Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Leo hata kuangalia mechi sikua na huo mpango ila Fotmob nimesubscribe timu 3. Taifa Stars, Arsenal na Sheffield.

So notifications za hizi timu hua zinakuja tu. Ikanialert in 15 minutes game inaanza mi nikawa nacheki game ya Lecce na Napoli. Hii mechi kwetu haina faida, mshindi kashajulikana, mtu wa kwanza mpaka wa tano anaenda CL so ukimaliza second na Forest akamaliza 5th wote mnakutana CL.

Nikapata alert Rice kascore.

Nikapata alert Bournemouth kascore.

Nikapata alert Bournemouth kascore ila VAR inacheki goli.

Jumanne si tutabanduliwa kama ndiyo hivi
Braza umesubsrcibe mpaka matakataka ya Taifa Stars??? 😂😂😂😂😂😂😂
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Hii timu kuanzia mwanzo wa msimu mpaka game ya 28 inaitwa Arsenal, zikibakia game 10 za mwisho inabadilika na kua Arsenalia, Jukwaa linageuka kutoka furaha na kua vilio.
Sasa kama Bournemouth tu anawapiga nje ndani, kweli jumatano mtaweza kupindua meza kwa ile mijitu ya miraba 6 pale Parc des Princes?

#Arsenalia
1740382991259.jpg
 
Huyo Saka mnayemuona ndio star men wenu ambaye mlikuwa mnaamini akiwa fit mnachukua EPL tangu amerudi amewasaidia nini ??

Mmebahatisha point 9 kwenye possible 18 points na Saka akiwemo.
 
wadau wa mpira tuliliona hili mapema sana sasa nyie arsenal jumaa tano mnaingia na fatigue kidogo wakati wenzenu 98% ipo reserved mazoezini huo mpira wa comeback mnaofikiria sio rahisi kiivyo japo kwenye mpira lolote linawezekana

Tactic approach ya arsenal itakuwa sawa na approach aliotumia kwenye mchezo wake na Liverpool ulioisha
2-2 pale Emirates walianza kwa kasi ya ajabu kutafuta goli la lazima mapema ili wakae kwenye mfumo wao kilichotokea ikawa piga ni kupige hawafikiria hili linaweza kutokea huko ikitokea wamepata bao la mapema kwamba nao psg wata react na mchezo kuzidi kuwa mgumu kwa arsenal mlima wa aggregate kuzidi kujaa
na hio mechi itakuwa ngumu kwenu sababu huku epl bado hatujamalizana na nyie nafasi ya pili kushuka chini mpaka wa 7 mmepisha point 10 soo hamuwez zarau mechi za ligi huku wenzenu kama kawaida yao wanaweka 1st squad yote bench maana washa beba kombe watakuwa wanacheza 30 mins for match fitness tu sio kukamia then baada ya hapo wanaingia fresh kuwakamia watu waliotoka kwenye fatigue ya kugombania top 5 epl

mbona kazi bado mbichi hii
 
Arsenal inamtaka Rodrygo wa Madrid. Rodrygo ametaka aongee kwanza Xabi ili ajua kama ana uhakika wa namba kisha afanye maamuzi.

Starting price ni 100M
 
City iliona mambo hayaendi. January akatumia 250M ili apate nafasi ya kucheza CL.

Arsenal tukaona mambo hayaendi. Ili kushindania kombe la ligi na CL hatukusajili mchezaji yeyote January
 
Kwako wew unaona rodrygo anafaa kuichezea arsenal
Very tricky question.

Rodrygo ana skills, analijua goli, anaweza take ons na dribbles na ni shooter mzuri. Ila Rodrygo siyo finished article, so akija Arsenal atatakiwa kuadopt.

Kwa 100M kumleta mchezaji ili aadopt ni uchizi, pili kama Arsenal kweli tunahitaji makombe wachezaji wa mpaka waadopt siyo option tena.

