Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Kilichobaki tujadili msimu ujao tu,
What if tukamsajili dembele, merino afundishwe kucheza 6 alafu rice acheze cm
Then tutafute 9 wakueleweka, havertz awe anapokezana na rice au uyo 9.
At the same time nwaner awe intergrated zaid kwenye AM
Baada ya kukosa vyote
Stori za msimu ujao zinaanza tena
Kweli aseno ni Netflix iliyochangamka
 
Arsenal wanaendela kujipiga wenyewe na butwaa kwa msimu wa tatu huu mfululizo and they shamefully act surprised na matokeo ya jana
 

Attachments

  • Screenshot_20250508-112556_Instagram.jpg
    462.1 KB · Views: 10
Unataka UEFA na Saka ? Odegaard? Mna kichaa kabisa,,, ! Tottenham anaweza kuchukua kombe, wanalandani wenzenu, hakuna rangi mtaacha kuona,,,, ama United mbovu tunayoiona anaweza pia kuchukua kombe na akahesabika kuwa na msimu bora kuliko nyie !
 
Hongereni Arsenyo kwa kufanikiwa kuingia fainali Uefa women's champions league.
 
Mimi ni United, shida ya Arsenal si kwamba ni timu mbaya hapana ni timu Bora sana, lakini wanachokosa Arsenal ni ile Personality na Maturity, unajua kwenye mpira kuna ile mentality Fulani ya kubeba majukumu as if una share ya umiliki kwenye timu, kama utakuwa unaangalia vizuri na unaujua mpira bila mapenzi utaona timu zote zinazochukua makombe zina hizo sifa, unaweza kuona timu hii mbona haichezi vizuri lakini inachukua makombe ni kwasababu ya burning desire iliyo kwenye mioyo ya wachezaji.

Vipaji na mifumo haitoshi, Inahitaji uwe na wachezaji wa aina hiyo ambao wao Kila nafasi ama dakika ina maana kwao, Juzi Inter Milan na Barca Kila timu ilikuwa inajua muda wowote tunaweza kufunga goli, Kila mara ni keep pushing, Sasa Arsenal wao wanafuata tu njia za kocha na kucheza vipaji vyao lakini wamesahau kuwekeza kwenye akili, pindi tu Arsenal players wakiwa na ile akili ya kibingwa watavunja gundu lao na kufika mbali sana.

Arsenal wameziacha mbali timu nyingi hasa kiuchezaji, Inahitaji uwe na timu kuifunga Arsenal. Vipaji na mbinu havitoshi , good personality ndiyo iliwafanya Madrid wachukue UEFA back to back na si kwamba Zidane alikuwa ni kocha Bora sana hapana bali wale jamaa Kina Toni kroos, Modric, Cristiano, Casemiro, Ramos, Marcelo walikuwa wanajua tunaenda kufanya Nini kiasi ambacho hata bila kocha wanacheza.
 
Kiuhalisia Arteta hawezi kuipa Arsenal kombe la maana labda itokee bahati mbaya.

Ukiangalia namna wachezaji wa Arsenal wanavyocheza katika mechi muhimu unaona kabsa kiakili wanafanana na kocha wao.

Yule mtoto Myles skells jana alikuwa na siku mbaya sana kazini kapoteza mipira mi4 ambayo ilikuwa inaleta hatari kwa Arsenal lakini kocha alikuwa katulia tu anaamini mambo yapo sawa huku Enrique anamwambia dembele pasha uingie.

Namna Arsenal jana walivyokuwa wanacheza ni kama vile watarudiana na Psg mara 20 ndio bingwa apatikane sio knock out ya mwisho.

Enrique alionesha mbinu sio mbwembwe huku Arsenal wanaonesha mbwembwe sio mbinu.Jana katika set pieces Psg alikuwa bora zaidi ya Arsenal.Hapo nkajua kazi hakuna tena.
 
Arteta ni mwanafunzi wa Pep kwa asilimia kubwa, hili halina ubishi. Amechukua mbinu nyingi toka kwa Pep akiwa City iliyokuwa na Gundogan, Silva, Bernado, KdB, Aguero, Mahrez, Sane, n.k. Na pengine ameangalia mbinu za Pep akiwa Barca iliyokuwa na Xavi, Messi, Busquet na Iniesta. Kwa lundo la talents kama hizi Pep alikuwa hatumii nguvu kubwa kufikisha ujumbe wake kwa wachezaji na matokeo yanapatikana. Ndio maana jamaa hakuwa anawekeza sana kwenye CF kwenye timu zake.
Ila sasa Arteta anataka kucheza bila CF (eti Merino/Kai) halafu support ya attacking brains inatoka kwa Odegaard, Martinelli, Saka na Rice.

Mngechukua kombe ilikuwa dhihaka kubwa sana kwa ulimwengu wa mpira. Kila siku humu tunawaambia tatizo ni Arteta, ninyi mnawalaumu Kroenke.
Rice sio mchezaji wa 105miliions, hana tofauti na Henderson wa Liverpool ambaye media za uingerezz zilitaka apewe Ballon d Or
 
Timerlane nakubaliana na wewe. Kinachoigharimu Arsenal kwa sasa ni hofu ya kisakolojia ya kushinda makombe, ubora wa Arsenal ndani ya hii misimu 3 ni mkubwa mno. Mshambuliaji wa kati pekee hatoshi kubadili psychological fear.

Confidence huja hata kwa kubeba vikombe vidogo vidogo kama FA na Carabao ila ukikaa muda mrefu bila kikombe hata uwe na ubora mkubwa kiufundi wachezaji wanakuwa hawana ile mentality ya kushinda makombe.
 
Kina Masingeli wenyewe wanakwambia Tetea ndie mwalimu wa Pep

Project ya Mikel Arteta ndani ya Arsenyo inafikirisha sana, sidhani kama inaweza kukumbukwa na kupewa heshima na mashabiki wa soka kwa kila msimu kumaliza mikono mitupu.
Tetea anapaswa kulaumiwa sana na mashabiki wa Arsenalia kwa timu kutokubeba makombe.
Kila mwisho wa msimu mashabiki wanakua na matarajio makubwa ya msimu ujao bila ya kuwaza msimu unaofata wapinzani nao wanajipanga ili warejee wakiwa washindani wa kweli.
Kuna timu 2 kati ya Chelsea, Manchester na Spurs zina nafasi kubwa ya kubeba ndoo msimu huu, hivyo watakuwa na msimu Bora kuliko Arsenyau na Tetea wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…