Miguu ya Jesus tu.
Kuna kitu kimoja, inatarajiwa mtu mfupi mikimbio yake inakua ya mkupuo kuliko mrefu. Mfano waliwahi tabiri mikimbio ya Martinelli itaathirika baada ya kuongezeka urefu ila imekua tofauti.
Tuje kwa Kai.
Wakati yupo Ujerumani hakua mrefu sana, ilimwezesha kunyumbulika kwa urahisi na kufanya runs za msingi zilizofanya awe hatari mpaka kenge wakamtamani wakampeleka darajani. Urefu kaanza kuupatia pale hivyo runs na unyumbulikaji ukapungua, plus uchezaji wa Kenge ukazidi kumfanya awe isolated.
Arsenal tumemchukua Kai, ana miaka 24, ana chansi ya kurefuka zaidi. Kuna picha moja yupo na Mertesacker gunners wa Reddit akasema sasa hapa ndiyo naelewa Kai ni mrefu kiasi gani. Per ni giant ana 6'6 lakini kamuacha Kai points 2 tu.
This means urefu wa Kai ni ishu kwenye acceleration na ishu kwenye unyumbulikaji, nafikiri ndiyo maana hata headers siyo mzuri ingawa ni mrefu.
Jana baada ya kutoa pasi kwa Trossard aliyekua anakimbia kumpa msaada Trossard nadhani ni Martin. Urefu wake unamzuia kuaccelerate fasta na kunyumbulika bila kumshtukia tofauti na Leandro, Martin, Partey, Jesus, Saka na wengine.
Haya ni maoni yangu