Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Nyie Kima najua kabisa nyinyi ni wasindikizaji na lazima mtatuangusha.
Hivi mmeshavuta picha msimu huu makombe ya Uefa, Europa na Conference Leagues yote yakitua England tutakua tumeiheshimisha Epl kwa kiasi gani?
 
Kijana acha kuwafokea mabingwa wa Europa.
Ikifika May ndio utajua tofauti ya mafanikio ya Man Utd mabingwa wa Europa 2024/2025 na Arsenyau bingwa wa top4 na uefa semi final.
Kwamba mwanaume mzima unajisifia kushiriki Europe league michuano ambayo eti washindani wako ni mid table teams kwenye ligi zao kama Athletic Bilbao,Frankfurt,Sevilla,Roma na Lyon????? Hauoni aibu?

Hauoni kwamba sasa hivi umoja wa manyumbu(nyumbu united) tayari na yenyewe imeshakuwa midtable team? Na ndio maana mnashiriki european secondary competition?

Ukishaona mashindano ambayo timu kama Bayern munich,PSG,Inter,Real madrid yaani european heavy weights hazishiriki basi ujue hiyo ni michuano ya watoto, na hautakiwi kabisa kujivunia hata ukiichukua michuano hiyo mara kumi

Wewe unafikiri ni kwanin Sevilla pamoja na kuchukua michuano hiyo mara nyingi lakini hawaheshimika kama moja ya timu kubwa ulaya? Kwa sababu ni bingwa wa michuano ya watoto.

Sasa kumbe nyumbu siku hizi mnajivunia kurudi utotoni? Haya hongereni
 
Arsenyau acha kudharau kitu ambacho kuanzia wewe, baba yako na babu yako wote hamjawahi kukimiliki.
Wewe hauna tofauti yoyote na yule anaemcheka na kumdharau mwenzake anaemiliki Ist wakati yeye tokea azaliwe na ukoo wao wote hawajawahi kumiliki hata funguo ya bodaboda.
We Kima nionyeshe timu yako imebeba kombe lolote la ulaya halafu mimi nikuonyeshe paka mwenye vichwa vitatu.
 
Point kali sana hii.
 
Tuseme zile kelele za kumtukana Kroenke na Arteta kwa kutosajili dirisha dogo la januari zimeishia wapi?
Je, ikitokea kama zali mkabeba UCL bila striker bado mtaona kuna umuhimu wa kusajili striker dirisha lijalo?

Au ndio kusema na nyie mmefika mliopofika kama bahati tu kiasi kwamba mkiambiwa mrudie itakuwa kipengele?
 
Arsenal akichukua CL bila ST itakua ni generational story, considering majeruhi aliyoanza msimu na yakaendelea mpaka msimu unaisha.

Itakua ni achievement kubwa kwa kuzingatia hata kikosi chetu cha invincible kilishindwa hiki kitu. Itakua ni best story ya kuhadithiana muda wa jioni vijiweni. Ila ni inamaanisha kusajili kuko palepale

Kama nyinyi mkirudi CL kwa mlango wa nyuma wa kuchukua Europa. Itakua the best underdog story.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…