Liam Rosemary anadai staff wa Arsenal waliingilia upande wa timu yake ikiwa inafanya mazoezi. Lakini video inaonyesha staff wa Arsenal akienda upande huo kuufuata mpira na hakukua na mchezaji wala staff wa Chelsea.
Upande mwingine Pep na wenzake wakaandika barua kuomba usajili mpya uliokuja baada ya first leg uruhusiwe kucheza fainali. Ingawa kanuni zinasema hairuhusiwi.
Leo jumamosi zinachezwa mechi saba mtu ana options za kuangalia mechi zaidi ya moja ila atasema mechi ya Arsenal inaboa. Na timu ndiyo zinakuja kama Chelsea.
Pundit mmoja akasema anaamini Newcastle anatakiwa kutafuta ushindi na aende akiwa hot. Ndani ya dakika 30 tie ikawa imeisha, dakika ya 32 wakaanza kulia.
Dakika ya 45 mi nikalala.
John Terry anapost video anasema haina haja ya kushangilia sana kombe lenyewe ni Carabao tu. Kama ulikua mdogo utakua hujawahi kumuona akiwa anashangilia Carabao mpaka Mourinho akagalagala chini, au kama huna mb utakua hukuona akiwa anafanya live streaming ya dk za mwisho akihisi Chelsea inapata goli kumbe ni goli la Arsenal.
And that fool had no shame and called that goal offside.