Swali lako linakua tricky kwakua ni kama linamaanisha "Yanahitajika makombe, Rodrygo ni mchezaji sahihi?" Hapa sasa ndiyo kujibu swali inakua ngumu. Ni mzuri ila ana uzuri wa kutosha kuleta instant impact? Hapo sina uhakika. Ila kama anakuja wakurupuane na Martinelli ni sawa
 
Umejibu vizury kiongozi, itakua lengo moja wapo ni ushindani wa namba kama hapo ulipogusia kwa martinelli.
 
Ni kivipi Brighton ameweza kuscore dk ya 28 dhidi ya Newcastle na akalinda goli mpaka dk ya 88?

Game management ya Arsenal is worrying. Miaka miwili nyuma Arsenal ilikua inaweza kuiongoza timu pinzani goli mbili na mechi ikaisha suluhu. Zikatoka lawama swala likaisha.

Sasa huku mwisho limeanza upya.

Na kitu kimoja. Kama unahisi Arteta ni tatizo technically nakuhakikishia jamaa anaweza kutoka Arsenal na akaenda timu nyingine na akafanya vizuri. Mshkaji siyo mbaya ila financial backup ya bodi ni kichomi.
 
Ndiyo tunaambiana bahati ina mchango kwenye tournaments.

Yaani kwenye ligi Arsenal imepigwa, Spurs imesuluhu na Nyumbu kafa ila mpaka sasa mathematically Nyumbu ana chance ya kuchukua kombe.

Nimeona online wameraise ishu moja hivi kwamba once Arsenal tulimaliza nje ya top four na tukashinda FA ila aliyemaliza ndani ya top four akasema kafanikiwa kuliko Arsenal.

As of now, Arsenal anaweza kumaliza ndani ya top four ila spurs au nyumbu akachukua trophy. Mashabiki wa hizi timu mbili wanasema kama watachukua trophy na Arsenal akamaliza ndani ya top four ila asichukue CL basi Arsenal atakua na msimu mbovu kuliko ambaye atachukua Europa.

Kwanza nataka niseme kwamba tayari nyumbu msimu wa juzi walichukua trophy huku Arsenal tukiwa wa pili na wakasema wana msimu successful kuliko tuliomaliza wa pili. Kwa msimu ule hata mimi nikaona nyumbu hawajielewi. Coz ile trophy kwa Arsenal ni nyumbani.

But this time around hawa watu mmoja wao ana chance ya kutembea na Europa cup na utakutana naye CL. Yaani anamaliza nje ya top ila unakutana naye CL huku ana kombe la Ulaya. Na unahisi umefanya poa kumzidi? How?

Kwa kile kikombe cha mwanzo niliwaona miyeyusho, but kwa sasa kwenye Europa yeyote kati ya spurs au nyumbu akiondoka na Europa anakua amefanya successful campaign kuliko Arsenal.

Hii ni kutokana na hadhi ya trophy yenyewe. Swala la wakija watakua mnazi wa uwani hilo ni juu yao ila ni wazi watakua wamefanya poa kutuzidi
 
Ni kivipi Brighton ameweza kuscore dk ya 28 dhidi ya Newcastle na akalinda goli mpaka dk ya 88?

Game management ya Arsenal is worrying. Miaka miwili nyuma Arsenal ilikua inaweza kuiongoza timu pinzani goli mbili na mechi ikaisha suluhu. Zikatoka lawama swala likaisha.

Sasa huku mwisho limeanza upya.

Na kitu kimoja. Kama unahisi Arteta ni tatizo technically nakuhakikishia jamaa anaweza kutoka Arsenal na akaenda timu nyingine na akafanya vizuri. Mshkaji siyo mbaya ila financial backup ya bodi ni kichomi.
Financially Arteta amebebwa kuliko managers wengine wote wa arsenal tangu zama za Wenger. Nadhani katika kila nafasi uwanjani arsenal ina watu wazuri kwa standards zenu kasoro eneo la CF. Na hata hilo eneo inawezekana ikawa ushauri wa Arteta ili kutengeneza muscles za kushindana kipindi cha summer.

Ni maoni yangu tunapoelekea kupindua meza paris.
 
Financially ukimfananisha na makocha wa Arsenal ni sahihi. Ila ukimfananisha na timu zingine ni msiba.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom