Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Baada ya game ya leo ya Villa na Everton sasa Villa kadrop points 8, City 9 na Arsenal 4.

Kiazi kimoja kilipiga hesabu ya Villa kuifunga Everton ili akae mkiani kwa Arsenal.

Nikisema hawajui mpira wanakasirika
 
Zimebaki mechi 16.

Mfano Villa na City wakachafukwa kila mmoja akashinda games zote zilizobaki Villa na City watapata points 91.

Arsenal akishind mechi 14 atakua na points 92 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote. Start the countdown
 
Mechi ya Kesho na Inter haina muhimu Sana kwetu.Arteta achezeshe kikosi cha pili apumzishe wachezaji muhimu maana jumapili tunahitaji point 3 kwa lazima.

Mechi na Inter tukipoteza hakuna tatizo
 
labyrinth nilikwambia Haaland asipofunga Man city huwa wanastruggle Sana kupata matokeo bt ukakaza fuvu nadhani mwenyewe umeona kinachowakuta huko.

Kuhusu beki za Man City Josko Guvardiol msimu wake ndo umeisha hivo mpaka next season ndo arudi uwanjani.
Stones sio wa kumtegemea kbsa kwa sababu huyu ni trip moja uwanjani trip nyingine wodini.
Dias atakuwa nje kwa zaidi ya week sita na kabla anarudi nadhani tutakuwa tushacheza na City
 
Hili kombe linatutaka ni ujinga tu wa kocha wetu.

Angetuliza akili au akituliza akili kombe atabeba mapema sana ili awekeze Uefa na makombe mengine.

Mwisho wa msimu ni ngumu sana kupambania makombe yote kama kocha mbinu kisoda.Inahitaji kocha haswaa kuweza kufanya hilo.

Viwango vya wachezaji wa Arsenal eneo la ushambuliaji ni takataka sana hawana muendelezo.

Lingine odegaard sijui kampa nini yule kocha wetu.Kiukweli ni mchezaji wa kawaida hana uhatari huo.

Kama Arsenal tungekuwa na yule njino au sura ya kizezeta Bruno Fernandez lile eneo la Odegaard basi tungewapima vizuri sana kina Gyokeres kama wanajua kupasia au vipi.

Ukiangalia city Halaand anapata nafasi nyingi sana jambo ambalo hauwezi kuliona kwa Gyokeres.Nshaona zaidi ya mara moja jamaa akikaa kwenye eneo zuri lakupiga pasi hawampi.

Sasa sijui ndio maelekezo ya mwalimu hata sijui.

Ule upande wa Trosard na Martinel ndio upande unaotukwamisha zaidi katika kikosi bila kusahau yule captain asiestahili.

Rice ndio mtu anaestahili kuwa captain kikosini na ni aibu Rice kuongozwa uwanjani na kiande aina ya Odegaard.

Kama atabadilika basi na mimi tabadili maoni yangu ila Ode ni miongoni mwa wachezaji waliotukosesha furaha hii misimu iliyopita.
 
Style ya uchezaji wa Arsenal ndio inamkwamisha Gyokeres.
Gyokeres akienda Manchester United atashine Sana kwa sababu ya Ile mipasi hatari ya Bruno.Jamaa sio mbaya vile watu wanafikiria
 
Unazungumza kuhusu kombe 😆😆 nadhani tukihesabu kwa miaka 21 hii makombe ya arsenal na arsenal fans walioujiua sababu ya false hopes unahisi idadi itakua vipi?
Narudia Tena....tukishanyanyua kwapa May....binafsi ntakutumia barua ya mualiko uje ule ubwabwa ikibidi nyumbani kwangu tufurahie ubingwa.....maana nahisi mara ya mwisho tunabeba hii EPL itakuwa ulikuwa hujazaliwa bwana mdgo🤠🤠
 
Narudia Tena....tukishanyanyua kwapa May....binafsi ntakutumia barua ya mualiko uje ule ubwabwa ikibidi nyumbani kwangu tufurahie ubingwa.....maana nahisi mara ya mwisho tunabeba hii EPL itakuwa ulikuwa hujazaliwa bwana mdgo🤠🤠
Kwapa gani mnanyanyua nyie maandazi. Kimahesabu mna nafasi kubwa sana ya kutoka mikono mitupu. Lower your expectations usije ukapata magonjwa. Ni ushauri tu.
 
 
Zimebaki mechi 16.

Mfano Villa na City wakachafukwa kila mmoja akashinda games zote zilizobaki Villa na City watapata points 91.

Arsenal akishind mechi 14 atakua na points 92 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote. Start the countdown
Kuna mpwa kasema huko juu Arsenal kama timu na mashabiki mna comedy sana, hakika nimeamini.
Kila la kheri mabingwa 25/26 😁😁
 
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…