āš»Control spaces , shinda mipambano yako , fanya runs nzuri , kuwa sharp uwanjani ni vitu ambavyo wamefanya kwa usahihi sana dhidi ya Newcastle leo na kuwafanya vijana wa Eddie Howe kucheza mdundo wao
āš»Distance : Hii kitu muhimu sana , jinsi Arsenal walivyohakikisha distance kutoka mstari mmoja mpaka mwingine na mchezaji kwa mchezaji kuwa ndogo sana , faida yake ?
1: Iliwanyima muda na nafasi kwenye mpira Newcastle na kushindwa kupita ndani . Matokeo yake wakalazimishwa kufanya makosa au kupiga mipira mirefu ambayo Arsenal ilikuwa rahisi kwao
2: Inasaidia sana kufanya pressinf nzuri haraka pale walipokuwa wanapoteza mpira
3: Inasaidia ku control mechi kwasababu inakupa options za pasi ambazo sio za umbali mrefu hivyo mpira kutembea vizuri
āš»Yes najua kuna namna makocha wanasisitiza timu kuanza nyuma lakini kama pasi haipo kwanini usianze mipira mirefu kwa mawinga halafu uanzie hapo ? Newcastle mara kadhaa walijipiga risasi mguuni kwa risk pasi zao hasa ukizingatia Arsenal walikuwa sharp sana
āš»Arsenal waliwaonesha Newcastle sura yao ya pili kwamba nini wanaweza kufanya wakiamua kukabia chini ... compact 4-4-2 ambayo inafunga spaces , ndani hakuna njia , Newcastle walipata tabu sana kuwafungua Arsenal hasa kwa kutumia ile silaha yao ya combination play ( Bruno - Trippier - Almiron )
NOTE
1: Jorginho ali control sana mchezo hasa kipindi cha kwanza , simple passing na humuoni akiliacha eneo lake tupu
2: Arsenal kwenye mipira iliyokufa š„ hakika Nicolas Jover anafanya kazi vizuri
3: Leo Arsenal walikuwa wanacheza kama vile wana hasira na Newcastle , mbinyo huo š„š
4: Sifa ya Newcastle ya msimu uliopita ya kuzuia vizuri msimu huu imepotea ... wameruhusu magoli 4 mechi kadhaa mpaka sasa
5: Bukayo Saka sasa hivi ukijaa tu kwenye mfumo unaokota kambani
6: Licha ya kurusu magoli 4 lakini performance ya Karius huwezi amini kama alikuwa hachezi š¤
7: Mbio za ubingwa bado za moto sana
FT: Arsenal 4-1 Newcastle