.
[emoji1593]Listen .! Najua kazi ya namba 9 / straika ni kuweka mpira wavuni ( na katika timu kubwa ndio rada inakuwa kubwa sana kwako kufunga mara kwa mara ) ... So Yes najua hilo ni eneo ambalo Gabriel Jesus anatakiwa kuboresha ( ana miaka 26 sasa )
[emoji1593]But kuna vitu anafanya uwanjani ... vinakunyanyua kwenye siti yako au vinakuacha mdomo wazi na pengine Arsenal wanahitaji namba 9 mwingine ili Jesus atumike eneo lingine la uwanja ( Kulia au kushoto pembeni )
1: Dribbling ( mpira unakuwa karibu sana na kiatu chake sio chumba kizima [emoji3])
2: Workrate yake akiwa uwanjani ( anakupa 100%)
3: Uwezo wake wa kuvuruga muundo wa ulinzi wa timu pinzani ( destabilization) kwa :- Movements, Flicks , Dribbling , Pace
4: Kuna hii ambayo naamini wengi wanachukulia poa , Jesus ana uimara mzuri wa kimwili kukabiliana na challenges / mipambano ( duels ) dhidi ya mpinzani wake
Kiufupi General Play yake ipo katika level nzuri sana ngumu kuifumbia macho :
VITU AMBAVYO VIPO HASI KWAKE
1: Majeraha
2: Umaliziaji wake sio wa ufanisi sana akipata nafasi
NOTE
Leo najua mashabiki wengi wa Arsenal watakuwa wanadumisha undugu wa jiji moja la London na Chelsea [emoji3]
Baada ya wao jana kuwafundisha Man United jinsi gani ya kumfunga Notts Forest katika uwanja wao .!
Ila yule AWONIYI , Arsenal mkae chini mmalize tofauti zenu . Ameshafanya kuwafunga Arsenal kama kitu cha kawaida , halafu kumuweka Saliba pembeni vile na kuuwa mali chini na kutumbukiza kambani ndio tabia gani ile ?[emoji3][emoji3]
AMBANGILE