Nilikua X jana nikakuta shabiki wa Barcelona anasema itapendeza kama Arsenal itakutana na Barcelona kwenye hatua ya nusu fainali au mtoano.
Mashabiki wenzake wakaanza kumjibu "This Arsenal team should be avoided at any cost" mwingine akamjibu "Hatuna defense nzuri na Arsenal ina defense nzuri, wanashambulia vizuri na wazuri kwenye set pieces ambazo Inter alitusumbua nazo. Kwa kifupi Arsenal hii ni Inter ya mwaka jana inayotumia steroids"
Mwingine akajibu "At best tuingie na suicide mode kama ile ya Inter, piga nikupige tutakapoishia ndiyo hapo hapo"
Mwingine akasema "Hatuna defense ya kuizuia Arsenal wakati defense yao ni best in the world kwa sasa"
Generally ilikua ni mashabiki wa Barcelona kupoint kwamba hawana defense nzuri wanategemea mno attack ishinde nyingi.
Matokeo ya jana ya Slavia vs Barcelona na rekodi yao ya kuconcede inaonyesha jinsi gani mashabiki wa Barcelona walikua wakweli katika kuichambua timu yao.
Nikiwa X pia nikakuta kuna shabiki wa Liverpool amesema Arsenal akichukua kombe atakua the worst champion in history. Kisha mwenzake akamtumia screenshot akiwa anatoa remarks kipindi kile Liverpool inaongoza ligi, alisema kwamba "Huu ni msimu wetu, tukipoteza ni sisi wenyewe kwa sababu City ipo hovyo msimu huu anayeweza kututisha kidogo labda Arsenal"
Chid Benz kwenye ngoma yake kali kabisa inaitwa "Ngoma itambae" maarufu kama "Dar es Salaam Stand Up" alikua ana kionjo kinasema "Wanakubali kiaina"