By default Inter atacheza low block na kurely kwenye counter. Naassume Barcelona watarely kwenye hizi cross na wings ili kuisasambua hii defense.
Sisi pia tulijaribu hivyo dhidi ya Inter na tukatoka kapa. Tukatoka na possession ya 63% total shots 20, on target 4, off target 6 na shots 10 zote basi Lao lilihakikisha haupiti mpira wowote.
Tukawa na big chances 3 na zote tukamiss. With Barcelona hizi big chances 3 inawezekana 2 au moja ikamkuta Lewandowski, so obviously Barcelona ana chance ya kupita simply kwakua ana striker, na ni bonge la striker mshkaji.
Ni ngumu kwa msimu huu sisi kucheza na low block teams simply kwakua hatuna ST. Naona Barcelona akipita kwenye hii tie.