Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Angepgwa risasi kwa lipi? Kutoa red card au kwa kuruhusu mpira uchezwe kabla Walker hajaenda kwenda nafasi yake au kuacha ile faulo ya Martinel kwa Herdason.
Kwa hyo refa asubiri mpaka mjipange ndo apige filimbi?

Huyo fala Michael Oliver wewe ndo humjui labda. Juventus hawana hamu naye 2018 nusu fainali.

Ni refa bogaz kabisa
 
Ta

Tafuteni mwalimu wa nidhamu mapema, la sivyo kila mechi mtapoteza mchezaji kwa red card. Sheria ya kupiga mpira mbali baada ya refa kupuliza kipenga imetiwa mkazo msimu huu.
Hiyo sheria haina consistency kwa timu zingine ni Arsenal tu.

Ngonjera zako hapa siyo mahali pake
 
Tumechafua social networks jana. Wana hasira sana kama polisi wa nchi fulani EA na raia wa chama fulani πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ

Ushauri kwa ndugu zangu Gunners, leo ukitoka usivae jezi ya Arsenal, wanaweza kukuteka hawa.

Viazi vinalalamika jana Kai Havertz hajapiga complete pass hata moja. Huu ndo UHARAMU FOOTBALL, UNDAVA tunaouzungumzia sasa.
 
Duuh! Kweli nyakati zinabadilika.. Man city leo anashangilia draw kama amechukua ubingwa dhidi ya timu pungufu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜€πŸ˜€.. Hawatosahau hili haram football la leo
Haland alikuwa haamini anachokiona ulimi njeπŸ˜€πŸ˜€...
 
Nottingham Forest alikukojolea sebuleni kwako Anfield kenge wewe
 
Hawa ilikuwa tunawapiga leo, halafu tunasubiri adhabu yao, tupewe makombe yao na washushwe maharaja.
Ila bado ligi bado mapema. Hata tukifungwa leo bado mwisho wa msimu ndoo yetu.
Acha utoto arsenal ichukue kombe la wapi subirini city wanyang'anywe point ndio njia rahisi ya arsenal kuchukua kombe sio uwanjani.
 
Majirani walitamani tule hata kono la nyani lakini wapi *****....mwezi wa 12 wte rasmi watajiunga na kipara guardiola kutuzuia....ligi huwa inaanza huo wakati.....sasahivi eti Chelsea naye wa Tano sijui....ukiona hvyo uje bdo bado ligi haijaanza....ikishaanza utaona tu Manunu na Chelkenge wanapokezana zile nafasi zao pendwa pale kati 8 na 9
 
Msimu uliopita Arsenal tukiwa tunacheza na City Kovacic akapata yellow kisha akafanya kosa jingine akatakiwa kupata yellow nyingine.

Refa hakutoa yellow ya pili.

Alipokuja kuulizwa baadaye akasema angetoa ya pili angeinfluence mechi yote.

Jana usiku Trossard akagewa yellow mbili na kuinfluence mechi nzima.

Refa ambaye aligoma kumpa Kovacic yellow ya pili ni Michael Oliver.

Refa aliyempa jana Trossard kadi mbili za yellow ni Michael Oliver.

Go figure
 
Suala sio kufananisha matukio yaliyokwishatokea na ya jana, tuangalie sheria inasemaje mchezaji anapopiga mpira mbali baada ya mwamuzi kupuliza kipyenga.

Tatizo lemu AssAnal mnasahau mapema, huwa mnaanza ligi kwa kiherehere kama hivi ila mwishoni ulimi wote nje. Ni nini kinawapa tumaini kuwa msimu huu utakuwa tofauti na misimu mingine yote iliyopita mkawa mnataga?
 
Twende taratibu, ushabiki maandazi weka pembeni.

Wazungu wanasema hivi "In association with International Football Association Board (IFAB) guidance to enhance effective playing time, referees will caution(yellow card) players when they are deemed to have delayed the restart.

A player will be cautioned if they are guilty of delaying the restart of play or failing to respect the required distance when play is restarted with a dropped ball, corner kick, free kick or throw-in."

Cheki hapa chini, Doku makusudi kabisa, anapiga mpira wakati Arsenal wamezawadiwa free kick. Kwa mujibu wa maelezo hapo juu na ya kwako, Doku ilibidi awe cautioned na yellow card. Refa alitoa kadi?

Tuje kwa tukio la Trossard. Tukubaliane wote, Trossard alicheza foul kwa Silva. Baada ya foul Trossard aliwahi mpira, na kuupiga mbele ili Martinelli awahi ule mpira. Lengo sio kuchelewesha muda. Nimekuwekea picha hapa chini. Refa akatoa kadi.

Mechi Ile Ile, maamuzi tofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…