Arusha imekuzwa kuliko ilivyo!! ( Overrated )

Arusha imekuzwa kuliko ilivyo!! ( Overrated )

Wasukuma mnapenda ligi, Mwanza mtaendelea kuongoza in terms of population, lakini Arusha ni habari nyingine
 
Arusha wakati naingia,niliuliza wenyewe,hili ndio jiji? Ukweli haufichiki,Arusha bado haikustahili kuwa jiji ni sababu ya sifa za kijinga na machalii kujikweza hakuna lolote. Financially,msimu kama huu wa utalii ukiwa kwenye peak ndio Furaha na faraja ya vijana wa Mjini hapa. Hayo madini,yapo huko km kadhaa na hapa mjini wanaonufaika nayo ni hawa wachuuzi wa kimasai ambao nao ni balaa. Bhangi,wengi mnaijua ya Ngaramtoni,ila bhangi kali inatokea sehemu inaitwa kisimiri,huko kama huna kichwa nzuri kuvua nguo ni kugusa
 
Mtoa mada anakosea,hakuna jiji TZN la kulinganisha na Dar,huwa wanalinganisha majiji/mikoa mingine.Hata hivyo kuna hoteli kisasa zaidi na hadhi kubwa kupita mji/mkoa wowote wa TZN ikiwemo Dar lakini kwa ajili ya wazungu.By the way hali ya maisha/maendeleo na makazi ya individual ordinary people ni magumu ukilinganisha na maeneo mengi ya nchi,ndo maana nyuma tu ya hayo magorofa hapo mjini ni nyumba za matope balaa,wilayani huko ndo usiseme,huwezi linganisha na mikoa ya nyanda za juu kusini(Mbeya,Iringa,Njombe,Ruvuma,Rukwa,Katavi) ila wana hang over ya kudhania magorofa ya hapo mjini ndo maisha,wanavuta bange coz of life hardship stresses,tuwahurumie tu!
Kilimanjaro ndio mkoa pekee ulioendelea mpaka Kijijini wenye huduma zote kabla ya uhuru na baada ya uhuru na kama sio sera za uhujumu uchumi nafikiri ungekuwa mbali sana kuliko sasa mingine bado.Ukiniuliza mbona kuna maskini nitakujibu kwamba hata USA japo imendelea sana kuna maskini pia.
 
Tanzania bado inawatu wajinga kumbe.
 
Wanabodi habari zenu
Nilikuwa sijawahi kufika Arusha, tangu nikiwa sekondari mpaka chuo nimesoma na machalii mbalimbali toka mkoa huo wa Arusha, wamekuwa wanapasifia sana kama si mno.

Hata wadau mbalimbali waliowahi kufika wamekuwa wanapasifia sana ni pazuri na pamejengeka vizuri hata kufikia hadhi ya kuitwa " Geneva of Africa ". Pia uwepo wa makao makuu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, uwepo wa machimbo ya madini na sekta ya utalii imechangia sifa za Jiji hilo la Arusha kuzagaa mikoa mingine hali inayofanya kila mtu atamani kufika Arusha akiamini ni pazuri kama alivyohadithiwa.

Mungu si Athumani, nikapata safari ya kwenda Arusha wiki iliyopita, MAMA YANGU!! Sikuamini macho yangu, ni sehemu moja ya kawaida sana tena sana. Kwanza hapo wanapopaita Mjini ni pa kishamba sana, Stand ya mabasi ni kawaida yaani hata stand ya daladala ya Mbezi ni nzuri.
Majengo yenyewe ni ya kuhesabu hapo katikati ya mji.

Nikaingia sasa maeneo kama Sakina, Moshono, Njiro pakawaida sana, nikaamini mkoa ni mkoa tu!! Jiji kama lile kuna hiace zile fupi ndio zimejaa mpaka kero, huko Ngaramtoni kuna vumbi ambalo sijawahi kuliona kabisa. Bei ya vitu ndio usiseme yaani kitu cha kuuzwa elfu 5 utaambiwa elfu 30. Hata viwanja vya kijanja vya kujirusha Arusha ni vya kuhesabu na ushamba mwingi sana.

