ila nahisi umeshindwa kuipresent. Unauliza kama mnaridhika na utendaji wa Lema na kama anatimiza majukumu mliyomhitaji ayatimize. Je majukumu mliyompa ni yapi???ungeyataja hapa ili mchangia mada anayetaka kupima utendaji wa Lema imuwie rahisi. Lakini kwa kuficha majukumu mliyomhitaji kuyatimiza unakuwa hujafanya sawa mana huwez pima chochote hapa mana perceptions zetu kwa majukumu ya wabunge zinatofautiana sana na wengi wetu hatujui majukumu ya mbunge. Kimsingi wengi wanadhani mbunge ni mfadhiri, hii si sawa.
Aidha, umesahau kuwa Madiwani walikula kiapo cha kuutumikia Umma wao wenyewe na sio kwa kupitia ushawishi wa Lema. Kumbuka hapo Arusha kuna madiwani hadi wa CCM so ukitaka kumbana Lema kwa utendaji mbovu wa madiwani unakuwa hujamtendea haki. Maana hukumchagua diwani wa CCM kwa kushawishiwa na Lema,madiwani wa CDM ok ingawa napo hupaswi kuliweka hivyo. Kila mtu diwani/mbunge ana majukumu yake aliyoapa kuyasimamia ktk kipindi chake. So mtight kila mtu individually.
Lakini naona central question ulitakiwa kuuliza wanaarusha kama wanaridhika na utendaji wa Serikali ya Kikwete. Kumbuka jukumu la Lema ni kuisimamia serikali, kutunga sheria Bungeni, kuwakilisha interests za wananchi wake bungeni na kuhamasisha/kusimamia shughuli za maendeleo, so kama Serikali haina cha kufanya kwenye maendeleo nadhan kumnyooshea Lema kidole huwa tunakosea sana. Kuna dhana potofu iliyojengeka miongoni mwetu ya kudhania Mbunge ni mfadhiri. Jukumu kubwa la Lema ni kutunga sheria bungeni, nadhani kazi hii ameifanya kwa kuchangia hoja mbalimbali ktk misaada ya sheria mbalimbali kupita wabunge wengi tu pale mjengoni. Kuhusu jukumu lake la kuibana Serikali, hapo ndo usiseme na kwenye maendeleo sina takwimu za kutosha ila kupitia hapa JF tulielezwa he is doing well. Labda utabanaishe majukumu gani mengine zaidi ya haya mlitumana huko mtaani ndo tutaweza kukuelewa otherwise, utaonekana ni mjenga chuki miongoni mwa jamii sifa ambayo ni haipaswi kumilikiwa na kijana wa karne hii.
Kwa heshima naomba kuwasilisha.