DOKEZO Arusha: Changamoto wanazopitia abiria wanaotumia Kituo Kikubwa cha Daladala Kilombero msimu huu wa mvua

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,253
Kituo kikubwa cha daladala kilichopo Kilombero karibu kabisa na Soko la Kilombero jijini hapa kimegeuka kuwa kero kubwa hasa kipindi hiki cha mvua kutokana na kukosekana kwa sehemu ya kujikinga mvua kwa abiria wanaotumia kituo hicho.
Kilombero.jpg

Muundo wa kituo hiki umejengwa kama uwanja wa mpira na sio kama kituo cha daladala kama vilivyo vya mikoa mingine, alisema mmoja wa abiria aliyekuwa kituoni hapo. Na kuendelea kusema kuwa halmashauri ya jiji inatafuna tu pesa na kusahau kuboresha miundombinu muhimu wanayotumia wananchi.

Kituo hicho cha daladala kutokana na kukosekana kwa miundombinu muhimu, maji ya mvua yamekuwa yakitwama katika eneo hilo na hivyo kusababisha kuwa tope katika eneo hilo.

Ikumbukwe kuwa msimu huu wa mvua hakuna sehemu yoyote abiria anaweza kujificha mvua ndani ya kituo hicho.

Mbali na hilo pia ndani ya kituo hicho hakuna taa zozote hivyo basi wakati wa usiku madereva na abiria kushindwa kutumia kituo hicho cha daladala kuanzia saa moja jioni kutokana na giza na wingi wa vibaka wanaoibia abiria pindi giza liingiapo
 
Back
Top Bottom