Kitu pekee cha kujipongeza na kujisifu kwa watu wa Arusha ni uwepo wa mbuzi choma kwa Mrombo, baasi hiko ndio nimeona tu!! Kwa maneno mengine Arusha ni overrated region.
Mkuu acha ushamba, hujui indicators of development! Maendeleo ya sehemu hayapimwi kwa vumbi na wingi wa magari
 
Nasisitiza Arusha life ni gumu sana kuliko pahala popote Tanzania,income gap/disparity ni kubwa mno,watu wachache wamehodhi ardhi kubwa ordinary people wanasafa,hang over ya magorofa ya mjini inawapumbaza while the masses are toiling,nasisitiza Arusha ni poor kuliko mikoa ya nyanda za juu kusini,huku kwetu hakuna magorofa marefu kwa ajili ya watalii maana magorofa sio kipimo cha ubora wa maisha ila kuna kuna huduma zote tena nzuri kuliko Arusha,nimesema safiri from kia to karatu,then from iringa to njombe/tunduma ufanye eye observation ya makazi ya watu kwenye miji na vijiji alafu usema wapi kuna maendeleo
https://www.google.com/url?sa=t&sou...ggwMAg&usg=AFQjCNE-qWAtFgAoT3KbbmQHJogt0llO2Q
 
Nasisitiza Arusha life ni gumu sana kuliko pahala popote Tanzania,income gap/disparity ni kubwa mno,watu wachache wamehodhi ardhi kubwa ordinary people wanasafa,hang over ya magorofa ya mjini inawapumbaza while the masses are toiling,nasisitiza Arusha ni poor kuliko mikoa ya nyanda za juu kusini,huku kwetu hakuna magorofa marefu kwa ajili ya watalii maana magorofa sio kipimo cha ubora wa maisha ila kuna kuna huduma zote tena nzuri kuliko Arusha,nimesema safiri from kia to karatu,then from iringa to njombe/tunduma ufanye eye observation ya makazi ya watu kwenye miji na vijiji alafu usema wapi kuna maendeleo
Umenena!
 
Kilimanjaro maendeleo vijijini mapaka mjini, kuna jamaa yangu wa kusini nilitoka nae Mo town naenda marangu akawa ananiuluza tunaenda vijijini o mjinii.....alishangaa sana maendeleo yaani majumba mazuri katikati ya migomba...
 
Tuachie Arusha yetu aiseee,naona baada ya kuona vitu bei juu ukashindwa nunua basi waleta hasira zako
 
Tatizo wewe umeishia stand ..kuna satellite cities Arusha ...ambazo DAR hakuna......inategemea mwenyeji wako
Sasa mkuu wewe nae una overate muda huu,Satellite city unajua ni nini au unasema tu.
Tena Arusha ndio inaweza kuwa ya mwisho kupata hiyo kitu madheee.
Arusha ni Jiji la Kawaida sana tena sana,na mfumo wa maisha ni wa ujanja sana kama vile upo Soweto vile.Ni watumiajia ambao wanajua kwamba kesho watapata tena.sio watu wa future plans unless kwa wale waliopo nje ya Arusha.
Na ndio maana hao matajiri wao wengi,utafutaji wao wengine ilibidi watoke wajifunze kuweka akiba kwa malengo.
 
Ukitaka kujua uzuri wa Arusha mtafute mfanyakazi wa ICTR aliekuwa Arusha na Muda wake ukaisha akatakiwa kuondoka ndio atakwambia uzuri au ubaya wake. Siku nyingine njoo na wako umpendae kisha uende viwanja ndo utajua ushamba wa watu wa Arusha. Hata hivyo yategemea uzuri wa mji nini katika mtazamo wako.
 
Ni kweli kabisa kaka kuifananisha arusha na nyanda za juu kusin ni sawa na uuaji kabisa na si kuua tu bali dhambi ya uuaji yenyewe.

Maana nyanda za juu kusin haina maghorofa,maeneo ya utalii kama arusha,sio kitov cha Africa na wala watu wake hawafanan kabisa na watu wa arusha.

Mikoa ya nyanda za juu kusini kwanza kumebarikiwa,watu wake wana mcha na kumjua MUNGU kwa % kubwa.

Wanajituma kutafuta maisha ,hawana sifa mbaya zaid ya upungufu wa kibinadamu,wakarimu,

Wanamshukuru MUNGU kwa kile wanacho kipata kwa 7bu wao hawafanani na wengine.

Mungu kawabarikia uzao wa vyakula vya aina zote hata kufikia kulisha taifa ni heshima ya pekee sana.

Wana akili ya utafutaj kwa jinsia zote na ardhi yao inasadifu yaliyomo nn utafute huko ukose?

Maisha yao ni yakawaida na fedha yao haishikwi na watu wachache na ndio mana si ajabu kusikia mboga sh.200,hata mtu wa bajet ya 3000 kwa siku anaish.

SI UMEONA UTOFAUTI????KWELI HUWEZI KUFANANISHA NA ARUSHA MKUU
ni kweli mikoa uloitaja inaongoza kwa uzalishaji wa chakula ila pia inaongoza kwa idadi kubwa ya watu (hasa watoto) wenye ukosefu wa lishe bora (utapiamlo) ndo mana ni dhambi kufikiria kufikiri kuilinganisha na arusha
 
Wanabodi habari zenu
Nilikuwa sijawahi kufika Arusha, tangu nikiwa sekondari mpaka chuo nimesoma na machalii mbalimbali toka mkoa huo wa Arusha, wamekuwa wanapasifia sana kama si mno.

Hata wadau mbalimbali waliowahi kufika wamekuwa wanapasifia sana ni pazuri na pamejengeka vizuri hata kufikia hadhi ya kuitwa " Geneva of Africa ". Pia uwepo wa makao makuu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, uwepo wa machimbo ya madini na sekta ya utalii imechangia sifa za Jiji hilo la Arusha kuzagaa mikoa mingine hali inayofanya kila mtu atamani kufika Arusha akiamini ni pazuri kama alivyohadithiwa.

Mungu si Athumani, nikapata safari ya kwenda Arusha wiki iliyopita, MAMA YANGU!! Sikuamini macho yangu, ni sehemu moja ya kawaida sana tena sana. Kwanza hapo wanapopaita Mjini ni pa kishamba sana, Stand ya mabasi ni kawaida yaani hata stand ya daladala ya Mbezi ni nzuri.
Majengo yenyewe ni ya kuhesabu hapo katikati ya mji.

Nikaingia sasa maeneo kama Sakina, Moshono, Njiro pakawaida sana, nikaamini mkoa ni mkoa tu!! Jiji kama lile kuna hiace zile fupi ndio zimejaa mpaka kero, huko Ngaramtoni kuna vumbi ambalo sijawahi kuliona kabisa. Bei ya vitu ndio usiseme yaani kitu cha kuuzwa elfu 5 utaambiwa elfu 30. Hata viwanja vya kijanja vya kujirusha Arusha ni vya kuhesabu na ushamba mwingi sana.

Kitu pekee cha kujipongeza na kujisifu kwa watu wa Arusha ni uwepo wa mbuzi choma kwa Mrombo, baasi hiko ndio nimeona tu!! Kwa maneno mengine Arusha ni overrated region.

hata mim nasikia mwanza inasifiwa yeyo
 
Kinachokera Arusha ambayo ni lazima wakazi wake wabadilike ni tabia ya KUTEMA MATE OVYO BARABARANI. Ukitembea kwenye kwenye lami unaweza kuhisi kulikuwa na manyunyu ya mvua usiku.
 
Upanuzi wa barabara kutoka tengeru mpaka sakina ulioanza tangu mwaka jana na unaendelea so point yako kwamba watu hawataki barabara zitanuliwe ni upotoshaji
na sifa zote hizo ndio barabara inapanuliwa mwaka jana!??na hizi feeder roads kuelekea makazi ya watu kiwingine ambako hata gari haziwqez pishana!??c'mon,wacha ushabiki usio mantiki jamaa
 
na sifa zote hizo ndio barabara inapanuliwa mwaka jana!??na hizi feeder roads kuelekea makazi ya watu kiwingine ambako hata gari haziwqez pishana!??c'mon,wacha ushabiki usio mantiki jamaa
Km ipi ambayo gari haziwezi kupishana au unaongea tu kufurahisha kijiwe.
 
Kinachokera Arusha ambayo ni lazima wakazi wake wabadilike ni tabia ya KUTEMA MATE OVYO BARABARANI. Ukitembea kwenye kwenye lami unaweza kuhisi kulikuwa na manyunyu ya mvua usiku.
Labuda sirkali ipige marufuku ngisuji (ugoro)tofauti na hivyo kutema mate lazima
 
Back
Top Bottom